Uraibu wa urembo bandia (artificial beauty) kwa mwanamke wa kiafrika ni ugonjwa kamili wa kiakili

Uraibu wa urembo bandia (artificial beauty) kwa mwanamke wa kiafrika ni ugonjwa kamili wa kiakili

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,071
Kama ulikuwa hujui tu, uraibu wa urembo bandia kwa mwanamke wa kiafrika ni ugonjwa kamili wa kiakili kwa sasa.

Hapa ninazungumzia ile hali ya kubadili rangi na unyororo wa ngozi (wanaita kuglow!), kupashika kucha bandia, nywele bandia (rasta, weaving nk), kope bandia, kupiga jeki matiti, kupachika makalio bandia, kutengeneza picha bandia (kuweka filters), kufanya operesheni za kubadili maumbile nk.

Kadri mwanamke wa kiafrika anapopitia msongo mkubwa wa mawazo wa kuhisi kutokukubalika (kutokuvutia watu wengine) ndivyo anavyoshindwa kujikubali na kujipenda vile alivyo na kwa haraka ndivyo anavyoingia kwenye mtego wa tatizo la kitabia kutaka kufanana na mtu mwingine na mwisho uingia katika uraibu wa urembo bandia.

Hapa chini ni dalili kamili za hiyo hali, ikiwa mhusika angalau amekuwa nazo kwa uchache wa miezi sita mfululizo

1. Kutokutaka muonekano wako wa kiasili kujulikana tena mbele za watu.

2. Kutaka kuishi muda wote katika muonekano urembo bandia.

3. Kujiamini ukiwa tu katika muonekano urembo bandia.

4. Kutokujiamini ukiwa tu katika muonekkano wako wa kiasili.

5. Kutumia rasimali nyingi/kubwa (muda, pesa) ili kutafuta urembo bandia. (Urembo bandia kuwa ni jambo la kufa na kupona kwako)


Note:
Hii hali haichagui elimu, dini, kipato huku zaidi ikiwaathiri vijana na watu wa makamo (miaka 18-50), jamii za kiafrika popote duniani zikiwa ndio waathirika namba moja, huku kukua kwa teknolojia ikiwemo mitandao ya kijamii, programme za kusanifu picha (filter) na soko huria na holela la bidhaa na huduma za urembo.

Ikiwa ni wewe, ndugu yako, mke wako, rafiki yako, jirani yako anapitia hizo hali, basi tambua huyo ni mhanga tayari. Ukiweza mshauri kuonana na mtaalamu wa afya ya Akili ili kupata msaada mapema.
 
Hiyo Hali ni mbaya na inagharimu sana fedha nyingi na muda
Ukienda DRC mpaka baadhi ya wanaume wako kwenye uraibu huo hasa wanamuziki
 
Back
Top Bottom