Urusi na China ni hatari kwa usalama wa Dunia

We utakuwa. mwarabu koko sio bure!

Libya waliomuua Gadaffi ni walibia wenyewe kwa upumbavu wao.
Sijaona missile za US zikibomoa magorofa ya Libya kama nionavyo Ukraine.

Zaidi ya 70% ya migogoro ya kivita Duniani imesababishwa na U.S.A pekee...

Halafu mbona watu mnakuwa wanafiki hivi..?? Hamuoni maovu yanayofanywa na U.S.A pamoja na washirika wake..??

01. U.S.A & NATO waliivamia Libya na kumuua Ghadaffi, watu mkapiga kimya. Leo hii Libya amani hakuna., mshawahi jiuliza ile shehena ya Dhahabu na Silver kule Libya imeenda wapi..?? Jee! Baada ya Vita Libya kuna amani..??

02. U.S.A kavamia Iraq kwa kigezo cha kuwa kuna siraha za maangamizi, ffs.. hizo siraha mliziona..?? Afghanistan jee..?, kavuruga amani kule then kasepa mbona hamkulaani hilo..??

03. Israel anaendelea kuitesa Palestina, mpo kimya.. hakuna kuwekewa vikwazo wala nini..

PS: Sio kama nakubaliana na uamuzi wa Russia kuvamia Ukraine, nah! Ninachosema ni kuwa thread yako haina mantiki kwa sababu uliowatuhumu sio wenyewe... anza na U.S.A, NATO & Israel kwanza ndo uje kwa Russia na China.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muwe mnatumia akili zenu vizuri.
Rais wa Ukraine aliomba po kwa Putin,lakini Putin alikataa.Russia wanaua wananchi wa Ukraine kikatili sana.
Sijawahi kuona US anavamia nchi na kuua raia kikatili.Wao hulenga wanajeshi.
Sijawahi kuona mtu ame surrender kwa US na US wakakataa ili mradi waue na kuendeleza ukatili.

Kinachofanywa Ukraine na Russia ni zaidi ya ushetani.Tafuteni picha za madhila ya Ukraine mtaelewa ukatili wa Putin
Aise nimekosa maneno ya kusema! Kama Marekani ilivyoyafanyia mataifa mengine harafu inaonekana ni nchi nzuri kuliko Russia na China basi sina cha kucomment hapa!
 
“Sijawahi kuona US anavamia nchi na kuua raia kikatili.Wao hulenga wanajeshi.” Yan mtu anashupaza shingo kabisa kusema hivi kuna watu ninawasiwasi hatupo nao dunia Hii labda wanaishi space huko we ongelea nchi nyingine ila sio US
 
We utakuwa. mwarabu koko sio bure!

Libya waliomuua Gadaffi ni walibia wenyewe kwa upumbavu wao.
Sijaona missile za US zikibomoa magorofa ya Libya kama nionavyo Ukraine.
Endelea kuongea kwa mihemko.... vita yenyewe ya Libya inaonekana hukuifuatilia kabisa... hujui hata aliyeshambulia msafara wa Ghaddafi mara ya mwisho kabisa hadi akauwawa ni nani.

