Upinzani watangaza mapambano 2008

Ukweli ni kwamba upinzani hawana nyimbo kabisaaa wala game plan ya maana.

Halafu Mwanakijiji unaumwa au? Naona umebonyeza thanks mfululizo humu, sasa sijui kibao cha mall kimekufanya trigger happy?

wapinzani wana nyimbo ila watu kama Nzoka hamuwezi nyimbo za kizazi kipiya kisichopenda ufisadi ....... lol ...... kwi kwi kwi ... ole wako uanze kucheza wimbo wa mapepe kwenye radio yetu ya jamii huko ......
 
Shy
Wapinzani hawajawahi kuhaadaa watanzania, bali kwa sasa wanafanya kazi yao kama inavyotakiwa. JMK mwenyewe aliwahi kukili kwamba mara nyingi sana serikali yake imekalia kaa la moto. Ilimlazimu kubadilisha hata baraza la mawaziri zaidi ya mara moja. Sababu ya wapinzani.
Come on wapinzani kazeni kamba. Si muda mrefu CCM watakuwa wapinzani pia.
 
Duh, Wakuu hivi kweli huyu SHY mzima kweli?...naomba maelezo zaidi maanake nimeshtuka sana niliposoma maelezo yake hasa kipande hiki:-

Sitaki kubisha inaonekana wapinzani wamewashika sana vijana wa kitanzania walio nchi za nje haswa marekani kiasi kwamba zitto anapokanyaga huko wanaona mwokozi wao kafika watu wanasongamana wanataka kumwona kupiga nae picha na vitu kama hivyo .
Pamoja na kuacha hizo namba za simu na watanzania kujitokeza kuonana nae , sera na mambo anayoongea katika mikutano hii ni zile zile , za ufisadi ambazo sasa hivi ni zilipendwa , yale yale ya epa na mambo mengine ambayo kwa hakika sio ya kujenga upinzani sio ya kujenga nchi ni ya kupasua hadhi ya nchi na watu wake nje ya mipaka yake.

Yaani kweli kuna watu kama SHY ambao wana shy away from real problem kutafuta mchawi?.. Mkuu umenisikitisha sana kwa sababu bila upinzani haya maswala ungeyajua wapi?.. ama ulikuwa hufuatilii mifungo ya Lowassa aliposema ndege yetu inapaa! kina Kingunge na Kikwete mwenyewe akisema kelele za mlangoni haziwezi kumzuia kulala leo yupo wima usiku kucha akijaribu kupangua baraza lake la mawaziri ambalo haliwezi jengeka kwa sababu msingi tayari ni mbovu.
Tazama mabadiliko makubwa ndani ya Sekretarieti ya CCM, hiyo NEC, Mabalozi na mikataba yote haya wewe wayaona ni mambo yaliyopitwa na wakati ama kweli mwenztu bado umejigubika blanketi zito la Kijani/Njano..
 
Nadhani lilikuwa wazo zuri kwa Zitto kuwemo kwenye hiyo kamati. Hii ilikuwa ni kamati ya kitaalamu na wala siyo ya kisanii kwa hiyo kuwa na watu kutoka pande mbalimbali lilikuwa wazo zuri. Alinichekesha Mzee Bomani kwamba aliulizwa na watu mbalimbali kuwa na "wewe mzee umekubalije kuingia kwenye hii tume ya wasanii?" Yaani hata kabla ya kazi kumalizika kuna watu walishaiona hiyo tume kuwa ni gelesha tu. Lakini nadhani wamefanya kazi nzuri. Ngoja tusubiri tuione ripoti yenyewe, na kama wasemavyo Wamarekani the proof will be in the pudding.

Kamati hii ni mbwa mwenye meno ama ni mbwa kibogoyo?

Usisahau kuwa pia hatuangalii majina hapa ni matokeo, walichofanya pamoja na kitakachofanyika!!
Kwamba Bomani ama Zitto walikuwemo haina tofauti na kama ile ambayo Warioba na wengineo waliyokuwemo!
 
ya kaisari mpeni kaisari na ya SHY muachieni SHY...
Mi nilijua Kikwete atawatega!
We subiri uone!
Muungwana si tu kuwa ni msanii bali pia ni mwanasiasa mzoefu na KAMWE TUSIMU UNDERESTIMATE!
Huyu jamaa anaweza kuwa smart more than we give him credit for or even more than many of us can acknowledge!
 
Niliwahi kuona tangazo katika mtandao wakati Fulani , mmoja wa wabunge wa upinzani Tanzania ameacha namba yake ya simu atakayotumia atakapofika marekani , kwa wale ambao hawako busy wanapenda kuonana nae na vijana wengine wengi wenye muelekeo wa kipinzani .

