BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,109
Posted Date::1/2/2008
Upinzani watangaza mapambano 2008
Salim Said, MUM na Muhibu Said
Mwananchi
VYAMA vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na TLP, vimesema vitautumia mwaka mpya wa 2008 kuendesha mapambano ya kudai katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili kujenga demokrasia ya kweli nchini.
Azma ya vyama hivyo vilivyomo kwenye ushirikiano wa kisiasa, ni miongoni mwa salamu na ujumbe wa mwaka mpya, uliosomwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa niaba ya wenyeviti wenzake wa vyama hivyo, walipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CUF, jijini Dar es Salaam jana.
Akisoma salamu na ujumbe huo, Mbowe alisema mapambano hayo ambayo watayapa kipaumbele mwaka huu, yatatumia mbinu mbalimbali kuishinikiza serikali kuingiza ajenda hizo kwenye utendaji wake ndani ya mwaka huu. Tunautangaza mwaka mpya wa 2008 kuwa ni mwaka wa mapambano ya kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Tumekusudia kuongeza presha ya hali na mali kwa kuwashirikisha wadau wa ndani na nje ya siasa kuhakikisha katiba mpya inapatikana. Pia tunatambua umuhimu wa kuwapo tume huru ya uchaguzi, alisema Mbowe na kuongeza:
Tunayafanya mambo haya kama ndio ajenda yetu kuu kwa mwaka huu, kwa sababu kama itafika mwaka 2009 suala la madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi yatakuwa hayajaingizwa katika ajenda za utekelezaji wa serikali, basi itakuwa vigumu kutekelezwa, kwa kuwa mwaka 2009 hadi 2010 ni kipindi kifupi mno kudai mambo hayo.
Hata hivyo, alisema tayari wameshaandaa rasimu ya katiba ambayo wataipeleka kwa wananchi ili kuijadili na kutoa maoni yao juu ya katiba mpya.
Alisema suala la tume huru, si ushiriki wa wapinzani ndani yake, bali linatokana na mambo mengi, ukiwamo mfumo, sheria, muundo, mamlaka, majukumu na wajibu wake katika mustakbali na mchakato mzima wa kuandaa na kusimamia chaguzi mbalimbali nchini. �Hatuna mfano mzuri na cha kujifunza zaidi ya ni hali ya Kenya kwa sababu tume zinajiona kuwa ni sehemu ya serikali ndani ya nchi husika, alisema Mbowe.
Alisema hali ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania ni matokeo ya jeuri za viongozi wa serikali kupuuza ushauri wa wananchi, sera mbovu, zisizokuwa endelevu zinazopangwa na serikali kwa kuwafanya wananchi kama mateka na kuwafanya wanavyotaka.
Hali hiyo ndugu zangu haitokani na kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia. Hivyo ni visingizio tu vya serikali kwani Kenya, Uganda na hata Msumbiji nao wananunua mafuta hayo hayo na kwenye soko hilo hilo, lakini hakuna mfumko wa bei ya bidhaa kama Tanzania, alisema Mbowe.
Alitoa pole kwa Wakenya walioathiriwa na vurugu za kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomweka madarakani Rais wa nchi hiyo, Mwai Kibaki. Hata hivyo, alisema kitendo cha Rais Kibaki kutangazwa na kuapishwa kushika wadhifa huo haraka haraka ni kuonyesha matokeo ya uchaguzi huo hayakuwa sahihi.
Alisema kutangazwa na kuapishwa haraka haraka kwa Rais Kibaki, hakukufanywa kwa lengo la utendaji bali kumkabidhi madaraka na jeshi kama nyenzo ya kuwakandamiza aliowadhulumu haki zao kwenye uchaguzi.
Akizungumzia michezo, Mbowe alisema serikali imefanya sekta ya michezo kuwa ni jukwaa la propaganda za kisiasa, badala ya kuifanya kuwa sekta nzuri ya kutoa ajira kwa vijana.
Badala ya kuichukulia michezo kama sekta nzuri ya kutoa ajira, serikali ya CCM inaichukulia sekta hiyo kama jukwaa la propaganda za kisiasa ambapo timu yetu ya taifa ikishinda huitwa JK eleven, lakini inaposhindwa huitwa Taifa Stars, alisema Mbowe.
Alisema pia katika mwaka mpya wa 2008, ushirikiano wa vyama vyao, utaendelea kujenga hoja za nguvu ili kuibana serikali na kuwatetea wananchi bila woga na kuwahamasisha Watanzania kuunga mkono upinzani. Vilevile alisema wataendelea kuboresha na kustawisha ushirikiano wa vyama vyao kwa kushughulikia kasoro zinazojitokeza na kujenga hali ya kuaminiana.
Tutaendelea kuufanya ushirikiano wa vyama vyetu usiwe wa viongozi wa juu tu bali uwe ushirikiano wa Watanzania wote walioshikama na kupambanma na mfumo wa chama dola unaowasababishia kuendelea kuogelea kwenye ujinga, maradhi, umaskini, ufisadi na dhuluma kwa miaka 46 ya uhuru bila sababu zozote za msingi, alisema Mbowe.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Juma Duni Haji alidai kuwa tatizo la serikali ya Rais Jakaya Kikwete ni kuweka mbele usanii kuliko utendaji na kudai kuwa kwa kawaida katika nchi zinazofuata mfumo wa utawala bora kunakuwa na uwajibikaji na uwajibishwaji lakini Tanzania hakuna mambo hayo.
Kwa mfano, katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kulikuwa na mtu aliyetakiwa kupasuliwa mguu akapasuliwa kichwa na aliyetakiwa kupasuliwa kichwa akapasuliwa mguu. Ilitakiwa Waziri Mwakyusa (Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David) awajibike, lakini cha ajabu hakuna aliyewajibika au kuwajibishwa isipokuwa tume kuundiwa tume, alisema Haji.
Naye Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia aliwapa pole Watanzania kutokana na kuanza mwaka mpya kwa gharama kubwa za bei mpya ya umeme na kusema kuwa wasitarijie unafuu wowote wa maisha kwa sababu kupanda kwa umeme, kutasababisha kupanda kwa bei za kila kitu.
Nyota njema huonekana asubuhi, kama leo tunauanza mwaka mpya kwa kupandishiwa bei ya umeme, Watanzania tutarajie maisha magumu zaidi.. alisema Mbatia.
Wakati huo hu, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Benedict Mutungirehi alisema kupanda kwa gharama za umeme, kumefanywa ili kuwabana wananchi wafidie madeni ya Shirika la Umeme nchini na kampuni ya IPTL ambapo kila mwezi serikali hulipa zaidi ya Sh3 bilioni.