Halafu kwa akili yako mbovu usipojua adui anabomoa vipi lazima uwe muhanga tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana Rais wa Marekani Joe Biden kampigia simu Rais wa Ukraine na kumweleza kuwa awe na amani na asihofu vitisho vya Urusi baada ya Urusi kuweka vikosi vya kijeshi kwenye mpaka wa Ukraine, Rais Joe Biden aliahidi kuilinda Ukraine endapo Urusi itaivamia.
Masaa machache baadaye,NATO pia iliionya Urusi isijaribu kufanya uvamizi wowote kwa Ukraine,kwani itaingilia Kati kijeshi.
Urusi ilijibu kwa kiburi sana kuwa itaivamia Ukraine endapo itaona inafaa kufanya hivyo.
Hayo yametokea wakati Dunia ikiwa kimya mauaji ya kishenzi na kikatili yakiendelea Myanmar baada ya Serikali halali iliyochaguliwa Kidemokrasia kupinduliwa, wananchi wa Myanmar wanaandamana Taifa zima kudai Rais wao mwanamama Aung Su Kyi anayeshikiliwa na jeshi aachiwe huru,mamia ya watu wameuawa Myanmar.
Msako wa nyumba hadi nyumba unafanyika ktk Taifa hilo ili kuwaua na kuwafunga watu wote wanaopinga mapinduzi hayo.
Duru za kijasusi zinadai kuwa China ndo inafadhili Serikali haramu iliyofanya mapinduzi.
Wakati huo huo, Urusi nayo inadaiwa kufadhili vikundi vya waasi Central Africa .
Urusi na China ni mataifa makubwa yasiyokuwa na msaada wowote,ni mataifa adui wa Demokrasia na haki za Binadamu.
Pamoja na kuwa Marekani ina mapungufu yake,lakini ni Taifa lenye utu na huruma Tofauti kabisa na Urusi na China.
Urusi iliivamia Cremea na kuichukua kwa nguvu kutoka Ukraine, sasa hivi tena inajiandaa kuivamia Ukraine.
Urusi na China ndo mataifa yanayopendwa na Serikali za kidikteta Duniani kwa sababu huzilinda Serikali hizo kwa manufaa yao hata kama zinaua watu wake wote.
Hayati Saddam Hussein, alikuwa kipenzi cha Marekani pamoja na Udikteta wake,lakini alipoua Wakurd 5,000 kwa sumu na kuivamia Kuwait,wakamgeuka na kumtoa kwa nguvu.
Ni wapi mliona Urusi au China zikipeleka majeshi au misaada kwa nchi zenye shida Duniani?
Yaani hayo ni mataifa selfish na katili hasa,hayana ubinadamu hata kidogo.
Endapo Urusi itaivamia Ukraine,safari hii Marekani haitavumilia Kama ilivyovumilia wakati Urusi ilipoivamia Georgia.
Hii itaweza ku spark vita ya Tatu ya Dunia.
Myanmar ni Taifa la watu wenye nasaba na China,huko wameuawa hadi watoto wadogo kwa risasi, China inao uwezo wa kuzuia mauaji Myanmar lakini haifanyi hivyo kwa sababu ni Taifa katili lisilo na utu.
Urusi na China ni mataifa hatari kwa usalama wa Dunia.
Siku hizi hakuna taarifa za habari zisizo na pande mbili kama sarafu. Ukitaka siku hizi kupata habari kamili inabidi usikilize taarifa mbali mbali kuhusu hilo tukio - ndipo unajua ukweli zaidi. Usiingie kwenye mtego wa kumuamini anaepiga kelele zaidi ama alie na sura nzuri na suti nzuri - huo ni ushabiki sio uchambuzi. Dunia ya leo inachochea mgawanyo na ubaguzi - ni kazi yako wewe unaposikia taarifa za habari kutofuata mkumbo ila kuchanganua pande ingine husika.

Mimi niko upande wa uhalisia na ukweli. Zipo sababu nzuri za kumsikiliza mrusi...
  1. Kuna miji miwili mpakani mwa Ukraine na Urusi iliojitenga na Ukraine miaka nane na zaidi imepita lakini . Tuchukue mfano wa Sudani kusini ilivojitenga. Hii miji ina wakazi wa asili ya warusi. Tusisahau zamani Ukraine ilikuwa sehemu ya Urusi. Wakazi wa miji hii wamekuwa wanaonewa sana na Ukraine zaidi ya miaka nane, na wakina marekani na wenzao wa magharibi walijibakia kimya kama wanavojibakia kimya kuhusu mateso na ubaguzi wa waPalestina miaka nenda miaka rudi. Warusi wamelalama kwa miaka zaidi ya nane - hili suala sio la juzi kama wanatuambia wa magharibi. Hata majuzi hawa wakazi ndio wametupiwa makombora kwanza. JWTZ tulisaidia ndugu zetu wamakonde upande wa msumbiji majuzi tu walipokuwa wanaonewa na waasi.
  2. Wa magharibi waliahidi Urusi kwamba hawatatanua jeshi lao la NATO ili lisifike mipakani mwa Urusi na kuzua kasheshe. Ilikuwa uongo ama wamemdharau mrusi wakatanua hadi sasa wanataka kuingia Ukraine rasmi. Nasema rasmi kwa sababu tayari wanatuma silaha na wanajeshi Ukraine. Mrusi amekasirikia uongo huo na majuzi kabla ya haya yote kuanza waliomba maongezi ya msingi kutatua swala hii wakabezwa. Mrusi zamani alipotishia kuweka makombora Cuba karibu na marekani walifura kinoma... nini tofauti sasa ya mrusi kutotaka hilo hilo. Ni unafiki. Leo hii tukiona rwanda anaweka makombora yake mpakani mwetu akilengesha kwetu sidhani tutabaki kimya.
  3. JWTZ wakiamua kufanya mazoezi ya kivita Namanga - Kenya ana haki ya kulalama?
  4. wamagharibi wana madhambi mengi sana ya uvamizi wa kijeshi wenye misingi ya kibepari na sio kiutu... mbona haulalami? Na wao wana haki gani ya kumlalamikia mrusi wakati wao wenyewe ni mabingwa wa vitendo hivo?
  5. Mobutu alipomuua Lumumba alichochewa na wamagharibi kwa nia ya kuondoa kipingamizi cha kunyonya wananchi. Mobutu alikuwa kibaraka, mlafi na wamagharibi wakamchota. Ukraine na warusi ni kama ndugu - sidhani raisi wa Ukraine ambae sio kibaraka wa magharibi angetaka vita na ndugu zake.
 