Tafadhali tuoneshe tangazo hilo na uliliona wapi, "mtandao fulani" usije kuwa ni wa kufikirika. Tuoneshe ilo tangazo na hasa hapo liliposema kuwa "kwa wale ambao hawako busy wanapenda kuonana nae na vijana wengine wengi wenye muelekeo wa kipinzani". Utajijengea heshima kweli kama utamtaja Mbunge huyo na wapi uliona Tangazo hilo lenye maudhui hayo. Binafsi sijaliona na hivyo siwezi kusema kama lipo au halipo. Kama kuna mtu mwingine ameliona tunaomba atusaidie.

Sitaki kubisha inaonekana wapinzani wamewashika sana vijana wa kitanzania walio nchi za nje haswa marekani

Kuonekana kwa kitu kwenye fikra za mtu hakuwezi kuzuilika; kwa mfano inaonekana mafisadi wamewashika watu wengi wa Arusha na Bariadi kiasi kwamba na akili zao timamu wanakurupuka kuwapokea kwa shangwe watu walijiuzulu kwa kashfa!

kiasi kwamba zitto anapokanyaga huko wanaona mwokozi wao kafika watu wanasongamana wanataka kumwona kupiga nae picha na vitu kama hivyo .

Ni lini tena Zitto amewahi kukanyaga huku? Cha kushangaza umeshindwa kusema kuhusu maelfu ya watanzania waliokusanyika Jangwani kumsikiliza na wale waliojitokeza katika sehemu mbalimbali za mikoa ya Tanzania. Iweje Zitto kupokewa kama "Mwokozi" Tanzania na Watanzania wenzake ni jambo la kufurahia lakini akipokewa kiukimya Tanzania imekuwa nongwa?

Kwa kukupa taarifa tu, ni mimi niliyempokea uwanja wa ndege na hakukuwa na vimulimuli, saluti, pikipiki, na ngoma za sindimba kama alivyopokewa mzee wa Vijisenti ambaye anaonekana ni mwokozi kule Bariadi! au alivyopokewa yule mwenye ndege iliyopaa huku abiria wameachwa wameduwaa!!

Zitto hakupokewa kwa mbwembwe wala shangwe! Alipokewa kwa heshima ya kiongozi ambaye ameonesha uungwana wa kuja kututembelea hapa kwa gharama zake mwenyewe! Sisi tulitumia kidogo tu kwa chakula na zawadi za jiji la Magari!

Pamoja na kuacha hizo namba za simu na watanzania kujitokeza kuonana nae , sera na mambo anayoongea katika mikutano hii ni zile zile

Mambo mengine ni ya kufikirika, Kwanini mtu abadilishe sera anazozungumzia wakati tatizo bado ni lile lile? Hii inaelezea ni kwa sababu gani watawala wetu wameacha mambo ya msingi na sasa hawana cha kushikilia na badala yake hawachoki kuja na mipango mipya huku ya zamani ikiwa imekufa. Mara MKUTAKUTA, mara MFISADIKA, mara UKURUTU, n.k.. matatizo ya watanzania yako pale pale.

za ufisadi ambazo sasa hivi ni zilipendwa , yale yale ya epa na mambo mengine ambayo kwa hakika sio ya kujenga upinzani sio ya kujenga nchi ni ya kupasua hadhi ya nchi na watu wake nje ya mipaka yake .

Hii ni kejeli kwa Watanzania; yaani wewe ufisadi ni suala ambalo mtu alifumbie mdomo? yaani masuala ya EPA kwako ni masuala ya yaliyopitwa na wakati? Leo hii serikali haijui nani mmiliki wa Tangold, wewe unasema imepitwa na wakati? Leo hii haijulikani fedha zinazolipwa Dowans zinakwenda wapi wewe unasema zimepitwa na wakati? leo hii fedha zinaingia upande huu na kutokea upande ule wewe unasema kuzungumzia ni "imepitwa na wakati". Tupe pendekezo basi tuzungumzie mambo ya wakati kama siyo haya yaliyosimika mkuki wa ufisadi nje ya nyumba zetu na kuingia ndani na kuchukua mali na hazina ya watu wa Taifa hili? Wewe unasema yamepitwa na wakati!?

Namheshimu Nyepesi na Wenzake wengi kama watanzania lakini siwezi kuheshimu na kuendelea kusikiliza watu wenye mawazo ya kuvuruga wananchi wakiwa nje ya mipaka yao huwa nashangaa kama hawana masuala mengine ya kuongea zaidi ya haya .

Sijui "Nyepesi" ni nani, lakini inasikitikisha kuwa umeingia kwenye mtego wa kina Lowassa kuwa Wazalendo wa kweli na pekee ni wale walioko nyumbani; kwamba sisi tulioko nje ya nchi ni Watanzania nusu ambao hatutakiwi kutolea maoni. Kwa mawazo yako ni kuwa Mtanzania akishatoka nje ya mipaka basi utanzania wake umepungua kidogo na kwa kadiri anavyoenda mbali na ardhi ya Tanzania ndivyo ambavyo anatakiwa kukaa kimya!

