Urusi haina habari ya ISIS, yaipiga Ukraine kwa nguvu kulipiza kisasi

Kufuatia shambulia kubwa kwenye ukumbi wa starehe jijini Moscow ambapo kundi la ISIS lilijitaja kupitia vyombo vya magharibi kuwa ndilo lililohusika.Urusi imeonekana kutoshawishika na uozo wa taarifa hizo.

Watu kadhaa walikamatwa mara tu baada ya shambulio hilo kutokea ambapo watu zaidi ya 130 wamefariki dunia.

Tangu taarifa hizo za tukio na tuhuma za washukiwa kutoka nchi marafiki wa Ukraine kwa upande wake Urusi haijaonekana kutaja chochote kuhusu kikundi chochote cha kiislamu. Badala yake jeshi la Urusi limeshambulia kwa nguvu kubwa maeneo mbali mbali ya Ukraine yote. Shambulio ambalo ni kubwa kufanyika kwa siku za karibuni.

Kwa upande mwengine Urusi imeitaka Marekani isaidie kupatikana kwa wahusika kufuatia kauli yake kwamba Ukraine sio waliotekeleza shambulia hilo.
Sawa.
 
Ukitumia ubongo wako vizuri utagundua kwamba mrusi sio kwamba anaomba msaada. Anawaambia wanao ona kupondwa kwa mukraine kufuatia shumbulio la kigaidi ni uonevu. Kama wanaona ukraine hahusiki basi wawakamate watu wengine wanao ona wanahusika. Inahitaji akili iliyopevuka kuelewa hilo
OK; Kitendo hiko lakini kitawapa walio upande wa Ukraine sababu ya kutoa misaada zaidi na pia kwa maadui walio ndani ya Urusi kuongeza mashambulizi zaidi kwani wamejua huyu jamaa akipigwa huku yeye huenda kushambulia kule wrong/false target. Hii ni kutokana na walioshikwa kuitaja Uturuki, na ISIS wamekiri kujinasibisha na shambulio hilo lakini Mrusi bado anaing'ang'ania Ukraine.
 
Mrusi anajua anachofanya,,,,,,Hasira zinaishia Ukraine,,, wawapange wengine tena wakapige Moscow
Dah! Mrusi! Ngoja watatoa kipigo kingine tena ndipo akili itamkaa sawa - yeye aendelee tuu na hasira zake kwa Ukraine ili roho yake ifarijike.
 
Dah! Mrusi! Ngoja watatoa kipigo kingine tena ndipo akili itamkaa sawa - yeye aendelee tuu na hasira zake kwa Ukraine ili roho yake ifarijike.
Hakuna magaidi waliomsumbua mrusi zaidi ya wa Chechen na aliwatuliza,,,,hio nchi sio waoga wa kifo utapiga ila watahakikisha na wewe utapata zaidi ya ulichotuma kwao,,,nchi za ulaya wanawajua, mrusi ana historia kubwa sana ya vita tokea zamani sio ma LGBT hao
 
Maneno ya Marekani kuwa ukraine hausiki
Inatafsirika kwamba anayehusika wanamjua
Ndiyo maana ya kusema wasaidie kumtafuta muhusika

Kwani Russia wanashindwa nini kujua wahusika halisi ni nina nani?

Si walionywa lakini kwamba kuna hatari ya ugaidi nchini kwao?
 
Hakuna magaidi waliomsumbua mrusi zaidi ya wa Chechen na aliwatuliza,,,,hio nchi sio waoga wa kifo utapiga ila watahakikisha na wewe utapata zaidi ya ulichotuma kwao,,,nchi za ulaya wanawajua, mrusi ana historia kubwa sana ya vita tokea zamani sio ma LGBT hao
"Hakuna marefu yasiyo na ncha". Mjerumani alikuwa na jeuri sana enzi zake, Warumi zamani ndo waliitawala dunia ya wakati huo lakini wote wameufikia mwisho wao. Huyu Mrusi naye, kama waliomtangulia, ataufikia mwisho wake. Ni suala la muda tuu.
 
Ukiwa hapo yombo unaamini kabisa mrusi hakuzifanyia kazi? Unaamini mrusi hakuwa na taarifa zake binafsi? Taarifa za shambulio hata ukiwa nazo wewe na ndie raisi wa nchi ila taarifa hizo hazijataja eneo husika hata uwe na shirika la usalama wa taifa imara kiasi gani utashambuliwa tu. As long as taarifa ulizo nazo hazitaji eneo husiika. Tuneona imetoka israel na sasa urusi na marekani pia ilitokea na hata hapo Dar ilitokea.
NB: KUNYAMAZA SIWEZI!!
So what is ur point. Taarifa anazo akapewa nyingine then kapigwa halafu tena anaomba marekan isaidie kuwapata wapangaji wa tukio. Huo mlolongo umeusoma unaelewa unachoandika kweli. Au unafikiri mi ni pro America chief.
 
"Hakuna marefu yasiyo na ncha". Mjerumani alikuwa na jeuri sana enzi zake, Warumi zamani ndo waliitawala dunia ya wakati huo lakini wote wameufikia mwisho wao. Huyu Mrusi naye, kama waliomtangulia, ataufikia mwisho wake. Ni suala la muda tuu.
Mrusi hana historia kama za hao jamaa , hadi akupige ni kwamba umemuingilia kwenye mambo yake, ila ukiwa na 50 zako na yeye anabaki na 50 zake,,wakina Napoleon na ubabe wao wote walipoenda urusi wakatulizwa, huyo mjerumani nae pia hivyo hivyo, hata hujiulizi kwa nini warumi walitawala hadi waarabu ila hawakwenda kuwatawala warusi
 
Dude la kutisha wamepigwa mchana kweupe tena pale pale town. Acheni kuwa overrate hawa jamaa, ni kweli wapo vizuri ila si kwa ukubwa huo mnawapa. Taatifa yenyewe ya kuvamiwa alipewa na m - US mnapata picha gani?
Russia ni dude la kutisha
Hizo nchi za Magharibi wanajaribi kuwahadaa kwa kutumia ISIS lakini hawajui intelenjesia ya Russia iko juu

Hapo wameyakanyaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mrusi hana historia kama za hao jamaa , hadi akupige ni kwamba umemuingilia kwenye mambo yake, ila ukiwa na 50 zako na yeye anabaki na 50 zake,,wakina Napoleon na ubabe wao wote walipoenda urusi wakatulizwa, huyo mjerumani nae pia hivyo hivyo, hata hujiulizi kwa nini warumi walitawala hadi waarabu ila hawakwenda kuwatawala warusi
Wahenga walishauri kwamba Mti mkubwa huangushwa kwa hatua ukianzia na matawi yake ndipo mwisho unakata shina na hatimaye unachimba kisiki na mizizi yake. Hatua (Awamu) ya Anguko la Urusi (zamani USSR)lilishakamilika (100%) kwa USSR kusambaratika na kubakiza jina la Urusi. Urusi ya sasa ( cf shina na kisiki) ndo hiyo kila siku ni vita isiyoisha. Itafika mahali (hatimaye) Urusi itanyong'onyea i.e itakuwa dhaifu na wananchi wake watachoshwa na vita na wataigeukia Serikali yao na kuwaondoa madarakani hao waliopo wapenda vita.
 
Dude la kutisha wamepigwa mchana kweupe tena pale pale town. Acheni kuwa overrate hawa jamaa, ni kweli wapo vizuri ila si kwa ukubwa huo mnawapa. Taatifa yenyewe ya kuvamiwa alipewa na m - US mnapata picha gani?
Yani m-US alimpa hiyo Taarifa na kumwangalia (kumpima) kama mwalimu aliyetoa Quiz kwa mwanafunzi wake mjeuri.
 
Back
Top Bottom