Uraia wa nchi mbili na Rasimu ya Katiba Mpya: Toa maoni yako

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,177
1,195
hii ndo hoja ambayo tuliililia kila cku. Safi sana, wale wasioutaka kisa tu wanahisi hawawezi kutoka nje ya nchi hata cku moja hoja zao ni soft sana, simply wanasumbuliwa na wivu wa aina ilosemwa na Mkapa kule mgodini wakati akiwa bado rais
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Naunga mkono hoja. Sasa utawasikia wanoko Watanzania wenye uraia wa nchi mbili wataongeza ujambazi nchini, waliikimbia nchi hawa ni traitors wabaki huko huko waliko, wanataka kufaidi kule na huku blah blah blah blah!!!!! Wakiukubali au kuukataa uDC Watanzania wa leo si wale wa mwaka 47 watakaopata bahati ya kuuchangamkia uraia wa nchi waitakayo hawatalaza damu.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,040
2,000
Kwa mara ya kwanza rasimu iliyo kabidhiwa kwa Rais imependekeza uraia wa inchi 2.

wananzuoni mnasemaje kuhusu hili?

Ni wapi wanaposema kwamba uraia wa nchi mbili umeruhusiwa, maana maandiko hayako wazi .

Paragraph 57 inasema tu kwamba mtanzania ni mtanzania ili mradi tu mzazi wake ni mtanzania wakati wote. Tafsiri yake ni kwamba hata kama umechukua uraia wa nchi nyingine bado utakuwa ni mtanzania kama ulizaliwa Tanzania wakati wazazi wako walukuwa watanzania wakati wa kuazaliwa kwako.

Paragraph 59 ukurasa wa 23 unasema kwamba mtu aliye na asili ya Tanzania, na ambaye ameacha kuwa raia wa tanzania (sijui ni mazingira gani yanaweza kumfanya mtu mwenye asili ya tanzania mwenye passport za nchi nyingine bila kuukana uraia wake wa tanzania na kuendelea kutumia passport mbili.. ya tanzania na ya ugenini ... kutokuwa mtanzania), atakapokuwa tanzania, atakuwa na hadhi kama itakavyo ainishwa katika sheria za nchi.

Ni hadhi gani hiyo inayofichwa hapa? si waseme tu kwamba kuomba visa na mengineyo au kupangikwa siku za kukaa bongo.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,040
2,000
Hebu tuwekee vifungu vya rasimu vyenye kuainisha na kubainisha jambo hili...

Mambo ya Uraia yemeongelewa kwenye ukurasa wa 22-23 sura ya 5 ya Rasimu, paragraph 56-59... technically one page only .. na kuna maswali mengi ya kujiuliza katika uraia huo hata kwa njia nyingine kama ancestrol acquired citizenship.. Uraia wa tanzania ni wa aina mbili tu, wa kuzalia na wa kujiandikisha. Kuna mapungufu mengi hapa kama Uraia utakuwa wa aina mbili hizi pekee.
Ngoja tusuburie bunge la katiba tuone majadiliano yatavyoenda.
 
jogoolashamba

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
348
195
Kwa mara ya kwanza rasimu iliyo kabidhiwa kwa Rais imependekeza uraia wa inchi 2.

wananzuoni mnasemaje kuhusu hili?

Mlipofungua Sekondari za Kata nyingi sana, Mama Margret Sitta akaja na dawa ya Walimu bambucha! Leo mnamlaani vikali sana Kawambwa kwa kushusha kiwango cha elimu. Kawambwa na Sitta wapi na wapi?

Uraia wa nchi mbili Waziri wa Mambo ya Nje akiwa ni Jogoolashamba basi matokeo yake atakuwa lawamani Jogoolashamba, siyo Membe na Mkuu wake. Na ikibidi Jogoolashamba atajiuzulu uwaziri kwa sababu ya matatizo hayo. Tuzoee tu kwenda na kasoro za Wakubwa wetu hata pale tunaona nia yao ni ya ajabu ajabu. Kuona mbali ni kasoro isiyokuwa rahisi kuipambanua.
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
13,072
2,000
Ni mawazo mazuri ingawa kwenye hii sehemu yanaweza kuleta mjadala mkali kule bungeni.

Nimetohoa sehemu hii ya tano inayohusu huu uraia wa asili au nasaba wa Tanzania.

SURA YA TANO URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

Uraia wa Jamhuri ya Muungano.

56
.-(1) Mtu ambaye, kabla ya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa Jamhuri ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili na utapatikana kwa njia ya kuzaliwa au kujiandikisha.

Uraia wa kuzaliwa.

