Upotoshaji Wikipedia Juu ya Nyerere?

Waislam wa ccm ambao wengi wanampenda JK wanachuki sana na mwalimu Nyerere.Hata JK nadhani hampendi kabisa mwalimu.Hizi zitakuwa jitihada za watu wake.BTW wamekosea kusema walinyimwa "neccessaries" badala yake ilitakiwa kuwa "neccessities"
 
Kilasara,
Juhudi bado zinaendelea. Ni mchakato wa muda mrefu. Wikipedia hawana lolote juu ya hizi juhudi. Nadhani kwa sasa wamekaribia kumtangaza "mwenye heri" na itachukua miaka na miongo kabla ya kufikia hatua ya "mtakatifu."
 
mkuu umebadilika sana siku hizi!Big ups fo real!nauchukia mfumo wetu kuliko maneno.Mimi ni mshabiki wa siasa za mwalimu.Lakini haya aliyotuachia sometime kuyafikiria yanaumiza sana.Uongozi na mfumo wake umekaa kama genge na mtandao wa maovu,ukandamizaji na kila aina ya utapeli na unyanyasaji.Kila pahala ni tumbili wamejaa,hakuna wa kumsaidia binadamu.Nina ghadhabu na hawa watu basi tu...
 
Mbona vitabu vya Historia viko wazi tu na kutuonyesha kuwa Watanzania hatukuwa na matatizo yoyote ya kiubaguzi wa Kikabila wala mwengine wowote ule kabla hata Nyerere hajazaliwa! bali Nyerere historia yake mwenyewe inalishuhudia hili; yeye akiwa Mzanaki mbara kutoka kijijini alipokelewa vizuri kabisa na watu wa pwani (na nina hakika kuna Wapwani walioenda bara kabla ya wakati wa Nyerere na kupokelewa vizuri tu na kujihisi kuwa wapo makwao) hii yote inakuonyesha kuwa Nyerere tayari aliukuta utamaduni wa Mtanzania ukiwa hauna ubaguzi Waliomtengeneza na kumfikisha Nyerere pale hawamuoni kama hivyo unavyomuona wewe, Roland Brown former Attonery General anamuelezea Joan kuwa ni "kioo cha akili ya Nyerere" kwa maana nyingine ndiye aliyekuwa akii reshape mind ya Nyerere, anaendelea Roland: (Joan alikuwa ni kioo cha Nyerere ) katika ku dili na waandishi wa habari huku akiwa na uwezo wa hali ya juu katika kumuandikia vitu Nyerere na kuonekana kama Nyerere mwenyewe, alimchorea Nyerere barua nyingi za kwenda kwa viongozi wa Nchi mbalimbali kadhalika kuandika hotuba nyingi za Nyerere.......huyo ndiye Nyerere.
 