Watu wana mambo mengi ya kuzungumzia ndani na nje ya nchi yao na si wewe na wala si mtu yeyote anayeweza kuamua vinginevyo. Kama ungechukua muda kidogo kusoma Katiba yetu ungeona kuwa haitoi mipaka ya maoni kuwa "mtanzania atakuwa na uhuru wa maoni akiwa Sumve, lakini akienda Mombasa maoni yake yatakoma!". Katika Katiba hiyo hakuna mahalia ambapo panasema "Mtanzania atazungumzia jambo hili akiwa Magomeni lakini akiwa London itakuwa mwiko". Ungeliewa hili ndugu yangu ungefurahia mchango wa mawazo ya watanzania wawapo nyumbani, wavukapo mipaka ya nchi yao na hata wale ambao wanaishi ugenini miaka nenda rudi. Usiwabague Watanzania kwa sababu ya ukazi wao kwa kujifanya wewe ni bora kuliko.

Pamoja na maneno yako hayo, hatutawaachia nchi mafisadi, na hatutapiga magoti mbele ya wabakaji wa nchi yetu na wezi wa mali za taifa letu. Hatutawaimbia nyimbo za shangwe waliondamwa na kashfa na wale watubezao hatuwasusia nchi!

Hao ni chadema ndio wameshikilia Epa , Ufisadi na Usalama wa Taifa ,

Wakati mwingine mtu anaandika hata ajuia anaandika nini? Hivi unataka kutuambia EPA, ufisadi na Usalama wa Taifa mbovu kabisa ndio Chadema? na CCM wamefanya nini? Ndio watetezi wa Taifa hili? Give me a break!

ukirudi kwa upande wa baba zako chama cha wananchi CUF , ningekuwa mimi ni mwanachama wa CUF ningehoji kwanini hao viongozi wawili wa CUF wako pale walipo mpaka sasa hivi

sasa kama ni si mwanachama wa CUF kwanini uhoji mambo ya CUF; Badala yake ungeuliza huko CCM (kama wewe ni mwanachama) imekuwaje Makamba na Kingunge wanasimamia muafaka? Wana ujuzi gani wa utatuzi wa migogoro? Wangempa Januari nafasi hiyo kwani angalau yeye kasomea mambo hayo!!

Tangia upinzani umeanzishwa ni viongozi wale wale wa CUF wanaowashika masikio baadhi ya wanachama wao , ni viongozi wale wale wakorofi wako madarakani katika chama hicho mpaka sasa hivi , sijui CUF hawana viongozi wengine ni lazima wawe hawa hwaw ?

Unatania! Viongozi wale wale? Hivi unataka tuanze kuhoji ni chama gani kina viongozi wale wale katika nafasi zake nyingi Tanzania? Kama hujui naomba uulize tu na nitakufa na furaha kuanza kukuorodheshea viongozi wakongwe katika chama fulani na serikali yake hadi sasa watoto na watoto wa watoto wao nao wameanza kurithi vyao! Kama ni sahihi kwa chama hicho iweje liwe kosa kwenye vyama vingine?

Mtihani wao wa kwanza wameshaushindwa wa kuleta maelewano huko visiwani , kwa sababu wameshashindwa jaribio hilo , sioni sababu ya kwanini wasiache nafasi hizo wazi waje watu wengine wenye utashi zaidi yao , watu wanaopenda kukaa mezani na kumaliza tofauti zao .

Huu ni mtihani wa CCM; ni wao wameshindwa na sasa wameanza kutumia nguvu za dola! Wameshindwa kwenye meza ya majadiliano na sasa wanaanza kutumia virungu vya kulazimishana. Nakubaliana na wewe hawa kina Makamba na Kingunge "kwanini wasiachie nafasi hizo wazi waje watu wengine wenye utashi zaidi yao, watu wanaopenda kukaa mezani na kumaliza tofauti zao". Hili ni kweli, kwanini kina Makamba wasiachie ngazi?!

Niliangalia hata wakati wa maandamano ya CUF visiwani wiki iliyopita mmoja wa washairi aliposema kwamba anaweza kujilipua kama mambo yataendelea kuwa hivyo , wengine wakawaambia wenzao wasipeleka bidhaa katika kisiwa kingine wakipeleka basi wao ni halali yao .
Yote hayo yanasemwa viongozi wa CUF wamekaa katika viti wanasinzia wengine wanacheka na kufurahia kwa madaha kama vile ile ni halali yao kusema vile na hakuna chochote kile mbele yake .