57
.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanganyika au Zanzibar atakuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa kuzaliwa, mama au baba yake ni, au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa mama au baba yake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.

(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.

(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atachukuliwa kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.

(5) Endapo uraia wa wazazi wa mtoto aliyepewa uraia chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4) utabainika kuwa si uraia wa Jamhuri ya Muungano, uraia wa mtoto huyo utasita.

Uraia wa kuandikishwa.

58
.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkaazi wa Jamhuri ya Muungano na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria za nchi anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano na ambaye - (a)

amedumu katika ndoa hiyo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo; na

(b)ametimiza masharti yaliyoainishwa katika sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), anaweza kuomba uraia wa kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(3) Endapo ndoa iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake wa Tanzania, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika ibara ndogo ya (2), atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.

(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake si raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuandikishwa.

(6) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, kusimamia masuala yanayohusu uraia wa Jamhuri ya Muungano.

Hadhi ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania.

59.
Bila ya kuathiri masharti yaliyomo kwenye Sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.

My take:

Tatizo ni pale kwamba mtu ambae alitupa pasi yake ya Tanzania je itakuwaje kama akitakiwa athibitishe uraia wake?
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
1522979_578473035573168_1521793816_o.jpg 1.jpg RASIMU COVER - DESEMBA 2013 001.jpg IMG_7958.JPG

Utambuliwa uraia wa Tanzania
Rasimu ya Katiba Mpya inapendekeza kutambuliwa kwa uraia wa kuzaliwa na kuasiliwa ambao ni wa nchi moja.

Rasimu hiyo inapendekeza pia kuwapa hadhi maalum watu wenye asili au nasaba ya Tanzania walioacha kuwa raia wa Tanzania kwa kuchukua uraia wa nchi nyingine.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
Katika rasimu ya awali ilionekana kutopewa uzito na utetezi ulioletwa ndani ya rasimu ilikuwa kwamba kwa sababu ya mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria za uhamiaji isingefaa liingizwe kwenye katiba, lakini katika rasimu hii ya sasa kuna dalili kwamba Wizara ya Mambo ya nchi za nje na uhusiano wa Kimataifa chini ya Waziri Membe wamefanya jitihada kubwa kushawishi tume ya Warioba na hivyo kuliingiza kwa kigezo cha kuwatambu kwa kuwapa hadhi maalum hao wenye asili ya Tanzania na baadaye wakabadili uraia wa kuzaliwa Tanzania na kuwa raia wa kuasiliwa katika nchi nyingine, hali kadhalika waliokuwa na uraia wa kuasiliwa Tanzania kisha kuamua kuwa raia wa kuasiliwa katika nchi nyingine.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
Utanganyika wetu kwanza........................ Tanzania baadaye

Mimi ni Mtanganyika, tatizo ni kwamba tunakumbatia sana hawa wa kutoka nchi nyingine ambao hawana uchungu na nchi hii wanakuja kuchota na kwenda zao, lakini hawa watanzania wana uchungu na nchi yao, kilichowafanya waingie uraia wa nchi hizo ni kufuata sheria wasiishi isivyo halali. Lakini wanachohangaika na masuala ya maisha na uchumi, wengi wanachohangaika ni kuchuma kisha warudi huku homeland.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,153

Maneno yao tu hayo kuwa wanataka kurudi mkuu mioyoni mwao wanajua kwa tofauti walizoziona huku hawawezi kuishi tena na ndio maana wanataka uraia wa huko wabaki nao ili yakigoma huku waondoke zao tena!!!!!!!!

Iwe mtu akitaka kurudi aukane wa huko apewe hiyo hati kwa probation then apewe uraia!!!!!

Hivi hao wa nje ndio wanaweza kubadili hali ya nchi kuliko tuliomo humu????!!!!
 
Zamani nipokuwa sijabahatika kutembea nchi za nje na kuishi huko nilifikiri na kuwaza kwa mtazamo wako huo, lakini nilipobahatika kufika huko pamoja na kutobadili uraia wa nchi yangu, nimepata kuelewa hali yalisi ya nchi ambako mtu hawana njia ye yote ya kupata ajira na ili aweze kufanikiwa analazimika kuwa na vibali vya kazi ambavyo havitolewi bure ila kwa taratibu za uhamiaji ambazo kuna ndoana zinazowafanya wengi walazimike kunasa ili kuendesha maisha.

Kwa bahati nzuri wengi nilioonana nao na kujadiliana kutoka nchi kadhaa hasa za bara la Ulaya na Marekani wanalilia kwao na kwamba kinachowaweka huko ni kupata cho chote cha kuja kusimamisha vema maisha na familia zao. Kama kuna wanaoona huko ni peponi ni wa kizazi cha Lulu ambao wamefika huko wakati bado bongoni mwao hawajakomaa kupima kwenye mizani mbivu na mbichi.