Sideeq,
Nilijua tu utasema hivyo. Hata Kenya kabla ya uhuru makabila yote yaliishi kwa amani. Lakini ukabila ulikuwepo. Mwingereza alifaidika nao kwa sababu alitumia mfumo wa divide and rule. Nitakupa kahistoria kadogo tu kule kwetu. Mwalimu wangu wa primary, alisoma Tabora. Huko alikutana na msichana wa Kinyamwezi na akampenda. Sasa kasheshe ilikuja pale alipokuwa anamleta nyumbani kumjulisha kwa wazazi wake. Nakumbuka mama yake alikimbilia nyumbani kwetu, (baba yangu alikuwa pasta, au mchungaji) kulalamika, eti huyu mwanawetu wa kiume, anatuletea msichana anayekunya mwezini. Tutaishije, tutaelewanaje? Atanileaje? Ilibidi baba atumie busara za ziada za uongozi wa dini, na pia kumkumbushia kwamba chini ya TANU sisi ni wamoja, kwa yule bibi kuja kumkubali mchumba wa mwalimu wangu. Huu ni mfano mmoja tu. Pale kwetu Musoma, tuna makabila zaidi ya 27 na mengine tulikuwa hatuingiliani kabisa na kudharauliana. Lakini ni TANU iliyotuunganisha pamoja. Kama wewe umekulia mitaa ya Kariakoo hili litakuwa jambo gumu kwako kulielewa, lakini kwetu ambako tulikuwa tumechanganyika makabila chungu nzima ni TANU ndiyo iliyotufundisha kuwa sisi ni Watanganyika. Hilo halina ubishi. Na kuhusu uhusiano wa Wicken na Nyerere nitakupa kisa kingine kidogo tu. Alipokuja Marekani 1977 kwenye state visit yake ya pili, Wicken alikuwa amemuaminisha kuwa atakutana na hostile crowd kwa sababu ya siasa zake za ujamaa. Mimi kwa bahati nzuri nilichaguliwa kazini kwangu kufuatana na msafara wa Mwalimu katika ziara hiyo. Alianzia chuo kikuu cha Howard. Pale ukumbi mzima ulikuwa umejaa. Hotuba yake iliingiliwa na makofi na vigelegele, ndugu zangu Wamarekani weusi wakimwambia "we love you brother." Haya, tumetoka hapo tumekwenda San Francisco, ambako nako alikuta City Hall imejaa, na watu wengine wamesimama pembezoni mwa ukumbi. Mimi nilikuwa nyuma ya pazia nikitayarisha mitambo ya kurekodi. Nimemwangalia Mwalimu walipofungua pazia, akaona ukumbi wa watu, mbona alishtuka. Mpaka meya wa jiji la San Francisco akasema hajawahi kujaza ukumbi huo na anafurahi kwamba Mwalimu hagombei nafasi yoyote ya kisiasa katika mji wake. Na la mwisho, Wicken alikuwa amemwambia kuwa wine za Kimarekani ni cheap quality. Mimi ndiye niliyemshauri Mwalimu ajaribu chardonnay ya Kimarekani nilipokuwa hotelini kwake. Aliipenda, na tangu wakati huo kila mara tukikutana NY tulikuwa tunafungua chardonnay moja ya Kimarekani. Ni kweli Wicken alikuwa mshauri wake lakini in the last analysis Nyerere had his own mind. Kuandikiwa hotuba si hoja, lakini mwangalie Nyerere kwenye press conferences uone kama ni mtu aliyekuwa anategemea kuambiwa au kuandikiwa. Acha bwana!
 
Wikipedia has never been a reliable source of reference. Any student who quotes Wikipedia is doomed. At most you should use Wikipedia to search for more materials in the reference list or in any other reliable source.



May be for social sciences references,but for Natural sciences is one of the reliable sources of Information.So don't generalize.
 
Waislam wa ccm ambao wengi wanampenda JK wanachuki sana na mwalimu Nyerere.Hata JK nadhani hampendi kabisa mwalimu.Hizi zitakuwa jitihada za watu wake.BTW wamekosea kusema walinyimwa "neccessaries" badala yake ilitakiwa kuwa "neccessities"
Mkuu wangu kwa nini mnapenda sana kupigia debe Udini na uendelea kuwaandama waislaam?. Hivi unajua ya kwamba inachosha kusikia kila kkitu waislaam ndio wenye chuki na Nyerere wakati kuna kina Mtei, Kambona, Pope na wakristu kibao hawakumpenda baada ya Utaifishaji..

Swala la kujiuliza ni kama ukweli ktk bandiko hilo. Ikiwa hukubaliani nalo ukweli unaojua wewe ni upi na unapingana na hoja za watu kwa sababu unafahamu kilichotokea. Acheni hizi habari za waislaam hivi ama wakristu hivi maana mnachochea moto kuukoleza udini.
 
