Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,573
- 134,177
Asavali hao ni bei poa inabidi tuwapongeza kutoka dolali 700 hadi 300 mungu akupe nini,sasa pasco unacholilia nini hilo shirika letu liko ICU,wacha nasi akina yakhe tukwee pipa ,gWanabodi,
Kuna hili nimelishuhudia kwenye usafiri wetu wa anga wa kimataifa, ndio maana nauliza ni tunaibiwa, au tunasaidiwa kwa sababu wenyewe hatuwezi?.
Kwenye usafiri huu wa kimataifa, kila nchi inapewa haki ya international routes na protection ya local routes ili kulinda mashirika ya nchi yasimezwe na mashirika makubwa.
Katika route ya Afrika Kusini, kuna shirika moja jipya linajiita Com Air linafanya biashara kubwa ya kusafirisha abiria kati ya Dar na J'burg kwa bei poa.
Nauli ya kawaida ya return ticket ya Dar-J'burg -Dar ni Dola 700 lakini nauli ya Com Air ni Dola 300!.
Ndege inakuja Dar mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Inatua saa 7:30 za usiku na kutuka saa 8:30 za usiku, yaani inakuja na kuondoka kama mwizi!.
Mahali tunapoibiwa ni hapa!. Kumbe hili shirika linalojiita Com Air, sio lolote, si chochote bali ni Ndege ya BA inayotoka London kupitia Dar kuelekea J'burg!.
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za usafiri wa anga, ndege inayopitia Tanzania kwa utaratibu wa Via, hairuhusiwi kubeba abiria local, inatakiwa kushusha tuu na kuendelea na safari yake badala ya kusanya abiria wa Tanzania kwa nusu bei!.
Inawezekana wizi huu unafanywa kwa nia njema kwa vile flag carrier yetu ATC haina uwezo wa kupeleka ndege yake ya ngama safari ndefu, hivyo BA imeamua kuokoa jahazi japo kwa kijiita Com Air matokeo yake ni kuwa hata ATC ikifufuka, itaishia kukosa abiria kwa sababu haitaweza kihimili ushindani huu wa nusu bei!.
Pia ikumbukwe Tanzania hatuna tena ile route yetu ya London bado inahodhiwa na SAA kwa kisingizio cha kifidia hasara iliyosababishwa na Alliance Air!. Sasa hata ATC ikifufuka, itapumulia wapi?.
Kitu kingine kibaya kabisa hawa Com Air wanachowatendea Watanzania ni menu yao ya ndani ya ndege. Wanatangaza kuwa ni beef lakini menu inayokuja ni sausages za 'mkuu wa meza'!. Masikini wenzetu kwa vile hawawezi kuzijua, hujilia kwa imani beef ya wenzetu ni nyeupe, laini na ina ladha sana!. Japo mimi ni Mkristu lakini hili sio kuwatendea haki wenzetu.
Nawasilisha.
Pasco
Pretoria.
KyelaBoy, ndio maana nikauliza kama ni tunaibiwa au tunasadiwa?.Asavali hao ni bei poa inabidi tuwapongeza kutoka dolali 700 hadi 300 mungu akupe nini,sasa pasco unacholilia nini hilo shirika letu liko ICU,wacha nasi akina yakhe tukwee pipa ,
Tena wa bongo hatuhitaji viza. Yaani kuja South na kurudi ni bei poa kuliko kwenda Mwanza au Arusha na kurudi?. Swali sanya sanya za ndege zinaruhusiwa?.Duu mkuu inabidi niwatafute hao com air nije sauzi kutembea manaake nauli bei poa kama vile basi
Hii ni habari nyeti sana na ya kiintelijensia, inayotakiwa KUFANYIWA KAZI mara moja na TCAA.
Actually kilichotakiwa kufanywa ni kuwashitaki hawa jamaa ili waache mchezo huo, na kuwa severely fined..
Hairuhusiwi kabisa kupakia abiria enroute!...labda aBiria hao wawe wanaenda kwenye final destination ya ndege hiyo, na si vituo vya VIA...vinginevyo hiyo inakuwa ni daladala, na inapoteza ile sifa maalum ya usafiri wa anga ya fastness , reliability and comfortability..
Otherwise mashirika yanayo'emerge yasingesimama kwa miguu yao ever!
gWanabodi,
BA imeamua kuokoa jahazi japo kwa kijiita Com Air matokeo yake ni kuwa hata ATC ikifufuka, itaishia kukosa abiria kwa sababu haitaweza kihimili ushindani huu wa nusu bei!.
Pia ikumbukwe Tanzania hatuna tena ile route yetu ya London bado inahodhiwa na SAA kwa kisingizio cha kifidia hasara iliyosababishwa na Alliance Air!. Sasa hata ATC ikifufuka, itapumulia wapi?.
TANMO, kweli ATC bado iko ICU, lakini kama ni kusaidiwa, si tusaidiwe basi angalau na Precision!Mkuu madam ATC bado ipo kaburini basi tuendelee kuifaidi hiyo Ofa "isiyo halali" tuliyobahatika kupewa na BA. Ila tukisema tupige kelele ofa ifungwe bado tutakaoumia ni sisi. Unless unajua ni lini ATC itafufuka na una uhakika beyond any doubt kuwa itafufuka kweli kwa sera tulizonazo....
Kaizer, sijatia chumvi, hizo ni beef sausages jina, ila you can not tell kitu ambacho hujawahi, hebu nenda pale Mlimani City kanunue beef sausages za ukweli na zile nyingine, chemsha halafu kula, utaniambia. Zile nyingine wanazitia spice hivyo za beef ni chamtoto!Ila mkuu Pasco apo kwenye beef sausages umetia chumvi sana bana...yaana wajamaa wanazifurahia kabisa ladha yake? hahahah
Kusema ukweli unapoangalia mashirika ya wenzetu , unajiuliza how long it will take kwa ATC kurudi kwenye its senses....hivi ni lazima kuwa na shirika la ndege la taifa?
Du siku hizi 540 na Precision ni kama kampuni za simu,bei ya promo hadi mwanza 98,000 hakika ushindani mzuri precision siku hizi wamepata mpinzani wa ukweliWe panda hiyo ya US$ 300 achana na wezi ATC watupu, wala usimwambie mtu.