Us Green Card Lottery

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,227
1,553
Bandugu,

Huwezi kushinda mchezo wa bahati na sibu kama hujacheza. Link zifuatazo hapa chini zitakuwezesha wewe kuingia ktk bahati na sibu hiyo BILA GHARAMA YOYOTE, angalieni asiwatapeli mtu....HAKUNA CHA AGENT................its very simple fuata maelekezo, fill in the forms tuma application yako instantly online:

fungua hii link ya kwanza halafu ujaze fomu, link nyingine mbili chini yake ni kukupa maelezo zaidi kwa ajili ya kuelewa nini unafanya: KUMBUKA KUFUATA MAELEKEZO especially ktk picha

http://www.dvlottery.state.gov/

http://travel.state.gov/visa/immigrants/types/types_1318.html

http://www.usimmigrationsupport.org/greencardlottery.html

Haya jamani Kila la kheri
 
Thanks Ogah
Kila mara nikiangalia nimegundua kuwa ni wakenya wengi wanaopata hizo greecards, watanzania ni wachache sana, sanasana ni wahindi wanaojiita watanzania ndio wanapata hizo greencards nilikuwa nadhani kuwa labda wao wanatumia ujanja fulani kushinda, any idea?
 
Nadhani kuna upendeleo fulani wa baadhi ya nchi, Kenya ikiwa mojawapo. Miaka ya karibuni idadi ya Watanzania wanaoshinda bahati nasibu hii imeanza kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Lakini ni vizuri kuhakikisha unafuata masharti yote yaliwekwa ili kuhakikisha application yako haiwekwi kapuni.
 
si kweli kwamba kuna upendeleo wa nchi fulani.....................tatizo letu Watanznia ni kuwa habari nyingi we DO NOT SHARE.................leo hii ukiwauliza Watanzania wengi wanajua kuwa hii GreenCard Lottery ni mpaka upitie kwa Maagent.................hata ukiangalia magazetini Bongo utakuta baadhi ya watu wanafanya biashara...............simply because they have Internet Access!! thats all.......and they scoop a lot of money out of tanzanians tena wale walio na uwezo tu!!!!

Nafikri wanaoongoza ktk kupata zaidi hii Lottery kwa Afrika ni NIGERIA...........you know why......it is because Nigerians are very aggressive ktk kupata informations kama hizi so as Kenyans......na wenzetu hupeana hizi habari kwa saana tu.

Kwa hiyo ni kweli utaona hivi karibuni idadi ya Watanzania wapatao hii GreenCard imeongezeka simply because mambo ya mtandao nayo yameongezeka na watu wameanza kuchacharika..............though nina imani wanafanya hivyo through agents.

Cha MSINGI FUATA MASHARTI (especialy ktk picha) kama yalivyoainishwa............na usichoke ukijaribu mwaka huu ukashindwa jaribu hata mara sita hata kumi utakuja pata tu...............my experience kuna watu wamejaribu mpaka mara ya tatu au nne ndio wanapata, na kuna wengine wakijaribu once wanapata..............i.e. its really a lottery!!

Zoezi zima ni bure...no need ya kutumia Agent.....soma kwenye hiyo link nilizoweka utakutana na hiyo statement...............na mtandao nilioutoa ni wa Serikali ya US sio wa kitapeli........so just try your LUCK! you never know

Nawaomba sana Watanzania wenzangu tubadilike na tupeane informations na pia tuwe AGGRESSIVE kuzitumia i.e. KU-APPLY.............informations kama za SCHOLARSHIPS kama alivyotoa ndg yangu Steve D na Mwl Prof Kichuguu.................nafasi za kazi kama anavyozitoa mzee mzima Mac De Melo....kwa kweli hawa nawapongeza sana.

Pia kuna Professional Immigration Schemes ktk nchi ya Canada na Uingereza unapewa permanent residence with a right to work...................hii ni kwa fani mbali mbali, kama system yetu ya nyumbani haiwezi kutu-absorb wote basi lets try sehemu zingine....na tukapate experience huko kwani professionals wanahitajika saana tu.

Kwa mfano Juzi juzi hapa Uingereza walitangaza wazi katika HOme Office yao kuwa wana Uhaba wa Quantity Surveyors and other professions......kw ahiyo jamani tuchangamkie hizi nafasi

Kwa walio Interested na Profession Immigration to Canada link ni hapa chini
http://www.cic.gc.ca/english/information/applications/skilled-simple.asp
na fomu zao ni hizi hapa
http://www.cic.gc.ca/english/pdf/kits/forms/imm0008e_SW.pdf

Kwa walio na Interest na Profession Immigration to UK link ni hii hapa
http://www.workingintheuk.gov.uk/working_in_the_uk/EN/homepage/schemes_and_programmes/hsmp.html
Click hiyo sehemu iliyoandikwa Highly Skilled Migrant Program

Jamani tuzitafute huku kwa watu halafu turudi Nyumbani tuwekeze

Kila la kheri Bandugu
 
Nadhani kuna upendeleo fulani wa baadhi ya nchi, Kenya ikiwa mojawapo.