Nilitegemea mmoja wa viongozi hawa au msemaji wa CUF aje mbele na kusema kile kilichosomwa na yule mshairi sio msimamo wa CUF lakini hakikutokea kitu kama hicho kwahiyo tuchukulie basi kuanzia sasa hivi na mpaka hapo viongozi wa CUF watakapoamua baadaye

Kwamba sera za CUF kuanzia sasa hivi ni KUJILIPUA , KUKATAZA BIASHARA NA UNGUJA NA KUPUNGUZA UNDUGU WAO kwa sababu hawa wengine sio wanachama wao , wao ni CCM.

Wewe unaweza kuchukulia vyovyote lakini mtu anayehisi kunyanyaswa, kuteswa na kunyimwa nafasi ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake kwenye nchi yake yeye mwenyewe unampa option gani? Tusitengeneze matatizo sisi wenyewe halafu tulaumu wengine. Kuanza kukamata watu na kuwatia kizuizini haiwezekani kuwa ni suluhisho la kudumu la matatizo ya kisiasa. Afrika Kusini walishindwa, Israeli wameshinda, Sadam alishindwa, Hitler alishindwa, Stalin alishindwa na CCM na serikali yake itashindwa vile vile.

Roho ya mwanadamu haifungwi pingu na tamanio la kutambuliwa utu, hadhi, usawa, na heshima ya mwanadamu haikomi kwa mwili kutiwa gerezani. Hakuna Taifa lililoweza kabisa kuzima matamanio ya watu kutambuliwa haki na nafasi yao katika jamii yao.

Njia pekee ya kutatua matatizo ya Pemba si kufungua kesi za uhaini kwani mkiwafunga hawa watoto wao watakuja kuhoji, na mkiwafunga watoto, wajukuu na vilembwe hadi vining'ina vitakuja kuhoji! Njia pekee ni kukaa chini kama ndugu na watu walio sawa, kuchambua tatizo na kiini cha tatizo, kukubali mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi, kutoa mapendekezo na kukubali kutokupata yote mtu atakayo (compromise). Kwa mtindo huu wa CCM kuwa inataka ipate yote, ijue inapandikiza mbegu za tatizo la umilele katika visiwa hivyo.

Ndugu Shy,

Wivu ni kitu kibaya sana na mtu mwenye wivu ni mtu ambaye hawezi kuona wema wa mtu mwingine. Mtu mwenye wivu hutiwa kiza cha macho kiasi kwamba lolote analofanya mbaya wake hata la kuja kumsaidia wakati nyumba yake inaungua mtu huyo atalichukulia kama njama. Ni wazi umezoea siasa za uzugaji ambapo wanasiasa wanafanya mambo kwa kujipendekeza tu na anapotokea kijana mdogo kama Zitto kutikisa nchi kwa kweli haingii akilini.

Alichokifanya Zitto kimeandikwa katika historia na kamwe hakuna anayeweza kufuta! Mchango wa Zitto kwenye mjadala wa hatima ya Tanzania na hali ya kisiasa ni mchango wa kukumbuka na ninaona fahari kabisa kutangaza kuwa natofautiana na Zitto kwenye mambo kadhaa lakini kwenye mambo mengi tuko karibu mno kuliko nilivyodhania. Nilipinga yeye kuingia kwenye Kamati ya Rais ya Madini na yeye anajua hivyo, lakini nimeheshimu ushiriki wake na mchango wake na historia itatuhukumu sote wawili. Na kwa kadiri ninavyoelewa sasa, nadhani historia itanihukumu mimi vibaya zaidi katika hilo.

Lakini nashangaa kwanini umetugusa sisi tulioko Marekani na kutuona kama mazezeta kwamba tunamfuata mtu alimradi tu? Mbona hujahoji Rais Kikwete alipokuja na kukutana na Watanzania New York? au DC? Hii Jumamosi iliyopita Rais Karume alikutana na jumuiya ya Watanzania DC kwanini hilo kwako ni sawa?

Kwa taarifa yako, Mhe. Zitto ni kiongozi wa Kitaifa na si wa Chadema tu. Ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano ambapo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Mashirika ya Umma. Kwanini asikutane na watanzania popote pale anapotaka?

Na nikuhakikishie tu na kukutoa hofu kuwa watakapokuja wabunge wengine wa CUF, au UDP au CCM na wakawa tayari kukutana nasi tutawapokea kwa mikono miwili isiyo na ubaguzi kama unaoupendekeza wewe. Na kwa taarifa yako, Zitto alipokuja hapa nilimuambia mapema kuwa mkutano huu si wa kisiasa, si kufungua tawi na siyo wa chama fulani. Aliheshimu hilo kwani hata watu walipokuwa wanauliza maswali kuhusu Chadema aliyakwepa na kuwakumbusha wasikilizaji kuwa mkutano haukuwa kuhusu Chadema.