To the contrary, the South African Boers respect and admired Nyerere's brilliance although he was against them. They used to call him an "An Evil Genius".
Nyerere had given refuge to the many black nationalist leaders who fled South Africa under apartheid. They were allowed to set up training camps inside Tanzania. kmv are you serious? kvm when was those pigs respect and admired nyerere. they didnot respect mandela or sobukwe. know your African history before you write any bullshit.
 
mkuu naizungumzia ccm.Ukweli ni ukweli tu mkuu,sisi watanzania ni wanafiki tusioupenda ukweli.JK ndo kinara wa udini,na member humu wadini wanaojinasibisha na ccm pamoja na uislam ndo wanaomtukana Nyerere kila uchao.The truth shall remain what it is...Kumbuka nawazungumzia ccm hapa.
 
armanisankara,
Let me come to the defense of KMV.
It is true the boers "respected" Nyerere's brilliance as they respected Mandelas. Ian Smith called him an 'evil genius," because although they acknowledged his geniusness they did not agree with it because it was against their interests.
It is like fighting in a war and you see the general on the other side using clever tactics against you. You admire the tactics but do not like the general. It was the same with Mwalimu. And by the way even in jail Mandela's jailor used to call him "sir."
 
Ukisoma kitabu kiitwacho "The Dark side of Mwalimu Nyerere", utakubali kuwa hakuna lililokosewa hapo!
 
Unaposema JK ni kinara wa Udini nakuomba nambie kauli hata moja aliyowahi kutoa yenye UDINI ama maamuzi ya sheria ama tendo lolote linaloashiria Udini wake..Haijalishi kuwa CCM au chama chochote maana Udini ni wa mtu na sheria sio wa chama.
 
Waacheni wikipedia waandike nyie watanzania mko poor kwenye documentation.Mtoto aliyezaliwa karne hii hajakuta taarifa yeyote kuhusiana na historia ya watanganyika/tanzania.Matokeo yake watu mnatoka mapovu tu huku document za kukanusha hamna!Haya wikipedia wamesema hivyo na wameweka references wekeni na nyie references zenu kuwapinga siyo kupayuka tu.

Lakini All in All tukubali tukatae serikali zilizokuwa/ zinaongozwa na mfumo wa kijamaa (Socialism)lazima kuwepo na ukandamizaji wa haki fulani kwa wananchi hasa wale wanaoonyesha kuipinga/kuichallenge.
 
Unaposema JK ni kinara wa Udini nakuomba nambie kauli hata moja aliyowahi kutoa yenye UDINI ama maamuzi ya sheria ama tendo lolote linaloashiria Udini wake..Haijalishi kuwa CCM au chama chochote maana Udini ni wa mtu na sheria sio wa chama.
Mkuu wanasiasa tangu lini wakawa wepesi kusomeka?Wana ccm wanaosema kuwa kuna mfumo kristo ndo hao hao pro JK na anti mwalimu.

Ukiambiwa serikali imeshiriki kumtesa Ulimboka utauliza ni wapi JK alituma watu?Utauliza kauli aliyoitoa ya kuwatuma wanausalama kwenda kumtesa Ulimboka?
 
Kama wewe ni honest basi utakubaliana na mimi kuwa si Nyerere aliyefuta ubaguzi Tanganyika/Tanzania kwa sababu hiyo TANU iliyokuondolea wewe ubaguzi haikuasisiwa na Nyerere! Mimi, chardonnay, NY, nilipokuwa hotelini kwake, ndiye niliyemshauri kuwa wine ni cheap.......
 
Watu wanaosema kuna mfumo kristu hawakemei Ukristu kama imani ya dini isipokuwa mfumo wa utawala wake ambao kuna kundi la watu ndio waamuzi wa Taifa linakoelekea. Mara nyingi watu wana quote Vatican inavyo control tawala kwa kutumia imani za dini ktk mahusiano yake ndani na nchi nyinginezo. Ndio maana kuna nchi inaitwa Vatican City lakini nchi hiyo iko controlled na Kanisa. Hakuna utawala kama huu duniani isipokuwa nchi hiyo tu pengine kidogo Iran inafuata kutokana na wale Ayatollah 12 lakini hawana control na tawala nje ya mipaka yao. Ni mfumo pekee ambao hauna mfano mahala popote na maana neno hili limetumika na sii kulaani ama chuki na Ukristu. Kuna habari zisemazo kuwa haiwezekani rais kutoka bara akatokea dhehebu jingine nje ya Catholic church.