Jana Rais wa Marekani Joe Biden kampigia simu Rais wa Ukraine na kumweleza kuwa awe na amani na asihofu vitisho vya Urusi baada ya Urusi kuweka vikosi vya kijeshi kwenye mpaka wa Ukraine, Rais Joe Biden aliahidi kuilinda Ukraine endapo Urusi itaivamia.
Masaa machache baadaye,NATO pia iliionya Urusi isijaribu kufanya uvamizi wowote kwa Ukraine,kwani itaingilia Kati kijeshi.
Urusi ilijibu kwa kiburi sana kuwa itaivamia Ukraine endapo itaona inafaa kufanya hivyo.
Hayo yametokea wakati Dunia ikiwa kimya mauaji ya kishenzi na kikatili yakiendelea Myanmar baada ya Serikali halali iliyochaguliwa Kidemokrasia kupinduliwa, wananchi wa Myanmar wanaandamana Taifa zima kudai Rais wao mwanamama Aung Su Kyi anayeshikiliwa na jeshi aachiwe huru,mamia ya watu wameuawa Myanmar.
Msako wa nyumba hadi nyumba unafanyika ktk Taifa hilo ili kuwaua na kuwafunga watu wote wanaopinga mapinduzi hayo.
Duru za kijasusi zinadai kuwa China ndo inafadhili Serikali haramu iliyofanya mapinduzi.
Wakati huo huo, Urusi nayo inadaiwa kufadhili vikundi vya waasi Central Africa .
Urusi na China ni mataifa makubwa yasiyokuwa na msaada wowote,ni mataifa adui wa Demokrasia na haki za Binadamu.
Pamoja na kuwa Marekani ina mapungufu yake,lakini ni Taifa lenye utu na huruma Tofauti kabisa na Urusi na China.
Urusi iliivamia Cremea na kuichukua kwa nguvu kutoka Ukraine, sasa hivi tena inajiandaa kuivamia Ukraine.
Urusi na China ndo mataifa yanayopendwa na Serikali za kidikteta Duniani kwa sababu huzilinda Serikali hizo kwa manufaa yao hata kama zinaua watu wake wote.
Hayati Saddam Hussein, alikuwa kipenzi cha Marekani pamoja na Udikteta wake,lakini alipoua Wakurd 5,000 kwa sumu na kuivamia Kuwait,wakamgeuka na kumtoa kwa nguvu.
Ni wapi mliona Urusi au China zikipeleka majeshi au misaada kwa nchi zenye shida Duniani?
Yaani hayo ni mataifa selfish na katili hasa,hayana ubinadamu hata kidogo.
Endapo Urusi itaivamia Ukraine,safari hii Marekani haitavumilia Kama ilivyovumilia wakati Urusi ilipoivamia Georgia.
Hii itaweza ku spark vita ya Tatu ya Dunia.
Myanmar ni Taifa la watu wenye nasaba na China,huko wameuawa hadi watoto wadogo kwa risasi, China inao uwezo wa kuzuia mauaji Myanmar lakini haifanyi hivyo kwa sababu ni Taifa katili lisilo na utu.
Urusi na China ni mataifa hatari kwa usalama wa Dunia.
Vipi mauaji yanayoendelea syria, Libya, na yaliyofanyika Afghanistan, Iraq, china urusi wamehusika vipi?

Ninyi hamna uwezo wa kufikiri kunyume na brainwashing za BBC na DW?

