Jamani ushauri wenu unahitajika, Graduation inataka kunitoa roho

Jamani ushauri wenu unahitajika, Graduation inataka kunitoa roho

puker

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
1,057
Reaction score
2,192
Naamini hamjambo, bila kuchelewa niende Moja Kwa Moja kwenye mada. Yupo mdogo wangu wa kike wa mwisho, tulimpeleka short course mambo ya ufundi wa umeme wa magari. Mungu kamsaidia amemaliza salama, Sasa kesho kutwa wana maafali.

Sasa Mimi kama kaka, alinishirikisha kuhusu hilo, nikalipokea na nikamuahidi kushirikiana nae kadri nitakavyojaliwa ila ukweli ni kwamba naenda mwaka wa pili Sasa Hali yangu ya kiuchumi ni mbaya mno.

Ukilinganisha na status niliyokuwa nayo na mambo anayohitaji kifanyiwa mdogo wangu, kiukweli naona ni aibu isio na kichwa Wala mguu, nimemshauri akachukue cheti kimya kimya, then swala la kumpongeza tutalifanya hata siku nyingine, hapa ndio kajaa upepo hataki kusikia la mhazini Wala la mnadi swala,

Sasa ndugu zangu binafsi najua atajisikia vibaya Mimi kutokuwepo lakini sioni kama ni busara kulazimisha vitu ambavyo binafsi sioni kama ni muhimu kulingana na Hali ya mifuko yetu, kwanza anataka mavitu mengi complicated ambayo sioni kama yanamsingi kama Iko cheti, hebu nipeni uzoefu na busara katika hili.
 
cbbd89acd5c44315ad01274980ff1ad7.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom