Uratibu mbaya wa makadirio ya kodi ndiyo sababu kubwa ya ukwepaji kodi

Serikali ndio watu wa kwanza tuwalaumu na wanakosesha nchi mapato Kwa kuandaa sera mbovu zilizopitwa na wakati na serikali huwarudisha nyuma kimaendeleo Kwa kuweka viwango vibovu vya kodi na mianya ya Rushwa na kubaki kudandia kila kitu Kwa kukurupuka, angalia mfano calculator ya TRA kwenye magari yanayotoka nje kuja ndani yaani nchi haitengenezi hayo magari lakini kodi inakua maradufu hio ndio tunaita wanabaki kudandia tu bila kufikiria, Kwa mfano ruhusu watu waagize magari, walipe ushuru kiasi huku ukizingatia mazingira na uelewe wengi wakiwa na vyombo vya moto utauza mafuta mengi na vipuri hapo mzunguko utakuepo
 
Kingine watoe muda wa kipindi cha miezi mitatu Kwa biashara mpya, hii maana yake itaondoa ukiritimba wa migogoro ya kikodi Kwa wahusika wote, haiwezekani biashara inaanza leo na leo hiyohiyo ukadirie kodi hapana hapa unaandaa mazingira ya ukwepaji na ukumbuke biashara ina majira yaani high season na low season, hivo mamlaka iwakuze wafanyabishara wawe wakubwa huku wakiwapa elimu ili waone fahari kulipa kodi,
Mkuu,HIli Pia Lipo Ndani ya Uwezo wa TRA Tanzania Miezi mitatu inawezekana Kabisa.
 
Makusanyo ya kujikosesha , haya Rwanda hapo mtalii kutoka popote duniani halipii visa maana wanajua mtalii huyu atalala kwenye mahotel yao, atakula vyakula Kwa pesa na atakunywa pesa itabakia kwao, kwenye utalii tu mkiweka free visa entry mtaona ongezeko kubwa la watalii
 
Umeeleza vizuri sana, lakin ata wewe bado hujafahamu aina za kodi ya mapato na rate zake. You should understand that administration ya kodi sio rahisi kabisa kidunia. Hakuna nchi isiyokuwa na migogoro ya kodi duniani tunatofautiana tu ktk Mamlaka za kikodi na usimamizi wake. Mfanyabiashara or Income earner anafanya kila hila kuficha mapato yake na Mamlaka au serikali inafanya kila hila kufichua mapato yake katika namna za kisheria mifumo ya kodi. 30% rate hiyo ni income tax rate inayotozwa kwa makampuni kwenye faida na mfanyabiashara binafsi anatozwa 3.5% tu kwa mapato yake ya mwaka mzima. Bado huyo hyo mfanyabiashara anayo room ya kujikadiria kodi yake na kuwasilisha TRA(Provisional assessment) na akawasilisha final return. TRA wapo wazi sana tatizo ni compliance ya kodi tu Tanzania ni ndogo. Siasa nayo ina athari kubwa sana kwenye eneo la kodi
Mkuu Hii kodi yako ya 3.5% sijaielewa ingawa nahisi unazungumzia Kodi ambayo inatozwa kwenye Gross revenue yaani Mapato bila kuzingatia matumizi.Nakubaliana na wewe kwamba Afisa wa kodi na mlipa kodi ni Paka na Panya na Compliance ya Kodi kwa Tanzania iko chini.

All in all Sidhani kama Tatizo liko TRA,TRA ni wasimamizi wa sheria ambazo huwa zinatungwa na BUnge ambalo ndilo linalote sheria zao KODI ambazo ni Ngumu kwa TRA na walipa Kodi kuzisimamia bila kuathira Uchumi na kuumiza wafanyabiashara.All in all Tuendelee Kujadili Naamini kabisa TRA huwa wanapita huku na wanaweza kuongeza machache na Kuboresha Panapofaa.
 
Mimi ni mtaalamu wa fedha na kwa mawazo yangu tatizo la kodi na TRA linaanza na uratatibu mbaya wa ukusanyaji wa kodi. Kuna kodi za aina mbili kubwa

1. Kodi za mauzo. Kwenye kodi hizi ambazo kwa ulewa wangu ni 18% mlipa kodi sio mfanyabiashara mfano mwenye duka. Mlipa kodi ni mnunuzi na mwenye biashara anatakiwa kuweka kodi pembeni na kuwapa TRA kisheria au kwa lugha ya kitaalamu hii kodi ni withholding tax. Sasa kuna watu wanafikiri mlipa kodi hii ni mwenye duka na imefika wakati mpaka wauzaji wanafikiri wenyewe ni walipa kodi hii kumbe sio hivyo mlipa kodi ni mnunuzi. Hivyo mfanyabiashara anauza kitu Tsh 1000 anatakiwa aweke kodi ya 18% na mnunuzi kulipa Tsh 1,180 na hiyo Tsh 180 hajalipa yeye ni mnunuzi na sio pesa yake.

2. Kodi ya mapato ni kodi za wafanyabiashara. Hizi ni kodi ambazo zinatoka kwenye faida ya biashara. Yaani baada ya mfanyabiashara kutoa matumizi yote na kubali na faidi kuna kodi anatakiwa kulipa ya mapato. Sina uhakika na % lakini inatokana na ukuwa na aina ya biashara. Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi.

Tatizo Tanzania ni hizo kodi za namba 1. Mtu wa TRA badala ya kukagua vitabu vya risiti anaenda kwa mfanyabiashara na makadirio. Sasa makadirio ya nini wakati sheria inataka kila mtu atoe risiti. Na kama kuna risiti basi kiasi cha kodi kinajulikana kuna haja gani tena kuwatuma wafanyakazi na makadirio. Sasa mfano risiti zinaonyesha kodi ambazo wateja wamelipa za kwenda serikalini ni Tsh 10M hawa mafisadi wa TRA wanakuja na makadirio ambayo hatujui yametoka wapi ya kodi ya Tsh 20M halafu wanamwambia mwenye biashara kwamba tupe Tsh 2M halafu lipa kodi Tsh 5M Hivyo serikali inapungukiwa Tsh 3M. Lakini kibaya zaidi mwizi huyo huyo bado analipwa pesa na mshahara wake kwenye hiyo Tsh 7M. Sasa kama nchi tutaendeleo vipi kwa utaratibu huu?

1. Serikali badilisheni utaratibu toeni ujinga wa makadirio
2. Wekeni sheria kali kwa wala rushwa
3. Wekeni sheria kali kwa wafanyabiashara watoa rushwa mfano toeni hongera kama mfanyabiashara akiweza kumleta mla rushwa
4. Wekeni utamaduni na onyo kwa utamaduni wa rushwa
Kwa haya maelezo uliyotoa hilo neno Mtaalam wa Fedha liondoe hakuna mtaalam wa fedha hasiyekuwa conversant na maswala ya Tax. Huna unachokijua kuhusu kodi rudi kajifunze tena na kujifunza sio ujinga. Soma Income tax Act na marejeo yake, kasome Tax administration Act na marejeo yake, kasome Vat act.
 
Shida kubwa ni ufisadi kwenye matumizi ya kodi kusanywa.
Kila mtu angetamani kulipa kodi kama tungeweza kudhibiti wizi na ufisadi wa kodi kusanywa,kama kodi ingetumika kwa manufaa ya wote.
Mtu akishajua kodi yake inaenda kunufaisha wachache na familia zao,kamwe hawezi kuwa na morale ya kulipa kodi na ikitokea loophole lazima ataitumia kukwepa kodi.
 
Kwa haya maelezo uliyotoa hilo neno Mtaalam wa Fedha liondoe hakuna mtaalam wa fedha hasiyekuwa conversant na maswala ya Tax. Huna unachokijua kuhusu kodi rudi kajifunze tena na kujifunza sio ujinga. Soma Income tax Act na marejeo yake, kasome Tax administration Act na marejeo yake, kasome Vat act.
Yuko Sahihi Finance ni mwamvuli Tax ni taaluma na Accounts au Uhasibu ni Taaluma
 
Mkuu Hii kodi yako ya 3.5% sijaielewa ingawa nahisi unazungumzia Kodi ambayo inatozwa kwenye Gross revenue yaani Mapato bila kuzingatia matumizi.Nakubaliana na wewe kwamba Afisa wa kodi na mlipa kodi ni Paka na Panya na Compliance ya Kodi kwa Tanzania iko chini.

All in all Sidhani kama Tatizo liko TRA,TRA ni wasimamizi wa sheria ambazo huwa zinatungwa na BUnge ambalo ndilo linalote sheria zao KODI ambazo ni Ngumu kwa TRA na walipa Kodi kuzisimamia bila kuathira Uchumi na kuumiza wafanyabiashara.All in all Tuendelee Kujadili Naamini kabisa TRA huwa wanapita huku na wanaweza kuongeza machache na Kuboresha Panapofaa.
Safi sana kiongozi nikupongeze sana wewe inaonesha kodi unaijua vizuri sana alaf sio mtu wa kujitweza na unapenda kujifunza. Hii rate ya 3.5% ni rate ya income tax inatozwa kwenye mauzo ghafi ya mfanyabiashara asa wale wanaotunza mauzo ya bidhaa zao. Lakini akitaka kujikadiria sheria zipo wazi atajikadiria kwenye faida anayopata then atawasilisha hesabu za mizania TRA ili zikaguliwe.
 
