Mingoi
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 11,715
- 6,119
Waliotangulia wako akhera bhana.Hata mie namshauri zitto afuate mawazo ya waliomtangulia
Waliotangulia wako akhera bhana.Hata mie namshauri zitto afuate mawazo ya waliomtangulia
Mkuu wangu chama,
Ndani ya Chadema makundi yapo wala sio siri tena, Edwin Mtei, hawezi kumwambia hayo maneno mkwe wake Mbowe wala Dr Slaa, kamwambia Zitto sababu sio chaguo lake.
Hivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?(Sababu ni muislamu au?). Jee mnajua CCM itamsimamisha Membe?(Waislamu hawatampigia kura Membe sababu ni mkristo), sasa kwa vile huyo mgombea kipenzi wetu na Membe hawana tofauti katiuka zile kampeni za "kivile",(wote wakristo (Membe na Slaa) na hamjajua kwa mujibu wa katiba mpya, ili chama kishinde urais wa JMT, lazima kipate angalau theluthi moja ya kura za Visiwani!(99% Waislamu), hivi huyo mgombea wenu kipenzi (Dk Slaa-Mkristo), kwa siasa zetu "zile", hizo theluthi ya kura kutoka visiwani zinatokea wapi?!.Mkuu Molemo, alichofanya ZZK sio kutangaza kugombea urais kupitia Chadema, bali kutangaza nia ya kuiomba Chadema kumpitisha kama mgombea wa Chadema 2015!. Naomba sana utofautishe kati ya "kutangaza nia" na "kutangaza kugombea"!.
ZZK alipotangaza nia, mimi nilimuunga mkono na kutangaza nia ni jambo jema na jambo la kheri na nikatoa wito kabisa kuwa kila mwenye nia na aitangaze!, hivi kuna ubaya gani?. Hebu kanisome hapa Urais 2015 tusimlaumu Zitto; Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa ...
Lakini ZZK alipojitangaza rasmi kuwa hagombei tena ubunge na badala yake "atagombea urais kupitia Chadema" nilimpinga!. Nilimwambia wazi, that was wrong!, hakupaswa kujitangazwa, bali alipaswa tuu kuonyesha vitendo vya ki presidential candidate ndani ya chama, ili wenzake ndio wamuone na kumuomba agombee na sio kujipigia debe na hapa nilimtahadharisha Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!. Wenye uwezo wa kumtangaza mgombea ni Chama na sio mwan achama individual!.
Ila lazima mkubali, mkatae, ndani ya Chadema kuna double standards za hali ya juu!, kuna baadhi ya mambo yakifanywa na kina fulani ni halali, ila wakifanya kina fulani inageuka ningwa!.
Tatizo ni kuwa ndani ya mioyo ya wana Chadema wengi, wanaye mgombea wao mioyoni mwao, sio tuu kuwa mgombea huyo anakubalika sana kwao, bali anaabudiwa!. Kitendo cha ZZK kujitokeza anaonekana kama kumkufuru huyo mungu mtu anaye abudiwa!. Na kwa wasio jua, mimi naujua msimamo wa huyo mgombea wenu kipenzi kuhusu kugombea au kutogombea urais na usome hapa Msimamo wa Dr. Slaa Kwenye Urais 2015 ...
Unashauri kamati kuu itoe miongozo, hivi kumbe Chadema haina demokrasia ya kila mwanachama yoyote kugombea nafasi yoyote ni mpaka kamati kuu itoe miongozo!.
Tena kwa vile ZZK ni rafiki yangu, na kabla hata ya huo urais kuna uchaguzi wa viongozi wa Chadema, nitamshauri agombee tena Uenyekiti na this time hakuna kujitoa mpaka kieleweke!.
Hivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?. Jee mnajua CCM itamsimamisha Membe?, sasa kwa vile huyo mgombea kipenzi wetu na Membe hawana tofauti katiuka zile kampeni za "kivile", na hamjajua kwa mujibu wa katiba mpya, ili chama kishinde urais wa JMT, lazima kipate angalau theluthi moja ya kura za Visiwani!, hivi huyo mgombea wenu kipenzi, kwa siasa zetu "zile", hizo theluthi ya kura kutoka visiwani zinatokea wapi?!.
ZZK anakubalika sana kutokana na kuendesha "strategic politics" kwa urafiki wake na January Makamba, atazivuna kura zote za vijana wa CCM!, kwa urafiki wake na Jussa, atazivuna kura zote za CUF kule visiwani. Kwa usomi wake, atazivuna kura zote za vijana/wasomi na wataka badiliko ya kweli with clear goals na right strategies!.
