Jimama la North dakota limekupa karatasi na wewe unataka ufanyie biashara....Ni PM basi....
sidhani kama unaomba paper alafu wanyamwezi wakupe vitu kama hivyo....msoma madela- Malipo ya safari, DAR to NY nani atalipa
- Malipo ya visa nani atalipa
-Malipo ya nyumba, transport za hapa na pale nani analipa
-Mfano nilikuwa nafanya kazi Dar tuseme eg. Care International kama miaka sita, je wanatambua hili na kunipa kazi equivalent na hiyo.
- Je, nikitaka kujiendeleza naweza kupata sponsor au najisomesha mwenyewe.
-Je, kuna allowances zozote mtu hupata kutoka kwa hao watu wanaoendesha hiyo green card lottery.
Nilishinda DV Lottery miaka kama 10 iliyo pita.
Kabla sijaja majuu nikajitolea kuwaelekeza watu wengi namna ya kucheza, wengi wao walinielewa lakini walikuwa na swali moja kubwa sana.
Ukishinda wanakutumia Tiketi ya ndege?
Nikawauliza anaye taka kwenda America ni wao au ni wewe?
Nikaambiwa Sasa bila Tiketi nitakwendaje na faida yake ni nini? Au unatuficha namna ya kupata tiketi?
Wewe tiketi umepata wapi?
Nikawaeleza namna nilivyo jikusanya na kugharamia safari yangu.
Jibu la mwisho likawa.
Ah! kama ndo hivyo si heri nibaki Bongo tu.
Sasa kama Watanzania walio wengi wana mawazo kama hao nilo kutana nao mimi DV Lottery is not for them.
Hakuna ujanja wowote katika hili,watanzania wengi hatukuwa na mwamkoThanks Ogah
Kila mara nikiangalia nimegundua kuwa ni wakenya wengi wanaopata hizo greecards, watanzania ni wachache sana, sanasana ni wahindi wanaojiita watanzania ndio wanapata hizo greencards nilikuwa nadhani kuwa labda wao wanatumia ujanja fulani kushinda, any idea?
Wamarekani Wapuuzi kweli.......wameninyima kijani.....kwanza ri nchi lao uchumi sasa hivi si mzuri..
Suala la wingi au uchache wa Watanzania wanaoshiriko Green Card Lottery si muhimu, inawezekana WaTz wengi hawataki kushiriki.
Kwani kuna jambo gani la kutufanya WaTz wengi kuikimbia nchi yetu? Hapa bado tuna opportunities nyingi sana za kufanikiwa kuliko kwenda huko USA na kuwa vibarua. Hatuna cha kutukimbiza hapa. Angalia Waethiopia jinsi walivyopata kwa wingi. Inaonekana wengi wameshiriki hiyo Bahati nasibu na wanastahili maana hali ni ngumu sana kwao. Udikteta na uchumi mgumu.
Braza BAK ntakutafuta kwa ufafanuzi zaidi wa hii kitu. Haya maelezo ya wadau hapa sijaelewa na pia najua kutakuwepo na mabadiliko mengi tu kwa miaka hii.Nadhani kuna upendeleo fulani wa baadhi ya nchi, Kenya ikiwa mojawapo. Miaka ya karibuni idadi ya Watanzania wanaoshinda bahati nasibu hii imeanza kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Lakini ni vizuri kuhakikisha unafuata masharti yote yaliwekwa ili kuhakikisha application yako haiwekwi kapuni.
Braza BAK ntakutafuta kwa ufafanuzi zaidi wa hii kitu. Haya maelezo ya wadau hapa sijaelewa na pia najua kutakuwepo na mabadiliko mengi tu kwa miaka hii.
Ngoja nitafute Mkuu kuhusu hii kitu kama nitapata chochote, lakini nina wasiwasi mkubwa huyu Rais wa sasa anaweza kuifutilia mbali ili kupunguza wimbi la wahamiaji. Nakumbuka humu kuna mdada alijaribu miaka michache iliyopita lakini hakufanya mapema akasubiri hadi karibu na deadline. Siku hiyo ya deadline tuma tuma na wewe nadhani kulikuwa na watu wengi sana na ile web site ikaelemewa au ilicrush. Basi akaniomba nami nimsaidie kutuma tulihangaika sana kwa masaa nadhani mawili au matatu mpaka tukafaniwa na alifanikiwa kuwa mmoja wa waliochaguliwa.
Asante kwa dondoo bro.. Ila kwa sasa hivi nahisi kutakuwepo na mabadiliko mengi sana ya kiutaratibu kulinganisha na miaka ya nyuma... Hebu fanya kucheki utaratibu ukoje now kwanzia hatua za awali. Huyu raisi akiifuta tutamwachia nchi yake ya viwanda na ntajaribu hata nikiwa kama raia wa Madagascar.
Kikubwa ni kupeana taarifa tu mkuu ASAP, kuhusu kuweka taarifa za uongo siwezi fanya hicho kitu. Always niko serious kwenyw vitu serious na hii kitu nilitaka kushiriki hata mwaka jana ila sikupata mtu wa karibu anaeujua huu mchezo vizuri wa kunielekeza. Mwaka huu acha nataka nijaribu. unavyosema kwamba huyu jamaa anaufuta huu mchezo, hata mimi nna mashaka lakini tusiwe pessimistic kiivyo.Mara nyingi hata humu huwa zinawekwa zile link zao, na mara nyingi ambaye huziweka huwa ni MziziMkavu. Ila kwa ushauri wangu ukipata bahati ya kuapply usiweke chochote kile ambacho si cha kweli inawe kukugharimu ukabaki na majuto. Baadaye nikitulia Mkuu nitatafuta nadhani hii ndiyo miezi au inakaribia ya kutoa link ya kuweza kuapply kwa mwaka 2018, lakini huyu jamaa mpya nina wasi wasi anaweza kuifuta kabisa au kusema weusi wasiruhusiwe kutuma maombi.
Kikubwa ni kupeana taarifa tu mkuu ASAP, kuhusu kuweka taarifa za uongo siwezi fanya hicho kitu. Always niko serious kwenyw vitu serious na hii kitu nilitaka kushiriki hata mwaka jana ila sikupata mtu wa karibu anaeujua huu mchezo vizuri wa kunielekeza. Mwaka huu acha nataka nijaribu. unavyosema kwamba huyu jamaa anaufuta huu mchezo, hata mimi nna mashaka lakini tusiwe pessimistic kiivyo.
Sawa Mkuu kwa jinsi ninavyokusoma humu nakuona ni mtu makini na unayejitambua. Nilitoa tahadhari kutokana na kusema kwamba uko tayari kutumia hata uraia wa Madagascar . Link ndiyo hii hapa chini Mkuu ila usisubiri dakika za mwisho. Ingawaje nimesikia baadhi wanatuma maombi mara chungu nzima ili kuongeza probability ya kupata wenyewe wanadai tuma ombi moja tu. Kwa kuwa gharama zake ni ndogo sana sioni tatizo la kutuma maombi mara nyingi. Kila la heri na baraka Mkuu.
Electronic Diversity Visa Lottery
Thanks Ogah
Kila mara nikiangalia nimegundua kuwa ni wakenya wengi wanaopata hizo greecards, watanzania ni wachache sana, sanasana ni wahindi wanaojiita watanzania ndio wanapata hizo greencards nilikuwa nadhani kuwa labda wao wanatumia ujanja fulani kushinda, any idea?