Nani alipanda basi la mdundiko na machimukenda, express za kugombania ukishindwa sana unaanza mdogo mdogo town hadi nyamanoro, hadi ufike umepaukaaaa, kweli mwanza imetoka mwanza
Ningeshangaa kutokuonekana kwenye huu uzi...Mwanza Mwanza
Nimepanda magari ya Sadoti enzi hizo dereva akiwa 'kaka Mafyale'.. bahati mbaya sana huyu mzee alifilisika vibaya na kwa sasa amezeeka kweli.
Kuna express moja ilikuwa inapiga route za Mwaloni - mjini inaitwa MAJIRA...
mambo mpango ..coaster hiyo enzi hizo ilionekana gari ya maana sana
Digidigi zilikuwa zinafanya service kabla na baada ya safari mitaa ya Nera (home place) pale.
nimefungua thread kwa shangwe nikafikiri umeweka picha za treni.
jana nimefurahije Pinda kuturekebishia reli ya Dar-Mwanza. Raha sana kusafiri na treni.
back to topic: ok i dont know what u guys are talking about
Nakumbuka coaster zilivyoanza, zilikuwepo coaster za kwenda pasiansi ziliitwa Mayeji, ilikuwepo mayeji 1 hadi mayeji four, watoto wa mwanza seco wakaachana kabisa na habari ya chai maharage
Mwanza seco unanikumbusha ghuba na vulumai zake na mwalimu kinshuli
Mwalimu mafuru mzee wa history.. mihogo ya mama jamila kweli wewe wa enzi zetu.Wali sangara ilikuwa sangara kweli..majonzi yalikuja siku headmaster kitereja alipotangaza wataanza kupika ugali badala ya wali:A S wink:kumbe umepita pale mkuu, chezea wali na sangara/maharage, kinshuli yupo bana juzi tu ijumaa nimemuona town kachoka kweli mwalimu wetu, namtafuta mwalimu mafuru jamani sijui yuko wapi huyu. Unakumbuka mihogo ya mama Jamila?
Mwalimu mafuru mzee wa history.. mihogo ya mama jamila kweli wewe wa enzi zetu.Wali sangara ilikuwa sangara kweli..majonzi yalikuja siku headmaster kitereja alipotangaza wataanza kupika ugali badala ya wali:A S wink:
Unapotaja Nyamanoro unanikumbusha vitu vingi sana! Enzi hizo pale Seleman Nassoro vijana wanakaa na makoleo na majembe kufukia mashimo barabarani kisha kurushiwa shilingi tano na makonda km mchango wa kurekebisha barabara.Nani alipanda basi la mdundiko na machimukenda, express za kugombania ukishindwa sana unaanza mdogo mdogo town hadi nyamanoro, hadi ufike umepaukaaaa, kweli mwanza imetoka mwanza
Hiyo treni unayosema hg, usiombe kusafiri na daraja la 3 maarufu kama sogea tukae, unaweza kulia
ahahahahhh, duh umenikumbusha mbali aisee, mmiliki wa majira tulikuwa tunaishi nae jirani mtaa wa azimio. Mmoja wa watoto wa sadoti alimuoa mwalimu wangu wa hesabu enzi hizo mwenge primary, basi mwalimu alikuwa anajidai huyo babamkwe ana express
Ooh atakuwa kaka Mafele maana ndo alioa mwalimu.. nakumbuka harusi ilikuwa CCM Kirumba miongoni mwa wavaa sare alikuwepo mama yangu.... Miaka hiyo Sadoti alikuwa Sadoti kweli yaani (kuanzia mjini kila mtu alimfahamu)ukipata mgeni unamwambia wewe ulizia kwa Sadoti ukifika hapo basi ulizia mama fulani utafika.
Umeona eeh...! Hivi hiyo familia ya mzee sadoti bado wako hapo kirumba sokoni?
Ndio bado wako hapo ingawaje kuna watoto wake wawili wa kike walifariki na mjukuu wake wa kike.
Inaelekea tunafahamiana maana enzi hizo sisi tulikuwa tunaishi jirani kabisa na mzee Sadoti.
Ndio bado wako hapo ingawaje kuna watoto wake wawili wa kike walifariki na mjukuu wake wa kike.
Inaelekea tunafahamiana maana enzi hizo sisi tulikuwa tunaishi jirani kabisa na mzee Sadoti.
inawezekana mamiii, hebu kesho tukutane PM nitakapokuwa kwenye pc