Mpaka sasa nina ushahidi wa wengi wao kile wanachokipata ni kuja kuwekeza kidogo kidogo home kwa vile mfano pesa nchi za huko mabenki hayana riba nzuri, mfano Marekani interest utapata 0.025% kwa mwaka, na hiyo huishia kwao kwa visingizio mbalimbali wakati bongoland unaanzia na 3% and up. Utaona wengi wao wanaamua kuja kuweka pesa zao kwenye mabanki ya huku nyumbani.

Uwekezaji nao upo kwa sana, kuna wengi wanaoingiza bidhaa toka huko kwao kwa vile wengi wetu huwa vigumu kupata visa vya Ulaya na Marekani. Kuna manufa mengi tu ila tu wengi wenye mitazamo finyu wanaona upande mmoja wa sarafu bila kuigeuza kuangalia taswira ya sarafu hiyo upande wa pili.
 
EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,479
2,000
Kifungu husika kinasema kuwa "Bila kuathiri masharti yalipo kwenye Sura hii, mtu yoyoye mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi."

Hiki kifungu kimepachikwa tuu na hakitoi hadhi yoyote kwa sababu kinasema wazi kuwa hadhi hiyo itaainishwa katika sheria za nchi.

Pia kitu cha kushangaza ni kuwa hata kama sheria hizo za nchi zitakuja kutambua uraia wa nchi mbili, itakuwa na maana kuwa mtu mwenye uraia wa Marekani, kwa mfano, atatambuliwa kama raia wa Tanzania atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano tuu.

Kwa maana hiyo, huyo mtu hatatambuliwa kama raia wa Tanzania kama atakukuwa katika nchi nyingine kama Kenya na Uganda. Huyo raia hata-enjoy benefits za East African Community kama Watanzania wengine kama akiwa katika nchi wanachama.
 
Asante kwa ufafanuzi zaidi wa ibara hiyo ya rasimu ya katiba EMT.

Jopo la tume ya katiba ni watu wenye upeo wa sheria, uzoefu wa masuala ya kimataifa na wametumikia nchi hii kwa miaka mingi, busara kubwa waliyo nayo ndiyo imefanya waingize mwanya huo.

Ninachoweza kuona wasingeweza kuweka moja kwa moja kwamba raia wa aina hiyo watambuliwe ni kwa sababu jambo hili linatakiwa kufanyiwa kazi pamoja na kwamba huwa sheria za uhamiaji hubadilikabadilika kuendana na mazingira hali kadhalika wakati. Hivo basi kuna namna mbalimbali ya kuwatambua kadiri sheria za uhamiaji zitakavyorekebishwa.

Jambo la msingi walao hili limetambuliwa ndani ya rasimu ya sasa ya Katiba, kama litapitishwa kwa kura za wananchi hali kadhalika bunge la katiba basi italeta nafueni kwa watanzania wenzetu walioko nje ya nchi na kuwapa mwanya waje kujumuika nasi kuijenga nchi.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,153
1,250
Zamani nipokuwa sijabahatika kutembea nchi za nje na kuishi huko nilifikiri na kuwaza kwa mtazamo wako huo, lakini nilipobahatika kufika huko pamoja na kutobadili uraia wa nchi yangu, nimepata kuelewa hali yalisi ya nchi ambako mtu hawana njia ye yote ya kupata ajira na ili aweze kufanikiwa analazimika kuwa na vibali vya kazi ambavyo havitolewi bure ila kwa taratibu za uhamiaji ambazo kuna ndoana zinazowafanya wengi walazimike kunasa ili kuendesha maisha.

Kwa bahati nzuri wengi nilioonana nao na kujadiliana kutoka nchi kadhaa hasa za bara la Ulaya na Marekani wanalilia kwao na kwamba kinachowaweka huko ni kupata cho chote cha kuja kusimamisha vema maisha na familia zao. Kama kuna wanaoona huko ni peponi ni wa kizazi cha Lulu ambao wamefika huko wakati bado bongoni mwao hawajakomaa kupima kwenye mizani mbivu na mbichi.

Mpaka sasa nina ushahidi wa wengi wao kile wanachokipata ni kuja kuwekeza kidogo kidogo home kwa vile mfano pesa nchi za huko mabenki hayana riba nzuri, mfano Marekani interest utapata 0.025% kwa mwaka, na hiyo huishia kwao kwa visingizio mbalimbali wakati bongoland unaanzia na 3% and up. Utaona wengi wao wanaamua kuja kuweka pesa zao kwenye mabanki ya huku nyumbani.

