Urgent!...ushauri unahitajika kuninusuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urgent!...ushauri unahitajika kuninusuru

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MANYORI Jr, Oct 29, 2012.

 1. MANYORI Jr

  MANYORI Jr Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wanajamvi mi kijana mwenye umri wa miaka 23,kwa sasa ni mwanachuo hapa udsm.nimekuwa na mahusiano na dada mmoja ambaye nimepanga kumuoa aje awe mke halali.mdada huyu ye ni mwalim wa secondary huko mkoani,kabla ya mi kurudi huku dar chuoni nilikuwa naye kwa mda fulan ka week mbili hivi.lakini baada ya mi kuwa nimeondoka watu anaoishi nao wanasema amebadirika kkiasi cha wao kutokumwelewa vizuri!amekuwa akiomba ruhusa za mara kwa mara kwend mjini bila reason maalum,alaf kunatuhuma zngine nyingi tu ambazo yeye amezkana kabisa...hivi sasa mpaka naandika uzi huu yeye hayupo tena kituon amesafiri kwenda kumwona mamake.ila kabla ya kusafiri alinijulisha anakwenda tu nyumban na nilipomuuliza anaenda kufanyeje akasema anataka akaonane na babake aliyeko mwanza...ila jana kabadili na kunieleza anaenda kumwona mamake-mzee na mama hawaishi pamoja.inasemekana kutoka vyanzo vya uhakika kuwa amekuwa na uhusiano hivi karibun na mwalim fulan aliyekuja hapo shulen kwao ksimamia mtihani wa kidato cha nne......jamani nishaurini nifanyeje!? kwa sababu kila nikimuuliza anakataa na kusema haiwez ikatokea hivyo hata siku moja....msinikejeli kwa kuwa hiz ni changamoto za maisha ndani ya mapenz.naomba kuwasilisha uzi huu kwaajili ya msaada wenu tafadhari...
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  calm down......

  fanya uchunguzi kimya kimya... saa nyingine si kila unaloambiwa / unalosikia ni la kweli au likutie presha...

  mfano ukifunga chuo unaweza kwenda kufanya uchunguzi, na angalia mwendo wa mwenzio, amebadilika nk


   
 3. N

  Ngelimunyama Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ivi we ulitaka ule peke yako? Acha ubinafsi waache na wenzio wajipigie, we unadhani utampatia wapi wakumiliki peke yako! Tambua kabisa hyo mwenzio anamoyo wa nyama ivo usishangae akamtamani mwingine akamegwa.ivo ushauri wangu kaka maliza kwanza mishe zako siku ukitulia na kazi yako ndo usake mke, acha kukurupuka!
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono, aendelee na uchunguzi. Mapenzi ni kama kikohozi, huwa hayafichi ipo siku atagundua!
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,143
  Trophy Points: 280
  Kijana wangu Mapenzi ya mbali ni shida mno, trust me. Ukiona dalili za namna hio jaribu kuwa calm kupita kiasi halafu chunguza kimya kimya sana bila kushirikisha mtu mwingine moja kwa moja (yaani usimwambie mtu kuwa hebu nipatie taarifa za fulani) wewe ndenda mdogo mdogo kabisa na kama una mazoea ya kucheki simu yake mkiwa wote, pia acha kabisa, hata ikiita usipokee muite apokee mwenyewe.

  Endelea kumpenda na muaminishe kuwa unampenda na hakuna chochote kibaya unachokiwaza juu yake, unajua kitakachotokea?? Kama ni kweli ni mwizi, utamakamata tu maana hivi vitu kuna kujisahau, kwa njia hii utapata ushahidi original na sio ule wa kuambiwa na watu.

  hata hivyo, ikishindikana, mshukuru kwa muda mzuri mliowahi kuwa nao, then angalia mbele,ni rahisi kwa vijana wa kiume kupata mchumba anaemataka yeye lakini ni HATARI sana kwa binti kumpata mchumba nowadays. Labda wale wa ku-hit and run.
   