Redio uchwara za mabeberu
 
Muwe mnatumia akili zenu vizuri.
Rais wa Ukraine aliomba po kwa Putin,lakini Putin alikataa.Russia wanaua wananchi wa Ukraine kikatili sana.
Sijawahi kuona US anavamia nchi na kuua raia kikatili.Wao hulenga wanajeshi.
Sijawahi kuona mtu ame surrender kwa US na US wakakataa ili mradi waue na kuendeleza ukatili.

Kinachofanywa Ukraine na Russia ni zaidi ya ushetani.Tafuteni picha za madhila ya Ukraine mtaelewa ukatili wa Putin
Unafahamu kwanini mwedesha mastaka wa ICC alizuiwa asiingie USA?

Kule Ukraine tumeona mtu akipiga magoti mbele kifaru cha Russia na kifaru kinasimams
 
“Sijawahi kuona US anavamia nchi na kuua raia kikatili.Wao hulenga wanajeshi.” Yan mtu anashupaza shingo kabisa kusema hivi kuna watu ninawasiwasi hatupo nao dunia Hii labda wanaishi space huko we ongelea nchi nyingine ila sio US
 
Hata SYRIA ma mercenaries wa Urusi wanaopata usaidizi from their country wanawaua raia wa kawaida kila kukicha, wanamsaidia Assad kuua raia wake. Hii ata haipingiki sababu dunia nzima yajua utopolo wa Urusi ndani ya Syria
Umeshawahi jiuliza nani anasaidia upande mwingine? Umeshawahi jiuliza mbona ISIL ni kikundi tofauti ni kina alkaida kiujumla?
 
Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa mrengo wa Urusi na China. Katika kipindi cha uongozi wake nchi yetu ilipiga hatua kubwa sana, elimu ilikua bora sana,viwanda vingi sana,tulikuwa na Tiss bora sana, jeshi bora ,thamani ya pesa yetu ilikuwa juu sana na mengine mazuri mengi sana ukiacha demokrasia ambayo tulikuwa nyuma.kwangu mimi naona huu mrengo wa urusi na china una mazuri mengi sana ukilinganisha na huu wa kugawa ARV na vyandarua huku tukikatazwa kujenga Hata Bwawa la kuzalisha umeme wetu
 
Uko Sahihi
China na Urusi wale wanapenda sana kutetea madikteta sababu wana faidi kitu/vitu flani katika nchi hizo.
Angalia 'Belarus', 'Myanmar', 'Azerbaijan', 'Syria', 'Georgia', huko China kwenyewe, ndio utajua hawa jamaa hawajui haki wala utu. They do what they want!
Na sio rahisi usikie wametoa msaada wa kiuchumi, kiusalama nk pahali popote. Wao ni biashara kila kitu!
 
Unaonekana wewe hujui hata historia ya dunia kuhusu nani ni muovu. America ndo mapepo wa dunia hii...

Screenshot_20220305-182945_1.jpg
 
Rais Joe Biden aliahidi kuilinda Ukraine endapo Urusi itaivamia.
Masaa machache baadaye,NATO pia iliionya Urusi isijaribu kufanya uvamizi wowote kwa Ukraine,kwani itaingilia Kati kijeshi.
....Biden alimuingiza chaka huyu 'comedian'.... huku akifahamu fika

(1) Nchi yake katu haiko tayari kuingia vitani kuilinda nchi isiyo mwanachama wa NATO.

(2) Raia wa Marekani na hata wabunge wao hawapo tayari kuona taifa lao likiingia vitani na Urusi inayomiliki silaha za nuklia kama wao.

(3) Ukraine haina faida/maslahi yoyote kwa Marekani zaidi ya kutumika kama uwanja wa kuchuana na Urusi.

Comedian na yeye aliingia mzima mzima kwa hadaa za babu Biden hatimaye leo ameiletea nchi yake balaa.
 
Sijawahi kuona US anavamia nchi na kuua raia kikatili.Wao hulenga wanajeshi.
Kasome habari kuhusu ukatili uliotendeka huko Vietnam 'mai lai massacre'

Pitia kuhusu madhila yaliyosababishwa na ndege zisizotumia rubani za Marekani huko Pakistani,Yemen,Syria na Afghanistan.

Angalia idadi ya raia waliokufa kutokana na uvamizi wa Marekani huko Iraq.
 
Jana Rais wa Marekani Joe Biden kampigia simu Rais wa Ukraine na kumweleza kuwa awe na amani na asihofu vitisho vya Urusi baada ya Urusi kuweka vikosi vya kijeshi kwenye mpaka wa Ukraine, Rais Joe Biden aliahidi kuilinda Ukraine endapo Urusi itaivamia.
Masaa machache baadaye,NATO pia iliionya Urusi isijaribu kufanya uvamizi wowote kwa Ukraine,kwani itaingilia Kati kijeshi.
Urusi ilijibu kwa kiburi sana kuwa itaivamia Ukraine endapo itaona inafaa kufanya hivyo.
Hayo yametokea wakati Dunia ikiwa kimya mauaji ya kishenzi na kikatili yakiendelea Myanmar baada ya Serikali halali iliyochaguliwa Kidemokrasia kupinduliwa, wananchi wa Myanmar wanaandamana Taifa zima kudai Rais wao mwanamama Aung Su Kyi anayeshikiliwa na jeshi aachiwe huru,mamia ya watu wameuawa Myanmar.
Msako wa nyumba hadi nyumba unafanyika ktk Taifa hilo ili kuwaua na kuwafunga watu wote wanaopinga mapinduzi hayo.
Duru za kijasusi zinadai kuwa China ndo inafadhili Serikali haramu iliyofanya mapinduzi.
Wakati huo huo, Urusi nayo inadaiwa kufadhili vikundi vya waasi Central Africa .
Urusi na China ni mataifa makubwa yasiyokuwa na msaada wowote,ni mataifa adui wa Demokrasia na haki za Binadamu.
Pamoja na kuwa Marekani ina mapungufu yake,lakini ni Taifa lenye utu na huruma Tofauti kabisa na Urusi na China.
Urusi iliivamia Cremea na kuichukua kwa nguvu kutoka Ukraine, sasa hivi tena inajiandaa kuivamia Ukraine.
Urusi na China ndo mataifa yanayopendwa na Serikali za kidikteta Duniani kwa sababu huzilinda Serikali hizo kwa manufaa yao hata kama zinaua watu wake wote.
Hayati Saddam Hussein, alikuwa kipenzi cha Marekani pamoja na Udikteta wake,lakini alipoua Wakurd 5,000 kwa sumu na kuivamia Kuwait,wakamgeuka na kumtoa kwa nguvu.
Ni wapi mliona Urusi au China zikipeleka majeshi au misaada kwa nchi zenye shida Duniani?
Yaani hayo ni mataifa selfish na katili hasa,hayana ubinadamu hata kidogo.
Endapo Urusi itaivamia Ukraine,safari hii Marekani haitavumilia Kama ilivyovumilia wakati Urusi ilipoivamia Georgia.
Hii itaweza ku spark vita ya Tatu ya Dunia.
Myanmar ni Taifa la watu wenye nasaba na China,huko wameuawa hadi watoto wadogo kwa risasi, China inao uwezo wa kuzuia mauaji Myanmar lakini haifanyi hivyo kwa sababu ni Taifa katili lisilo na utu.
Urusi na China ni mataifa hatari kwa usalama wa Dunia.
Yametimia mkuu
 
“Sijawahi kuona US anavamia nchi na kuua raia kikatili.Wao hulenga wanajeshi.” Yan mtu anashupaza shingo kabisa kusema hivi kuna watu ninawasiwasi hatupo nao dunia Hii labda wanaishi space huko we ongelea nchi nyingine ila sio US
du historia inavofichwa ... mmarekani na wenzake ndo walivunja East African Community ya kwanza, ilishindana nao kiuchumi. CIA ni chombo cha mmarekani kinachohusika na mauaji ya viongozi na wapigania uhuru wengi - Nkrumah, Lumumba nikitaja wachache.
Usipojua historia yako ni rahisi kurudia makosa yako
 
Hatua gani kubwa tulipiga?
Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa mrengo wa Urusi na China. Katika kipindi cha uongozi wake nchi yetu ilipiga hatua kubwa sana, elimu ilikua bora sana,viwanda vingi sana,tulikuwa na Tiss bora sana, jeshi bora ,thamani ya pesa yetu ilikuwa juu sana na mengine mazuri mengi sana ukiacha demokrasia ambayo tulikuwa nyuma.kwangu mimi naona huu mrengo wa urusi na china una mazuri mengi sana ukilinganisha na huu wa kugawa ARV na vyandarua huku tukikatazwa kujenga Hata Bwawa la kuzalisha umeme wetu
 
Marekani ameshajipigia propaganda kuwa yeye ni msafi
 
Back
Top Bottom