Kama Pinda angeweza kufanya hilo alipoenda Iringa kwenye Mei Mosi na kutumia raslimali za serikali kufanya shughuli za CCM basi angeonekana ni mtu makini.

Natumaini nimekusaidia kuondoa wingu la utata, na chuki ya chinichini uliyoianzisha hapa.
 
Kikwete ni smart bana..ngoma watakaoicheza ni kina Zitto na upinzani ..Ye atakuwa amejilaza zake somewhere huko state house huku akiangalia makida za wapinzani za wenyewe kwa wenyewe KWENYE PLASMA TV KAMA ANAYO!
Kwasabau wao walifikiri itakuwa eti simply...Kikwete wa kulaumiwa!
Who said so?
 
wapinzani wana nyimbo ila watu kama Nzoka hamuwezi nyimbo za kizazi kipiya kisichopenda ufisadi ....... lol ...... kwi kwi kwi ... ole wako uanze kucheza wimbo wa mapepe kwenye radio yetu ya jamii huko ......

MWK, mimi niko neutral katika siasa ya Tanzania. Ila kitu kimoja kilichonisikitisha ni kuona Chadema wanawekeza hela kwenye helikopta kumzungusha mgombea wao. Yaani miaka 10, upinzani hawajagundua nguvu iko bungeni? Na kwamba hawana mizizi kama CCM.

Katika miezi 6 ijayo, inatakiwa hawa opposition wawe na kitu kama radio network ya kuweza kuongea na wapiga kura. Mimi wewe, sio wapiga kura. Hawa opposition (let alone CCM) hawana kitu kipya cha kuniambia mimi (au wewe) na wala mimi na wewe kura zetu hazina maana. Watu wenye matatizo wako vijijini. Kuona mtu kama Chenge, Lowassa wakishangiliwa kwao, says a lot more about the opposition than CCM.

Kwahiyo namwelewa Shy anasema nini...............
Hawa wapinzani nawenyewe mafisadi tu. Na jinsi wanavyokosa game plan, ninaanza kuamini hawa ni spoilers tu na sio wapinzani wa kweli.......hawa lazima wana % yao.
 
Tafadhali tuoneshe tangazo hilo na uliliona wapi, "mtandao fulani" usije kuwa ni wa kufikirika. Tuoneshe ilo tangazo na hasa hapo liliposema kuwa "kwa wale ambao hawako busy wanapenda kuonana nae na vijana wengine wengi wenye muelekeo wa kipinzani". Utajijengea heshima kweli kama utamtaja Mbunge huyo na wapi uliona Tangazo hilo lenye maudhui hayo. Binafsi sijaliona na hivyo siwezi kusema kama lipo au halipo. Kama kuna mtu mwingine ameliona tunaomba atusaidie.

Kuonekana kwa kitu kwenye fikra za mtu hakuwezi kuzuilika; kwa mfano inaonekana mafisadi wamewashika watu wengi wa Arusha na Bariadi kiasi kwamba na akili zao timamu wanakurupuka kuwapokea kwa shangwe watu walijiuzulu kwa kashfa!

Ni lini tena Zitto amewahi kukanyaga huku? Cha kushangaza umeshindwa kusema kuhusu maelfu ya watanzania waliokusanyika Jangwani kumsikiliza na wale waliojitokeza katika sehemu mbalimbali za mikoa ya Tanzania. Iweje Zitto kupokewa kama "Mwokozi" Tanzania na Watanzania wenzake ni jambo la kufurahia lakini akipokewa kiukimya Tanzania imekuwa nongwa?

Kwa kukupa taarifa tu, ni mimi niliyempokea uwanja wa ndege na hakukuwa na vimulimuli, saluti, pikipiki, na ngoma za sindimba kama alivyopokewa mzee wa Vijisenti ambaye anaonekana ni mwokozi kule Bariadi! au alivyopokewa yule mwenye ndege iliyopaa huku abiria wameachwa wameduwaa!!

Zitto hakupokewa kwa mbwembwe wala shangwe! Alipokewa kwa heshima ya kiongozi ambaye ameonesha uungwana wa kuja kututembelea hapa kwa gharama zake mwenyewe! Sisi tulitumia kidogo tu kwa chakula na zawadi za jiji la Magari!

Mambo mengine ni ya kufikirika, Kwanini mtu abadilishe sera anazozungumzia wakati tatizo bado ni lile lile? Hii inaelezea ni kwa sababu gani watawala wetu wameacha mambo ya msingi na sasa hawana cha kushikilia na badala yake hawachoki kuja na mipango mipya huku ya zamani ikiwa imekufa. Mara MKUTAKUTA, mara MFISADIKA, mara UKURUTU, n.k.. matatizo ya watanzania yako pale pale.

