Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Heko chifu wangu. Hizo ni kama bilioni 16 katika pesa za madafu....si haba ati.
Angalau tunaanza kuelekea kwenye muafaka.....
Sasa onyesha (kwa takwimu halisi ama hata projections) pia baada ya uwepo wa uraia pacha ni kiasi gani kitaongezeka katika hiyo bilioni 160?!?
Naomba nieleweke tena kwamba, hili la uraia pacha linanigusa katika ngazi ya familia. Lakini unapokuja mjadala wa uraia pacha katika engo ya kiuchumi, naogopa kuweka hisia katika kujadili.
Katika uchumi mkubwa hapo ndipo penye shida kwangu......na hili la uchumi mkubwa ndio imekuwa hoja ya bwana Membe na wenzake akina Nyerere (yule mama wa viti maalumu wa CHADEMA).