Nimejibu kama Mlipa kodi bwashee

Wengi hawajui Kwamba kutoza kodi ni Art yaani Sanaa fulani lakini kulipa Kodi ni Sayansi kwa Sababu unaifeel kibiology katika mfumo wako wa hisia

Walipakodi huwa tunahitaji management fulani Hivi kimwili na Kiroho 😄😄
Jomba umeongea ukweli mtupu. Kuna jamaa fulani alimwaga machozi kwenye ofisi za TRA Manzese kabla hazijahamishiwa Shekilango. Yaani kama kisaikolojia hauko sawa utaishia kupata presha wakati wa kulipa kodi. Njia sahihi ya kutovurugwa na wajomba wa TRA ni kuwafuata ofisini kwao kila inapotokea kufanya hivyo.
 
Safi sana kiongozi nikupongeze sana wewe inaonesha kodi unaijua vizuri sana alaf sio mtu wa kujitweza na unapenda kujifunza. Hii rate ya 3.5% ni rate ya income tax inatozwa kwenye mauzo ghafi ya mfanyabiashara asa wale wanaotunza mauzo ya bidhaa zao. Lakini akitaka kujikadiria sheria zipo wazi atajikadiria kwenye faida anayopata then atawasilisha hesabu za mizania TRA ili zikaguliwe.
Upo Sahihi Kabisa,Je unafikiri kuna Tatizo katika Mfumo wetu wa Presumptive Tax System hasa katika Usimamizi wake?Je kwa Unavyoona hii 3.5 inayotozwa kwenye Mapato ghafi ambayo kwa mtu mwenye gross ya Milioni 100 atalipa 3500,000 iko Poa?Binafsi naona bado kuna maeneo mengi sana ambayo yanahitaji Maboresho ya kodi hasa katika Viwango.Mtu mwenye Mapato Ghafi ya Milioni 100 kwa Mwaka kuna uwezekano Faida yake kwa mwaka ikawa ndogo sana kwa kutegemea aina ya Biashara na eneo alipo.Sasa Jaribu kufikiri huyu mtu anapaswa Alipe ada ya Mtoto wake alipe Bili za Umeme na Maji,ALipe gharama za Usafiri,ALipe Wafanyakazi,Alipe Tozo mbalimbali,Ale Alishe Familia Yake,Asaidie ndugu Jamaa na MArafiki,Je Unafikiri Milioni Mia ni nyingi kiasi cha serikali kutaka Ipewe Milioni 3.5 na kisha baada ya Hapo huyu bwana aendelee?Tunajadili Tu hiki kiwango kwa sababu najua wewe unaweza kukiona ni Kidogo ili kwenye Biashara ni kwango kikubwa sana.
 
Yuko Sahihi Finance ni mwamvuli Tax ni taaluma na Accounts au Uhasibu ni Taaluma
Kwa hayo maelezo yake aliyotoa hayupo sahihi ata kidogo huwezi kuwa mtaalam wa fedha alaf ukakosa knowledge kwenye eneo la kodi. Hivi tunavyo viongelea hapa ni vitu basic sana kwenye kodi mtaalam wa fedha yeyote lazima awe conversant navyo. Utamshauri vipi mtu/kampuni kuhusu maswala ya Fedha pasipo kuzingatia athari za kodi.
 
Kwa haya maelezo uliyotoa hilo neno Mtaalam wa Fedha liondoe hakuna mtaalam wa fedha hasiyekuwa conversant na maswala ya Tax. Huna unachokijua kuhusu kodi rudi kajifunze tena na kujifunza sio ujinga. Soma Income tax Act na marejeo yake, kasome Tax administration Act na marejeo yake, kasome Vat act.
Nafikiri Kwa sababu kaleta Mjadala Mzuri Tusihoji kuhusu Yeye(Huyu bwan yuko JF Tangu 2006),Tubaki na Hoja zake na Pale ambapo tunaona kuna mambo hajaweka sawa Tuboreshe Ili na Yeye aendelee Kuelimika na sisi wengine Tuendelee Kuelimika.Binafsi huwa nakwepa sana Kuharibu nyuzi zenye elimu kama hizi kwa kujaribu Kumuattack mtu ispokuwa katika Mzaha wa kawaida wa kuchangamsha Mjadala.Humu JF Tunaweza Hata Kujipa PHD wenyewe kwa wenyewe.Si Unaona JF wamekuita Expert,Na Yeye Wamemuita Platinum?All in All Naamini kwamba na Yeye ataendelea Kujifunza kama kuna maeneo ambayo bado hajazama vizuri
 
Upo Sahihi Kabisa,Je unafikiri kuna Tatizo katika Mfumo wetu wa Presumptive Tax System hasa katika Usimamizi wake?Je kwa Unavyoona hii 3.5 inayotozwa kwenye Mapato ghafi ambayo kwa mtu mwenye gross ya Milioni 100 atalipa 3500,000 iko Poa?Binafsi naona bado kuna maeneo mengi sana ambayo yanahitaji Maboresho ya kodi hasa katika Viwango.Mtu mwenye Mapato Ghafi ya Milioni 100 kwa Mwaka kuna uwezekano Faida yake kwa mwaka ikawa ndogo sana kwa kutegemea aina ya Biashara na eneo alipo.Sasa Jaribu kufikiri huyu mtu anapaswa Alipe ada ya Mtoto wake alipe Bili za Umeme na Maji,ALipe gharama za Usafiri,ALipe Wafanyakazi,Alipe Tozo mbalimbali,Ale Alishe Familia Yake,Asaidie ndugu Jamaa na MArafiki,Je Unafikiri Milioni Mia ni nyingi kiasi cha serikali kutaka Ipewe Milioni 3.5 na kisha baada ya Hapo huyu bwana aendelee?Tunajadili Tu hiki kiwango kwa sababu najua wewe unaweza kukiona ni Kidogo ili kwenye Biashara ni kwango kikubwa sana.
Of course tatizo lipo kuna haja ya kupitiwa. Lakini kuna option ya huyu mfanyabiashara kujikadiria kodi, although kisheria threshold ya mfanyabiashara anayepaswa kujikadiria lazima ianzie 100m. Tatizo ni Elimu na hawa wafanyabiashara wanapenda njia za mkato.
 
Mkuu,Sasa nafikiri TRA watafurahi sana kusikia Mapendekezo yetu ya nini kirekebishwe,nini kiondolewe,nini kipunguzwe,nini Kiboreshwe n.k.Nimetoa Baadhi ya maeneo ambayo nimeona yakipunguzwa yaaleta Ahueni.Mimi Kwa Mtazamo wangu naamni Kabisa Mtanzania atozwe kodi ambayo itahamishwa biashara kukua,Itavutia uwekezaji,Itarahisisa Ulipaji,Itaondoa Usumbufu na Mamlaka.
 
Upo sahihi Mkuu, nafurai nimejifunza kitu kutoka kwako kupitia haya maandishi🙏
 
Umeeleza vizuri sana, lakin ata wewe bado hujafahamu aina za kodi ya mapato na rate zake. You should understand that administration ya kodi sio rahisi kabisa kidunia. Hakuna nchi isiyokuwa na migogoro ya kodi duniani tunatofautiana tu ktk Mamlaka za kikodi na usimamizi wake. Mfanyabiashara or Income earner anafanya kila hila kuficha mapato yake na Mamlaka au serikali inafanya kila hila kufichua mapato yake katika namna za kisheria mifumo ya kodi. 30% rate hiyo ni income tax rate inayotozwa kwa makampuni kwenye faida na mfanyabiashara binafsi anatozwa 3.5% tu kwa mapato yake ya mwaka mzima. Bado huyo hyo mfanyabiashara anayo room ya kujikadiria kodi yake na kuwasilisha TRA(Provisional assessment) na akawasilisha final return. TRA wapo wazi sana tatizo ni compliance ya kodi tu Tanzania ni ndogo. Siasa nayo ina athari kubwa sana kwenye eneo la kodi
Mkuu,Uko Sahihi,Matumizi ya Neno,Mimi ni Mtalaamu wa.....Yanavuta Hisia na Kujenga Msingi Mkubwa Na Unapojitambulisha Hivyo hakikisha Unaonesha Utaalamu wako.Kauli yake imenifanya nipitie nyuzi zangu zote niangalie kama nimewahi kuanza uzi na Hiyo Kauli ya "Mimi ni Mtaalamu wa......'

Umenifumbua.Nafikiri Kamundu Ameelewa Ukakasi uliojitokeza..
 
Kwa hayo maelezo yake aliyotoa hayupo sahihi ata kidogo huwezi kuwa mtaalam wa fedha alaf ukakosa knowledge kwenye eneo la kodi. Hivi tunavyo viongelea hapa ni vitu basic sana kwenye kodi mtaalam wa fedha yeyote lazima awe conversant navyo. Utamshauri vipi mtu/kampuni kuhusu maswala ya Fedha pasipo kuzingatia athari za kodi.
Ni kweli Taxation ni Somo kwenye Course zote za Uhasibu
 
Back
Top Bottom