Hii ni kejeli kwa Watanzania; yaani wewe ufisadi ni suala ambalo mtu alifumbie mdomo? yaani masuala ya EPA kwako ni masuala ya yaliyopitwa na wakati? Leo hii serikali haijui nani mmiliki wa Tangold, wewe unasema imepitwa na wakati? Leo hii haijulikani fedha zinazolipwa Dowans zinakwenda wapi wewe unasema zimepitwa na wakati? leo hii fedha zinaingia upande huu na kutokea upande ule wewe unasema kuzungumzia ni "imepitwa na wakati". Tupe pendekezo basi tuzungumzie mambo ya wakati kama siyo haya yaliyosimika mkuki wa ufisadi nje ya nyumba zetu na kuingia ndani na kuchukua mali na hazina ya watu wa Taifa hili? Wewe unasema yamepitwa na wakati!?

Sijui "Nyepesi" ni nani, lakini inasikitikisha kuwa umeingia kwenye mtego wa kina Lowassa kuwa Wazalendo wa kweli na pekee ni wale walioko nyumbani; kwamba sisi tulioko nje ya nchi ni Watanzania nusu ambao hatutakiwi kutolea maoni. Kwa mawazo yako ni kuwa Mtanzania akishatoka nje ya mipaka basi utanzania wake umepungua kidogo na kwa kadiri anavyoenda mbali na ardhi ya Tanzania ndivyo ambavyo anatakiwa kukaa kimya!

Watu wana mambo mengi ya kuzungumzia ndani na nje ya nchi yao na si wewe na wala si mtu yeyote anayeweza kuamua vinginevyo. Kama ungechukua muda kidogo kusoma Katiba yetu ungeona kuwa haitoi mipaka ya maoni kuwa "mtanzania atakuwa na uhuru wa maoni akiwa Sumve, lakini akienda Mombasa maoni yake yatakoma!". Katika Katiba hiyo hakuna mahalia ambapo panasema "Mtanzania atazungumzia jambo hili akiwa Magomeni lakini akiwa London itakuwa mwiko". Ungeliewa hili ndugu yangu ungefurahia mchango wa mawazo ya watanzania wawapo nyumbani, wavukapo mipaka ya nchi yao na hata wale ambao wanaishi ugenini miaka nenda rudi. Usiwabague Watanzania kwa sababu ya ukazi wao kwa kujifanya wewe ni bora kuliko.

Pamoja na maneno yako hayo, hatutawaachia nchi mafisadi, na hatutapiga magoti mbele ya wabakaji wa nchi yetu na wezi wa mali za taifa letu. Hatutawaimbia nyimbo za shangwe waliondamwa na kashfa na wale watubezao hatuwasusia nchi!

Wakati mwingine mtu anaandika hata ajuia anaandika nini? Hivi unataka kutuambia EPA, ufisadi na Usalama wa Taifa mbovu kabisa ndio Chadema? na CCM wamefanya nini? Ndio watetezi wa Taifa hili? Give me a break!

sasa kama ni si mwanachama wa CUF kwanini uhoji mambo ya CUF; Badala yake ungeuliza huko CCM (kama wewe ni mwanachama) imekuwaje Makamba na Kingunge wanasimamia muafaka? Wana ujuzi gani wa utatuzi wa migogoro? Wangempa Januari nafasi hiyo kwani angalau yeye kasomea mambo hayo!!

Unatania! Viongozi wale wale? Hivi unataka tuanze kuhoji ni chama gani kina viongozi wale wale katika nafasi zake nyingi Tanzania? Kama hujui naomba uulize tu na nitakufa na furaha kuanza kukuorodheshea viongozi wakongwe katika chama fulani na serikali yake hadi sasa watoto na watoto wa watoto wao nao wameanza kurithi vyao! Kama ni sahihi kwa chama hicho iweje liwe kosa kwenye vyama vingine?

Huu ni mtihani wa CCM; ni wao wameshindwa na sasa wameanza kutumia nguvu za dola! Wameshindwa kwenye meza ya majadiliano na sasa wanaanza kutumia virungu vya kulazimishana. Nakubaliana na wewe hawa kina Makamba na Kingunge "kwanini wasiachie nafasi hizo wazi waje watu wengine wenye utashi zaidi yao, watu wanaopenda kukaa mezani na kumaliza tofauti zao". Hili ni kweli, kwanini kina Makamba wasiachie ngazi?!

