Upotoshaji wa historia ya Mgombea wakati wa Uchaguzi na mbinu za kuepuka kupotoshwa

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
41
1710734696873.png

Wakati wa uchaguzi, baadhi ya watu hutengeneza taarifa za uongo au kuficha ukweli kuhusu historia ya mgombea fulani ili kuathiri taswira yake kwa umma. Taarifa hizo zinaweza kuwa mwaka wa kuzaliwa, historia ya uraia wake, au elimu yake.

Mathalani, mtu au kundi la watu linaweza kusambaza taarifa za uwongo kuhusu umri wa mgombea kuonesha kama ni mdogo au mkongwe zaidi kuliko uhalisia, ikitegemea jinsi umri unavyoweza kuathiri jinsi watu wanavyomwona mgombea.

Vilevile, historia ya uraia au elimu ya mgombea inaweza kupotoshwa ili kujenga mazingira ya kumsafisha au kumharibia katika uchaguzi husika. Mfano, kwenye uchaguzi wa Marekani mwaka 2018 historia ya Barack Obama ilipotoshwa kwa watu kumzushia kuwa asili ya Obama ni Kenya taarifa ambazo baadaye zilichunguzwa na kubainika hazina ukweli.

Mbinu za kubaini Upotoshaji huu
1. Angalia Tafuta taarifa za Mgombea katika nyaraka au vyanzo vya zamani (Makavazi)

Tafuta taarifa za mgombea zilizopo mtandaoni tangu zamani au nyaraka zake halisi zisizo za mtandaoni kama vile vyeti vyake vya kuzaliwa au rekodi za shule au chuo alichosoma.

2. Muulize muhusika
Tafuta taarifa rasmi kwa kumhoji mgombea aliyehusishwa na historia Fulani ili kupata ufafanuzi kutokea kwake mwenyewe. Kuuliza taarifa hizi kwa muhusika kunaweza kukusaidia kupata taarifa na nyaraka rasmi zinazothibitisha historia ya mgombea.

3. Wasilisha taarifa hiyo katika majukwaa ya uhakiki
Majukwaa ya uhakiki kama JamiiCheck.com yana watalaamu ambao wanaweza kukusaidia kupata taarifa zaidi kuhusu Mgombea Fulani. Hivyo ukiona unakwama kupata uhalisia ni vyema ukawasilisha taarifa hiyo usaidiwe kufanya uhakiki.
 
Back
Top Bottom