Uwekezaji nao upo kwa sana, kuna wengi wanaoingiza bidhaa toka huko kwao kwa vile wengi wetu huwa vigumu kupata visa vya Ulaya na Marekani. Kuna manufa mengi tu ila tu wengi wenye mitazamo finyu wanaona upande mmoja wa sarafu bila kuigeuza kuangalia taswira ya sarafu hiyo upande wa pili.

Ni mawazo tu yako hayo na hao uliowahoji na suala hapa sio nani katembea wapi na wapi labda kama inabidi kuleta pasi ili kushindania nani msafiri zaid!!!!!!

Hivi kwa akili yako unadhani inahitaji mtu kwenda ulaya magharibi na marekani ya kaskazini kujua kuwa uraia wa nchi mbili ni siasa zaid kuliko uchumi na uhalisia????!!!!

Hebu nitajie Raia walioukana Utanzania na wapo nje wana mitaji ya kusukuma nchi hii lakini wamekwama kwa kigezo cha uraia!!!!

Ukiweka na aina ya biashara wanazotaka kuja kufanya utaelimisha wengi pia!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi

Jibu hoja nizoainisha kujenga utetezi si mipasho. Rudia kusoma tena uone nini nimekiongelea katika hoja zangu na ujaribu kujenga utetezi kwa hoja zangu kwamba hao hawaji kuwekeza home, kwamba yaliyowasibu kupoteza uraia wao ni kuhalalisha haki katika nchi vinginevyo wangeishi isivyo halali na kuacha uraia wa nchi nyingine si dhambi. Kwamba wanawekeza hapa homeland na hivyo kusaidia ajira kwa vijana. Hizo ndizo hoja nilizoainisha unatakiwa ulete zako kuzipiku zangu.

nimepata kuelewa hali yalisi ya nchi ambako mtu hawana njia ye yote ya kupata ajira na ili aweze kufanikiwa analazimika kuwa na vibali vya kazi ambavyo havitolewi bure ila kwa taratibu za uhamiaji ambazo kuna ndoana zinazowafanya wengi walazimike kunasa ili kuendesha maisha.

Kwa bahati nzuri wengi nilioonana nao na kujadiliana kutoka nchi kadhaa hasa za bara la Ulaya na Marekani wanalilia kwao na kwamba kinachowaweka huko ni kupata cho chote cha kuja kusimamisha vema maisha na familia zao. Kama kuna wanaoona huko ni peponi ni wa kizazi cha Lulu ambao wamefika huko wakati bado bongoni mwao hawajakomaa kupima kwenye mizani mbivu na mbichi.

Mpaka sasa nina ushahidi wa wengi wao kile wanachokipata ni kuja kuwekeza kidogo kidogo home kwa vile mfano pesa nchi za huko mabenki hayana riba nzuri, mfano Marekani interest utapata 0.025% kwa mwaka, na hiyo huishia kwao kwa visingizio mbalimbali wakati bongoland unaanzia na 3% and up. Utaona wengi wao wanaamua kuja kuweka pesa zao kwenye mabanki ya huku nyumbani.

Uwekezaji nao upo kwa sana, kuna wengi wanaoingiza bidhaa toka huko kwao kwa vile wengi wetu huwa vigumu kupata visa vya Ulaya na Marekani. Kuna manufa mengi tu ila tu wengi wenye mitazamo finyu wanaona upande mmoja wa sarafu bila kuigeuza kuangalia taswira ya sarafu hiyo upande wa pili.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,153
1,250
Jibu hoja nizoainisha kujenga utetezi si mipasho. Rudia kusoma tena uone nini nimekiongelea katika hoja zangu na ujaribu kujenga utetezi kwa hoja zangu kwamba hao hawaji kuwekeza home, kwamba yaliyowasibu kupoteza uraia wao ni kuhalalisha haki katika nchi vinginevyo wangeishi isivyo halali na kuacha uraia wa nchi nyingine si dhambi. Kwamba wanawekeza hapa homeland na hivyo kusaidia ajira kwa vijana. Hizo ndizo hoja nilizoainisha unatakiwa ulete zako kuzipiku zangu.

Mbona swali rahisi tu mkuu wewe umeongea na wengi huko na umesema una ushahidi!!!!

Wanataka kuja kufanya biashara za aina na ukubwa upi kama watapata nafasi ya kupewa uraia huo???!!!!!!

Walikupa business plan yoyote au yalikuwa ni maongezi ya kumkarimu mgeni???!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom