Ni nadharia ya kinyanyapaa ya mfumo dume wa Kimarekani, ambayo Kiranga kaidaka nzima nzima, inayosema wanawake wa kizungu wenye nywele za kijivu hawana kitu vichwani. Ni warembo hapana shaka, na mara nyingine hutumia kuvutia kwao kupata fursa anuwai. Mfumo dume uliosheheni ufinyu wa umudu wa sayansi. Hakuna binadamu ambae akili yake inaendana na maumbile yake ya nje. Huwezi kuagua na kutabiri kwamba mtu wa kijani au mwenye nywele ndefu atakuwa mpumbavu.
Kiranga anasema ni makarani wa kizungu wenye nywele za kijivu, yani kiasili wajinga, ndio walimpokea Mtanzania ambae ombi lake la kazi halikustahili hata kufikiriwa kufanya kazi Federal Resereve, sio raia wao.
Kwa maneno mengine, haikuwa kosa kusaili hadithi yake, ilikuwakuwaje waajiri wa Federal Reserve wafike hatua ya kupendezwa na wasifu na kumsikiliza akiwambeleza kwamba ana makazi ya kudumu wamfikirie? Kituko.
Ukishasema wewe sio raia wao, makaratasi yako yanatupwa kapuni, hawana muda kusoma wasifu, wana maombi lukuki ya raia. Ukijaza maombi Kwenye tarakishi ndio mbaya zaidi, ukishabonyeza kiboksi cha "sio raia" tovuti haliendelei mbele linakutupa nje.
Ukitumia mifano ya shida zilizowakuta ng'ambo kwa kutokuwa raia usilete tamthilia za kubuni.