Ni vizuri tukijua kuwa upendeleo huwa unatokana na nini. Na kwanini watanzania kwa siku za karibuni wakemuwa wakiongezeka, au wamarekani wamekuwa wakihitaji watanzania wengi zaidi? Au watanzania wamekuwa na mwimko wa kuapply.
 
Ogah! shukurani sana mkuu information is power unajua kweli watanzana wengi huwa hawana information ya nafasi kama hizi. Nakumbuka kwenye thread ya moja huko nyuma nilipendekeza iwepo thread maalumu ya scholarship ambayo itawasaidia sana vijana wetu wanaotafuta scholarship. Na hii pia ina faida kwa JF maana vijana wengi wakishajua kama kuna taarifa kama hizo hakika watakuwa wanasoma JF na watakuja kuwa wanachama wazuri wa maendeleo Tanzania. Wengi wanahamu ya kupata elimu, kazi na exposure nje ya nchi lakini hawajui pakuanzia ila kama kweli watu tukiwatunatoa taarifa za ajira, scholarship etc i think is good idea
 
Ogah ahsante kwa hizo links.

Na pia natoa shukran kwa wachangiaji wengine wa mada hii.

Nafikiri ni ile point kwamba sisi watanzania hatupeani taarifa na kusaidiana na matokeo yake tunabaki nyuma kwa kila sekta.

Lakini pia tusisahau kwamba wenzetu wa-Nigeria na wa-Ghana wameanza kusafiri kwa wingi tokea kabla ya Tanzania kupata uhuru na ndio maana wao hata kama wanafanya maombi pia inakuwa rahisi kwa ndugu zao ku-submit hayo maombi kwa uharaka.

Kwa mfano kama sikose maombi yalianza kupokelewa tokea tarehe 3 October kama sikosei na mpaka sasa kama nafikiri hawa wenzetu wamewahi.

Lakini kidogokidogo tutafika mambo sio mabaya.

Angalieni hii orodha niliyooipata kutoka tovuti ya U.S State Department kwa mama "Condi". Haya ni matokeo ya ile iliyochezwa mwaka jana.

AFRICA

ALGERIA
912
ERITREA
582

ANGOLA
13
ETHIOPIA
6,871

BENIN
218
GABON
42

BOTSWANA
1
GAMBIA, THE
50

BURKINA FASO
95
GHANA
3088

BURUNDI
16
GUINEA
146

CAMEROON
1461
GUINEA-BISSAU
5

CAPE VERDE
3
KENYA
2,337

CENTRAL AFRICAN REP.
13
LESOTHO
0

CHAD
28
LIBERIA
734

COMOROS
7
LIBYA
37

CONGO
687
MADAGASCAR
21

CONGO, DEMOCRATIC REPUBLIC OF THE
42
MALAWI
18

COTE D'IVOIRE
308
MALI
76

DJIBOUTI
11
MAURITANIA
17

EGYPT
7,229
MAURITIUS
8

EQUATORIAL GUINEA
1
MOROCCO
4,922

NAMIBIA
8
MOZAMBIQUE
4

NIGER
62
SOUTH AFRICA
287

NIGERIA
9,849
SUDAN
569

RWANDA
41
SWAZILAND
5

SAO TOME AND PRINCIPE
2
TANZANIA
148


SENEGAL
228
TOGO
1,592

SEYCHELLES
4
TUNISIA
124

SIERRA LEONE
540
UGANDA
213

SOMALIA
160
ZAMBIA
92

ZIMBABWE
73


Halafu siku hizi sio kwamba ukishinda unakuwa na "guarantee" ya kuingia states, kuna "process" kubwa sana ya kukuchambua kwa maswali na kutaka kuona kila kitu kuhusu wewe vikiwemo "qualifications" na kama hauna dalili za kuwa gaidi hapo baadae.
 
idadi Ya Watanzania Waliofanikiwa Kupata Dv Visa Kwa Kipindi Cha Miaka 10 Nyuma!!,jaribu Bahati Yako Sasa;

2007 - 148
2006 - 251
2005 - 356
2004 - 329
2003 - 349
2002 - 269
2001 - 231
2000 - 267
1999 - 357
1998 - 268



 
  • Thanks
Reactions: SDG
number inakwenda inashuka sio, lakini I thought inakwenda na Visa quota, kama wamepanga kutoa visa 5,000 kwa mwaka kwa raia wa Tanzania basi itabidi mgawane na kwenye greencard as well(sina uhakika na hili) ila nakumbuka wacuba walikuwa wanalalamika kuhusiana na huo mgawanyo.
 
Jamani kama walivyosema wenzangu hapa...tusijiwekee vikwazo..ohh kuna upendeleo, kuna quota nk..cha muhimu tuma karatasi zako na FUATA MASHARTI. Watanzania wenzangu tusipende mkato, dunia ya leo, you either fight for survival or you perish! Tujitahidi, hata kama ni shule, unaweza kuapply katika vyuo ishirini ukajibiwa kumi, ukapewa financial aid katika vitatu na ukapewa full scholarship katika kimoja. Thats the way it is.

wewe unataka masters ulaya, bado unataka mtu akutafutie scholarship? BE AGGRESSIVE bandugu, there is no success by chance siku hizi.
Harafu bado kuna watu wanawaibia wale wasio jua, kwa mfan mtu akikwambia kwamba umtafutie chuo ulaya au US ni dhahiri kwamba kwa kumsaidia utampa maelezo kwamba kila kitu kipo kwenye net tjifunze kusaidiana, mwenzako akipata haikupunguzii kitu wewe. na mtoa riziki ni MUNGU.
 
Nilishinda DV Lottery miaka kama 10 iliyo pita.
Kabla sijaja majuu nikajitolea kuwaelekeza watu wengi namna ya kucheza, wengi wao walinielewa lakini walikuwa na swali moja kubwa sana.

Ukishinda wanakutumia Tiketi ya ndege?

Nikawauliza anaye taka kwenda America ni wao au ni wewe?

Nikaambiwa Sasa bila Tiketi nitakwendaje na faida yake ni nini? Au unatuficha namna ya kupata tiketi?

Wewe tiketi umepata wapi?
Nikawaeleza namna nilivyo jikusanya na kugharamia safari yangu.

Jibu la mwisho likawa.
Ah! kama ndo hivyo si heri nibaki Bongo tu.

Sasa kama Watanzania walio wengi wana mawazo kama hao nilo kutana nao mimi DV Lottery is not for them.
 
Madela yaani umenifanya nicheke kweli leo.....duuhh

anyway yeyote atakayeamua kufuata masharti na acheze
 
Madilu hata mi nimecheka sana. lakini hiyo ndo familiar approach ya wengi. unasoma ulaya? scholarship ulipata wapi? Aise tuna safari ndefu bado!
 
Hili la ticket kusema kweli mie mwenyewe nilishalisikia, ila kuna certain websites wanasema wanaprovide air tickets kama ukiregister kupitia kwao(wanachaji hela) guess its another scam
 
Mimi nakumbuka miaka ile ya 90 mwanzoni niliamua kuliondolea uvivu suala la DV lottery basi nikaenda pale ubalozi wa Marekani enzi hizo pale Laibon road, hapakuwa na ulinzi mkali kama ilivyo leo, nikaingia mle nikaulizia hiyo DV lottery pale mlangoni basi nikaitiwa mtu wao mle akanisomesha mchezo wenyewe, akanijibu maswali yangu vizuri, halafu akanipa na handout yenye taratibu zote za mwaka ule.

Hakuna cha upendeleo wala nini, hivi vitu vinawezekana kabisa na tena huna haja ya kupoteza pesa kwa hao wanaojiita ma-agent.
 
Madilu zaidi ya kucheka sana lakini umetoa changamoto kwa wasiotaka na kukata tamaa za kujaribu lottery hiyo.
Ki ukweli kwa miaka hii masharti yamepungua sharti kubwa ni kuhusu picha tu!
Na kama ukifata masharti yake basi bahati inaweza kuwa yako
 
Jamani kama walivyosema wenzangu hapa...tusijiwekee vikwazo..ohh kuna upendeleo, kuna quota nk..cha muhimu tuma karatasi zako na FUATA MASHARTI. Watanzania wenzangu tusipende mkato, dunia ya leo, you either fight for survival or you perish! Tujitahidi, hata kama ni shule, unaweza kuapply katika vyuo ishirini ukajibiwa kumi, ukapewa financial aid katika vitatu na ukapewa full scholarship katika kimoja. Thats the way it is.

wewe unataka masters ulaya, bado unataka mtu akutafutie scholarship? BE AGGRESSIVE bandugu, there is no success by chance siku hizi.
Harafu bado kuna watu wanawaibia wale wasio jua, kwa mfan mtu akikwambia kwamba umtafutie chuo ulaya au US ni dhahiri kwamba kwa kumsaidia utampa maelezo kwamba kila kitu kipo kwenye net tjifunze kusaidiana, mwenzako akipata haikupunguzii kitu wewe. na mtoa riziki ni MUNGU.

Mkuu kwenye masuala ya Scolarships wengi wanaona kama ni miujiza kupata,hawajaribu na hata wakiona wenzao wanapata bado wanajua wametumia njia za "panya"
 
Kuukata kuna Gharama yake.
Maendeleo ni kwa wale wayatafutayo.


Hakuna upendeleo katika DV Lottery.

Ukija hapa America kuna opportunity nyingi sana lakini ni vema ujijue na kujidefine mwenyewe sivyo utaishia kwenye Section 8 na Food Stamp na kuishi kwa ghrama za walipa kodi wa America.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Oga, madilu nakubaliana nanyi kwa asilimia zote. Mimi nacheza, with hope kuwa next year nitawajulisha kuwa nimepata!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom