Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,086
Sidhani kama kwenye kikao cha sasa, nia ni kutoka na majina ya wagombea. Hatua ya kwanza ni kukubaliana na vigezo vitakavyotumika. Vigezo vikishakubalika, basi kazi itakuwa imekwisha.
Mapendekezo yangu, kwa nafasi za udiwani na ubunge, vigezo vinavyoweza kutumika, ni kama ifuatavyo:
1) Idadi ya kura ambazo chama kilipata katika eneo husika kwa nafasi ya ubunge, urais na udiwani mwaka 2010
2) Idadi ya kura ambazo chama kimepata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014
3) Majimbo ambayo chama kimojawapo cha upinzani kilichopo kwenye UKAWA kinashikilia yaachwe kwenye chama hicho kutoa mgombea
Kwa nafasi ya Urais, vigezo vya chama gani kitoe mgombea wa Urais, viwe kama ifuatavyo:
1) Idadi ya kura ambazo chama kilipata kwa nafasi ya Urais 2010
2) Idadi ya jumla ambayo chama kimepata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2015
3) Uungwaji mkono wa chama katika maeneo/mikoa yenye wapiga kura wengi
4) Mtandao wa chama mpaka ngazi za chini
5) Matokeo huru ya chama kinavyokubalika kwa nchi nzima
6) Chama kilichokubalika kutoa mgombea wa kiti cha urais, kikishamteua mgombea, kirudishe jina la mgombea kwa wanachama wa UKAWA, na apimwe kukubalika kwake kwa wanaukawa wote
7) Matokeo huru namna mgombea anavyokubalika kwa umma

Hapo watakua wamepiga nyoka kichwani.waanze jimbo kwa jimbo,mkoa kwa mkoa.na washirikiane kampeni.