Nashauri, baada ya Mzee Mtei kukikabidhi chama kwenye "safe hands" za mkwewe, his advisory role yake ibaki limited kwa insiders tuu wa chama na sio ku express his public opinion publically as if chama bado ni chake!. Heshima yake kama muasisi ipo pale pale, lakini kwa sasa chama sio chake tena, sasa chama ni cha wanachama!, tena Mwenyekiti Mbowe anatakiwa kujipambanua kabisa kwa hili kuwa "amekata kabisa zile mothers apron strings" ili isje onekana kina Mzee Edwin Mtei ndio bado wanaendesha chama by proxy kupitia kwa wakwe zao!.
Ili chadema kuonysha ina "practice what it preach" lazima iache democracy i prevail!.
Go ZZK Go!.
Pasco.
Mkuu wangu chama,
Ndani ya Chadema makundi yapo wala sio siri tena, Edwin Mtei, hawezi kumwambia hayo maneno mkwe wake Mbowe wala Dr Slaa, kamwambia Zitto sababu sio chaguo lake.
kwanini habari zote zimeandikwa na gazeti moja tu?tafakari
Mwasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Edwin Mtei amemuonya mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuacha kutangaza mambo ya Urais sasa kwani anasababisha mpasuko ndani ya CDM na badala yake ajikite kukijenga chama mpaka muda utakapofika ili chama kitoe utaratibu.
Mzee Mtei amesema amemshauri mara kadhaa Zitto umuhimu wa kutulia kama wenzake ndani ya chama na kukijenga chama lakini mbunge huyo amekuwa mkaidi na hasikii.
Pia Mzee Mtei amesema endapo mbunge huyo ataendeleza harakati zake za kutaka umri wa Urais ushuke hadi miaka chini ya 40 ili tu yeye apate nafasi ya kugombea basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia na mwenye uroho mkubwa wa madaraka.
Akijibu madai hayo ya Mzee Mtei, Zitto Kabwe amemuonya Muasisi huyo wa chama na amewataka wazee ndani ya CHADEMA kuheshimu Demokrasia na kusema anaamini ni yeye atakayeweza kuishinda CCM mwaka 2015 na anataka Mzee Mtei akiwa bado hajafa amshuhudie jinsi atakavyobadili nchi akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Source: Mwananchi Jumamosi.
My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.
Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
duh...kwa hiyo dini ndio factor kubwa ya kupigiwa kura!!!!tumekwisha tzHivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?(Sababu ni muislamu au?). Jee mnajua CCM itamsimamisha Membe?(Waislamu hawatampigia kura Membe sababu ni mkristo), sasa kwa vile huyo mgombea kipenzi wetu na Membe hawana tofauti katiuka zile kampeni za "kivile",(wote wakristo (Membe na Slaa) na hamjajua kwa mujibu wa katiba mpya, ili chama kishinde urais wa JMT, lazima kipate angalau theluthi moja ya kura za Visiwani!(99% Waislamu), hivi huyo mgombea wenu kipenzi (Dk Slaa-Mkristo), kwa siasa zetu "zile", hizo theluthi ya kura kutoka visiwani zinatokea wapi?!.
ZZK anakubalika sana kutokana na kuendesha "strategic politics" kwa urafiki wake na January Makamba(Muislamu), atazivuna kura zote za vijana wa CCM!, kwa urafiki wake na Jussa(Muislamu), atazivuna kura zote za CUF (Wanachama wake karibia woote waislamu) kule visiwani. Kwa usomi wake, atazivuna kura zote za vijana/wasomi na wataka badiliko ya kweli with clear goals na right strategies!.Nafikiri mtakuwa mmemuelewa kwanini anataka ZITO awe Rais,Viongozi wa CHADEMA haya ndio baadhi ya mawazo ya wanachama wenu kaeni chini muyapatie ufumbuzi!VIVA CDM!
Pengine safari hii atasikiliza huu ushauri. Ameamua kwa makusudi kuwa CONFUSER.
Dawa ya watu wa namna ni kuwatimua mapema, ni bomu zito litakalolipuka mbele ya safari.
Hana nia njema, alikuwa mpambabaji, now he has changed, likely cz has interests to protect.
Shame on mzee Mtei!
Chama
Gongo la mboto DSM
Kwa hiyo ndani ya Chadema ni marufuku kutangaza kugombea urais.