Wewe unaweza kuchukulia vyovyote lakini mtu anayehisi kunyanyaswa, kuteswa na kunyimwa nafasi ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake kwenye nchi yake yeye mwenyewe unampa option gani? Tusitengeneze matatizo sisi wenyewe halafu tulaumu wengine. Kuanza kukamata watu na kuwatia kizuizini haiwezekani kuwa ni suluhisho la kudumu la matatizo ya kisiasa. Afrika Kusini walishindwa, Israeli wameshinda, Sadam alishindwa, Hitler alishindwa, Stalin alishindwa na CCM na serikali yake itashindwa vile vile.

Roho ya mwanadamu haifungwi pingu na tamanio la kutambuliwa utu, hadhi, usawa, na heshima ya mwanadamu haikomi kwa mwili kutiwa gerezani. Hakuna Taifa lililoweza kabisa kuzima matamanio ya watu kutambuliwa haki na nafasi yao katika jamii yao.

Njia pekee ya kutatua matatizo ya Pemba si kufungua kesi za uhaini kwani mkiwafunga hawa watoto wao watakuja kuhoji, na mkiwafunga watoto, wajukuu na vilembwe hadi vining'ina vitakuja kuhoji! Njia pekee ni kukaa chini kama ndugu na watu walio sawa, kuchambua tatizo na kiini cha tatizo, kukubali mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi, kutoa mapendekezo na kukubali kutokupata yote mtu atakayo (compromise). Kwa mtindo huu wa CCM kuwa inataka ipate yote, ijue inapandikiza mbegu za tatizo la umilele katika visiwa hivyo.

Ndugu Shy,

Wivu ni kitu kibaya sana na mtu mwenye wivu ni mtu ambaye hawezi kuona wema wa mtu mwingine. Mtu mwenye wivu hutiwa kiza cha macho kiasi kwamba lolote analofanya mbaya wake hata la kuja kumsaidia wakati nyumba yake inaungua mtu huyo atalichukulia kama njama. Ni wazi umezoea siasa za uzugaji ambapo wanasiasa wanafanya mambo kwa kujipendekeza tu na anapotokea kijana mdogo kama Zitto kutikisa nchi kwa kweli haingii akilini.

Alichokifanya Zitto kimeandikwa katika historia na kamwe hakuna anayeweza kufuta! Mchango wa Zitto kwenye mjadala wa hatima ya Tanzania na hali ya kisiasa ni mchango wa kukumbuka na ninaona fahari kabisa kutangaza kuwa natofautiana na Zitto kwenye mambo kadhaa lakini kwenye mambo mengi tuko karibu mno kuliko nilivyodhania. Nilipinga yeye kuingia kwenye Kamati ya Rais ya Madini na yeye anajua hivyo, lakini nimeheshimu ushiriki wake na mchango wake na historia itatuhukumu sote wawili. Na kwa kadiri ninavyoelewa sasa, nadhani historia itanihukumu mimi vibaya zaidi katika hilo.

Lakini nashangaa kwanini umetugusa sisi tulioko Marekani na kutuona kama mazezeta kwamba tunamfuata mtu alimradi tu? Mbona hujahoji Rais Kikwete alipokuja na kukutana na Watanzania New York? au DC? Hii Jumamosi iliyopita Rais Karume alikutana na jumuiya ya Watanzania DC kwanini hilo kwako ni sawa?

Kwa taarifa yako, Mhe. Zitto ni kiongozi wa Kitaifa na si wa Chadema tu. Ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano ambapo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Mashirika ya Umma. Kwanini asikutane na watanzania popote pale anapotaka?

Na nikuhakikishie tu na kukutoa hofu kuwa watakapokuja wabunge wengine wa CUF, au UDP au CCM na wakawa tayari kukutana nasi tutawapokea kwa mikono miwili isiyo na ubaguzi kama unaoupendekeza wewe. Na kwa taarifa yako, Zitto alipokuja hapa nilimuambia mapema kuwa mkutano huu si wa kisiasa, si kufungua tawi na siyo wa chama fulani. Aliheshimu hilo kwani hata watu walipokuwa wanauliza maswali kuhusu Chadema aliyakwepa na kuwakumbusha wasikilizaji kuwa mkutano haukuwa kuhusu Chadema.

Kama Pinda angeweza kufanya hilo alipoenda Iringa kwenye Mei Mosi na kutumia raslimali za serikali kufanya shughuli za CCM basi angeonekana ni mtu makini.

Natumaini nimekusaidia kuondoa wingu la utata, na chuki ya chinichini uliyoianzisha hapa.

Hivi hakuna uwezekano wa Zitto kuliwakilisha "TAIFA" kwenye madai ya kuwajibishwa kwa Balali?
Ama na yeye anahisi kuwa BALALI KAFA?

Yote hayo uliyoyasema mkuu ni kweli tupu!
Ila sisi kama Zitto na wengineo hatukuwaona kina Kaborou?
Kina Marando? Lamwai?
Ana umaarufu wa Mzee wa Kiraracha aliokuwa nao?