 6. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Dah!!! Dunia sasa inaelekea mwishoni.
  Umri uliokuwa nao, na matatizo ya kamapenzi yatakusababishia future yako kuwa mbaya, epuka kuwa katika mahusiano yenye committment kubwa namna hiyo.
  Achana nae huyo mdada.
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Calm down focus on your studies, usichukilie kwa wakati huu hayo unayopitia kwa uzito mkubwa sana. Ndiyo ni mapenzi yanaumiza lakini piga moyo konde na uache kumfuatilia sana. Na kadri utakvyomfuatilia tena hasa kw kupitia watu wengine ndivyo utakavyopata habari mbaya lakini zisizo na ushahidi moja kwa moja na utazidi kuumia.

  Mwisho siku nyingine kama unapata habari kama hizo usimuulizeulize wewe tulia.
   
 8. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  kawaida sana, mwalimu anawaza apate mtoto na kuenjoy, sasa kama kakutana na mwalimu mwenzake ahaaaa..bhaaaaaaas, huna chako kijana, mapenzi is like novel ukisoma unampa na mwingine.
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  Siku hizi umekua?
  Unakula mchicha??

   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  Usimkimbize mwizi kwa makelele
  Mkimbize kimya kimya

  Afu mbona chuo warembo kibao?
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Soma shule ukifunga chuo utamchunguza vizuri mwenyewe, alafu jiepushe kuwashirikisha watu jambo ambalo hata wewe huna uhakika utaishia kuachana tu na mwenzio, ukiwa likizo chunguza mwenyewe tabia zake na utaamua kutokana na wewe mwenyewe unavyo ona moyo wako unataka, kumbuka masuala ya mapenzi ni personal sana huwezi kuamua jambo kutokana na watu wanavyoona wao, kwa mfano mimi kuna mwaka nilisafiri mwaka mmoja na nusu kwenda masomoni nikawa mbali na mpenzi wangu kwa kipindi hicho hicho, niliambiwa mengi sana na watu kuhusu huyu mwanamke lakini kwasababu nilikuwa ninampenda sana na sikuwahi kuthibitisha maneno niliyokuwa naambiwa na watu ikiwemo ndugu zangu, mimi niliamua kuendelea naye na nikamuoa kwasasa ndoa yetu ina zaidi ya miaka kumi na tuna watoto wawili hatukwaruzani sana japo migogoro midogomidogo ya kindoa ipo katika ndoa karibu zote, japokuwa inawezekana kabisa mambo niliyoambiwa yalikuwa ya kweli kwamba alikuwa anacheat lakini sikuweza kufanya maamuzi bila uthibitisho, ningekuwa nimeudhulumu sana moyo wangu kwa kuamua Jambo kisa tu John na Ally wao wanaona mpenzi wangu hafai
   
 12. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Nimeiba pasiwedi yako
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  Ukiiba pasiwedi yangu ya jf, najinyonga

  Bora nikupe ya ATM

   
 14. SWEEPER

  SWEEPER JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nenda darasani! Acha ujinga
   
 15. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Siyo ushauri mzuri,afadhali ungepita kimya!
   
 16. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  hapana Kongosho,mtani wangu platozoom anakula sana migebuka!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Piga buku kijana achana na mapenzi utayakuta tu, ukiendekeza wataku-discontinue hapo utatia akili sasa.....!!:whistle:
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,665
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Kijana mapenzi na shule vimekatazwa....msikilize mbarak mwinshehe (RIP)
   
 19. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Hapana nakula sana likolo
   
 20. d

  domiki4h Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wadau " usiulizie sana kwa watu" wengi hawapendi uhusiano wenu. kama unataka ukweli mshirikishe Mungu kwa maombi. pia unaweza kwenda msalimia bila kumtaarifu lazima utagundua tu kitu. Pio wakikupa taarifa zake waambia unahitaji ushahiidi.
   
Loading...