Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,169
- 10,899
Sergeant William Jerome Rivers, 46, Specialist Kennedy Ladon Sanders, 24 and Specialist Breonna Alexsondria Moffett, 23
Hao hapo juu ndio askari watatu wa Marekani waliokufa kwenye shambulio la Droni huko Jordan na ambao Pentagon imeazimia kulipiza kisasi kikubwa kutokana na vifo vyao.
Makundi kadhaa ya kihafidhina yamekuwa yakimshinikiza raisi Biden achukue hatua kali kulipiza kisasi ili tukio kama hilo lisijirudiea tena.
Nchi inayotajwa kuwa lengo la ulipizwaji kisasi hicho ni Iran na Lebanon waliko Hizbullah na sababu ni kuwa droni iliyotumika ni ile aina ya shahed inayotengenezwa Iran kama inazotumia Urusi katika vita na Ukraine ambazo huwa wanazinunua kutoka Iran.
Hapo inaonekana Marekani inatafuta sababu kuanzisha vita vingine vibaya mashariki ya kati huku vita vya Gaza hata havijamalizika.
Kuonekana kwa droni zilizotengenezwa Iran kutumika katika shambulio hilo ni kisingizio cha ovyo cha kuanzishia vita.Silaha za Marekani zimekuwa zikitumika dunia nzima kuua watu kwa maelfu.Jee wote hao ni halali kupelelka mashambulizi yao Marekani kwa sababu hiyo.
Huko Urusi,sasa wanapata hasara kubwa na kutokea kwa vifo kutokana na silaha kali zaidi ya droni zinazopelekewa Ukraine kutoka Marekani.Kwanini Urusi haijaingia vitani moja kwa moja kwa kujua silaha hizo zinatokea Marekani.
Mpiganaji mzuri ni yule anayepigana kutetea haki yake na baada ya kuwa na uhakika na anayemchokoza
Ukishindwa kujua kwa uhakika anayekuchokoza basi ukiingia vitani huwa unaelekea kufedheheka