Usafi wa mikono baada ya kutoka haja

Usafi wa mikono baada ya kutoka haja

Juzi kati niliona mama lishe katoka chooni nikajisikia kichefuchefu na kuacha kula hapo. Hili andiko ni kama lilinijia kabla ya kulisoma hapa. Kuhusu yale makopo ya chooni kila mtu anachambia hayako salama kuna uwezokano mkubwa ukaambukizwa fangasi ukaishia kuja kuwashwa sehemu za siri
 
Hivi wakuu hili suala la kwenda haja kubwa, halafu wakati wa kuchamba mtu anashika shika mavi ili kujiosha mnalionaje?

Ukweli ni kwamba wengi wamelishwa mavi. Huwezi kusema wote hujisafisha mikono vizuri na maji ya kutosha na sabuni au ikiwa wote hunawa na sabuni.

Na wengine hujisafisha na maji ya ndoo ya chooni au kopo la chooni linalotumiwa na wengi. Tena utakuta ni maji kidogo sekunde 2 tu mtu kashamaliza kunawa anarudi jikoni au kwenye mgahawa anaendelea kuaanda chakula au kupakulia chakula wateja wake. Hivi kweli kuna usafi unazingatiwa hapo?

Unakuta mmama au dada wa nyumbani ambaye ndiye mpishi wa familia akienda chooni anajisafisha kwa njia hiyo hivi kweli mna uhakika huwa hawawalishi kinyesi walaji?

Ifikie wakati huu utamaduni wa kuchamba kwa kushika shika kinyesi Watanzania waachane nao. Unatia kinyaa sana.

Ni kweli mkuu ,mama lishe wengi wachafu ,wanatulisha VIMA na MIJOKO ,ukiacha hayo pia wanatulisha SABUNI ,maji ya kusuuza vyombo ni kuanzia asubuhi mpaka lukwiri hayo hayo.
 
Ndio maana ni muhimu sana kunawa kwa sabuni kila mara ila Watanzania wengi huwa hata hawanawi kwa sabuni!
Kwanini kashfa hii mmeamua KUWAPA watanzania pekee au kwa kuwa tunaishi nao...me sidhani kama nchi za Africa zinatofautiana sana na za Asia naona mambo ndo hayohayo tu
 
Yaani labda kwenye ma vyoo ya maofisi wakiweka sabuni na sanitizer watu hukumbuka ila SIO vyoo vya majumbani na vya kulipia stand huko noma
Huko ni Mungu saidia tu

Mimi wakati wa kula ikiwa kuna cha kupakua au kukata kama kijiko, kisu au upawa wa kushea ili mtu ajikadirie msosi wake kwenye sahani yake huwa natumia mkono wa kushoto

Au kwenye yale mabufee ya kujisevia natumia mkono wa kushoto

Kwa sababu ule upawa, kisu au kijiko unakuta kimeshikwa shikwa na wengi hutumia mkono wa kulia
 
Back
Top Bottom