Unaposema nikiambiwa SERIKALI ilimtesa sina uhakika unaposema tena JK alituma wapi watu wake. Binafsi yangu siamni kwamba JK tuma watu kumtesa Ulimboka maana navyoamini mimi Ulimboka mwenyewe alikuwa nyoka, yaani alikuwa mtu wa usalama kwa hiyo siwezi kusema kwa uhakika kilitokea kitu gani. Sina ushahidi wowote zaidi ya kuamini hivyo..Na kuhusu Udini bado hujanijibu JK aliwahi kusema wapi ama kutoa amri gani kueneza Udini nchini maana nijuavyo kila ombi la waislaam ni yeye alolipiga chini tena akiwaambia wazi hayuko nao.
 
ukweli unauma.....

Nyelele arikuwa mtu mzuli sana, wakati wa Nyelele aliimalisha sana hari ya watu wake kierimu na rishe bola, vyakura kama mahalage

mchere, sukali, virikuwa vikipatikana kira kona ya Jamhuli ya Tanzania

Dah..! unasoma darasa la ngapi Mkuu?
 
Swali unaloniuliza nimeshalijibu,na nitakujibu tena kwa namna nyingine.Yeye ndo kiongozi mkuu wa nchi na udini ndo umepamba moto under his watch.Na kwasababu ya dini yake,kukaa kimya huku watu wake wakitoa maneno makali ya kidini na yeye tayari anakuwa mdini.Actions speaks louder than words and "birds of the same feathers flocks together".

Hata kampeni yake iliyopita walitumia udini usibishe hilo.

Halafu kwa kumalizia,hayo ya kusema mfumo kristo ndo udini wenyewe huo.Tanzania inaripoti vatican?umetoa wapi hizi taarifa mkuu?
 
Halafu kwa kumalizia,hayo ya kusema mfumo kristo ndo udini wenyewe huo.Tanzania inaripoti vatican?umetoa wapi hizi taarifa mkuu?
Rekodi zinamuonyesha Nyerere akiripoti Vatican.
 
Alaa sasa imekuwa kosa la JK kwa Udini unaotapakaa? sii kawapeni uhuru wa habari kwani sisi wajinga kiasi gani iwe ni kazi ya rais hata kuchambua mazungumza ya watu...JK katupa Freedom of speech, leo imekuwa kosa lake mnataka mtu kama Mkapa aliyewazuia watu kusema. Aliyeingia hadi misikitini kuua watu kwa sababu walikuwa wanapingana naye, aliyewaita watu wana wivu wa kike kwa sababu ya Ufisadi wake.. Ingekuwa nchi nyingine lile neno wivu wa kike tu wanawake wangemwandama hadi akavuliwa Urais lakini sii tanzania yetu. JK ana makosa yake lakini sii la Udini sisi wenyewe wadini.

Udini tunao sisi mkuu wangu na tumeuanzisha kwa hizi fikra za kutoaminiana, unafiki na hali mbaya ya maisha kiasi kwamba tumebakiza tumaini la wokovu wa Mungu. Watu wengi Tanzania wamemrudia Mungu kwa sababu ya shida zimezidi na hivyo uetetezi wa dini umekuwa kama ngao yao. Dini ni ya Mungu haitaki mtetezi wala mlinzi yeyote maana Mungu mwenyewe ndiye mlinzi na mtetezi mkuu...Watu wengi wanataka sana kuifanya kazi ya Mungu na hapo ndipo naposema Udini tunao sisi wala sio JK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…