My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,335
Jana Rais wa Marekani Joe Biden kampigia simu Rais wa Ukraine na kumweleza kuwa awe na amani na asihofu vitisho vya Urusi baada ya Urusi kuweka vikosi vya kijeshi kwenye mpaka wa Ukraine, Rais Joe Biden aliahidi kuilinda Ukraine endapo Urusi itaivamia.
Masaa machache baadaye,NATO pia iliionya Urusi isijaribu kufanya uvamizi wowote kwa Ukraine,kwani itaingilia Kati kijeshi.
Urusi ilijibu kwa kiburi sana kuwa itaivamia Ukraine endapo itaona inafaa kufanya hivyo.
Hayo yametokea wakati Dunia ikiwa kimya mauaji ya kishenzi na kikatili yakiendelea Myanmar baada ya Serikali halali iliyochaguliwa Kidemokrasia kupinduliwa, wananchi wa Myanmar wanaandamana Taifa zima kudai Rais wao mwanamama Aung Su Kyi anayeshikiliwa na jeshi aachiwe huru,mamia ya watu wameuawa Myanmar.
Msako wa nyumba hadi nyumba unafanyika ktk Taifa hilo ili kuwaua na kuwafunga watu wote wanaopinga mapinduzi hayo.
Duru za kijasusi zinadai kuwa China ndo inafadhili Serikali haramu iliyofanya mapinduzi.
Wakati huo huo, Urusi nayo inadaiwa kufadhili vikundi vya waasi Central Africa .
Urusi na China ni mataifa makubwa yasiyokuwa na msaada wowote,ni mataifa adui wa Demokrasia na haki za Binadamu.
Pamoja na kuwa Marekani ina mapungufu yake,lakini ni Taifa lenye utu na huruma Tofauti kabisa na Urusi na China.
Urusi iliivamia Cremea na kuichukua kwa nguvu kutoka Ukraine, sasa hivi tena inajiandaa kuivamia Ukraine.
Urusi na China ndo mataifa yanayopendwa na Serikali za kidikteta Duniani kwa sababu huzilinda Serikali hizo kwa manufaa yao hata kama zinaua watu wake wote.
Hayati Saddam Hussein, alikuwa kipenzi cha Marekani pamoja na Udikteta wake,lakini alipoua Wakurd 5,000 kwa sumu na kuivamia Kuwait,wakamgeuka na kumtoa kwa nguvu.
Ni wapi mliona Urusi au China zikipeleka majeshi au misaada kwa nchi zenye shida Duniani?
Yaani hayo ni mataifa selfish na katili hasa,hayana ubinadamu hata kidogo.
Endapo Urusi itaivamia Ukraine,safari hii Marekani haitavumilia Kama ilivyovumilia wakati Urusi ilipoivamia Georgia.
Hii itaweza ku spark vita ya Tatu ya Dunia.
Myanmar ni Taifa la watu wenye nasaba na China,huko wameuawa hadi watoto wadogo kwa risasi, China inao uwezo wa kuzuia mauaji Myanmar lakini haifanyi hivyo kwa sababu ni Taifa katili lisilo na utu.
Urusi na China ni mataifa hatari kwa usalama wa Dunia.