Ngoja nikwambie something..Viongozi wetu wamekuwa na uwezo mkubwa sana wa ku neutralize issue mpaka zinajifia zenyewe!

Zitto ali imissuse political loop hole kwasababu alijua kabisa kuwa inawezekana Rais akaikalia ripoti hii pia!
Lakini kwasababu alikuwa keshang'atwa na problem ya kutokuwa kazini na jinsi ambavyo licha ya kwamba alikuwa anapambana kwasababu ya wananchi..bado tu bunge lilimtema na hivyo kukosa mshahara wake na marupurupu na kubakia kubebwa na kusukumwa kama vile ilivyokuwa kwa mzee wa Kiraracha!
Kwa hiyo akaangalia akaona mh! Wacha nisikose vyote?
Kwamba yeye kuwepo ama kutowepo kwenye kamati haitaleta utofauti? Hiyo ndio misscalculation!
Atueleze pia kama alikuwa anasupport wazo la kamati ya bunge!
 
Tanzania ni nchi ya tatu kwa umasikini duniani na baadhi ya watu serikalini wanafikiria ni jinsi gani ya kukabiliana na upinzania, usalama wa taifa unatumika kwa siasa wakati Congo China wameinvest $4B na hakuna mipango ya usalama wa taifa kuona Tanzania itafaidika vipi, Zambia kuna boom usalama wa taifa haujaweka mikakati ya kuhakikisha bandari zetu zinatumika, viwanda vya kukata madini hatuna, usalama wa taifa hausaidi wafanyabiashara wa Tanzania kuweza kufanya bishara Rwanda, Burundi, Malawi, Congo na Uganda tumebakia kulumbana na kufanya ufisadi!!!.
 
Hivi Kikwete akisema kuwa anataka aanze kuzishughulikia zile ripoti nyingine zilizopita kabla hajaanza na hii ya madini...! Zitto atasema nini?
 
Mwafrika wa Kike na Mwana Kijiji mnaweza kujibu hilo swali hapo juu?
 
Zitto aseme nini wakati Rais keshasema?
Rais keshasema kuhusu ripoti?
Is it breaking news?

Najua maybe you meant that Rais keshasema kuwa ataitoa hiyo ripoti!
Sasa ni lini huko nyuma alishawahi kusema kuwa hatotoa ripoti?(eventhough utaratibu uko wazi kuwa zinakaliwa?)
 
MWK, mimi niko neutral katika siasa ya Tanzania. Ila kitu kimoja kilichonisikitisha ni kuona Chadema wanawekeza hela kwenye helikopta kumzungusha mgombea wao. Yaani miaka 10, upinzani hawajagundua nguvu iko bungeni? Na kwamba hawana mizizi kama CCM.

Katika miezi 6 ijayo, inatakiwa hawa opposition wawe na kitu kama radio network ya kuweza kuongea na wapiga kura. Mimi wewe, sio wapiga kura. Hawa opposition (let alone CCM) hawana kitu kipya cha kuniambia mimi (au wewe) na wala mimi na wewe kura zetu hazina maana. Watu wenye matatizo wako vijijini. Kuona mtu kama Chenge, Lowassa wakishangiliwa kwao, says a lot more about the opposition than CCM.

Kwahiyo namwelewa Shy anasema nini...............
Hawa wapinzani nawenyewe mafisadi tu. Na jinsi wanavyokosa game plan, ninaanza kuamini hawa ni spoilers tu na sio wapinzani wa kweli.......hawa lazima wana % yao.

Nimesema kwenye previous post yangu kuhusu sera mbadala. Majority ya wananchi tuko vijijini na kipato chetu ni kilimo sasa hawa wapinzani wanachoongea haifikii kijijini ambako ndio tuko wapiga kura.Kama kusambaza manifesto zao kimaandishi haitoshi.

Wanajitahidi na wameweza kuwavuta middle class ambao kwa kweli si wapigaji kura....njooni vijijini....

Sioni kama wapinzani wamefikisha siasa zao pale muhimu panapohitajika come 2010 tusishangae ZZM back in power....kwa nini wasiangalie Chiluba alifanya nini wakati alipoanzisha MMD
 
Shy leo naona ulikuwa umejiandaa kweli kweli, unaelekea sasa kuwa kwenye ile form ya zamani. Nafikiri sasa ukiendelea hivi utamfikia rafiki yangu kada mpinzani. Hila nafikiri majibu umeyapata ya kutosha.
 
Yona Maro is a freelance writer and online researcher based living in Tanzania and frequently contributes to Tips and Topics. He has published numerous articles in local and regional publications on a wide range of topics, including business, education, the arts, and local events.

Karibu JF. Hivi hizi online research unazofanya ndio hizi unazoandika humu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom