Upinzani ulioasisiwa na mwalimu Nyerere umefeli, Je turudi kwenye mfumo wa chama kimoja?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Ni ukweli ulio wazi kuwa Upinzani tulionao uliasisiwa kwa baraka za baba wa taifa mwalimu Nyerere baada ya 80% ya watanzania kutaka mfumo wa chama kimoja uendelee.

Ndio nawauliza wanabodi, je huu ndio wakati muafaka wa kuheshimu maoni ya wale 80%?

Au ifanyike kura ya maoni kuukubali au kuukataa mfumo wa vyama vingi nchini?

Mlale unono.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja, sahau! Yaani Watanzania wote zaidi ya milioni 55 tuwe ccm! Tunachofahamu ni kwamba, kuna udikteta uchwara tunalazimishwa kuukubali! hakika nao hautofanikiwa kamwe.
 
Wewe huwa unapenda sana kujipaka kinyesi chako mwenyewe. Hatukuelewi unalenga nini hasa kwa vitendo vyako hivyo. Au yawezekana akili yako haipo sawa.
 
Bado mfumo wa vyama vingi ndio chaguo sahihi kwa checks and balance. Jitihada makusudi zifanyike kuongeza mashariti kupunguza idadi ya vyama.
 
Hivi hapo wewe ndo umefeli kung'amua suala hilo la upinzani kwa undani.

Upinzani haujafeli. Waachieni uwanja wapige siasa muone kama mtakuwepo tena.
 
Upinzani unaachaje kufeli kama kiongozi wao anatawala milele?, anajina yeye ndo mfalme, hakuna haja ya mawazo mapya yeye ndo kila kitu kwao, HAPO LAZIMA WAFELI
 
tapatalk_1573197433883.jpeg
 
Upinzani unaoita watu mafisadi na kisha baadae kuwakubali na kuwapa ugombea uraisi ndani ya wiki..? Huo upinzani lzm udharaulike tu maana chichiem inajua kucheza nao na wanachezwa kisawasawa,usije kufikiri huko upinzani kuna safu nzuri ya uongozi Kama wanamuita chama tawala fisadi na kisha wanamtumia fisadi kutaka kuupata uraisi,hili halina tofauti na kuruka majivu na kukanyaga Moto!! Hao wapinzani acha wafunzwe mpk watakapo komaa!!
 
Watu wanasema hali ndio hii siku mkirudi chama kimoja ni bora tu nkaombe uraia syria najua kazi yangu ni 1 war
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa Upinzani tulionao uliasisiwa kwa baraka za baba wa taifa mwalimu Nyerere baada ya 80% ya watanzania kutaka mfumo wa chama kimoja uendelee.

Ndio nawauliza wanabodi, je huu ndio wakati muafaka wa kuheshimu maoni ya wale 80%?

Au ifanyike kura ya maoni kuukubali au kuukataa mfumo wa vyama vingi nchini?

Mlale unono.

Maendeleo hayana vyama!

Haaa haaaa, unajua ile 80% ilitoka wapi? Waliokuwa wanatembea na dodoso kupata maoni ya wananchi ni wanaccm, na walikuwa wanawatisha wananchi vyama vingi vitaleta vita, na mtu yoyote aliyekuwa anataka mfumo wa vyama vingi alikuwa anapata vitisho vya hali ya juu. Ni kama sasa hivi uende kwenye chombo cha habari kisha uonyeshe kusema ukweli hasi kuhusu Magufuli hicho chombo cha habari lazima kikatize huo mjadala. Bahati nzuri Nyerere alikuwa anajua hila za wanaccm wenzake ikabidi ajiongeze na kuruhusu mfumo wa vyama vingi.

Hii tabia ya ccm kupika data kama Jaffo alivyopika idadi ya wapiga kura ilikuwa ni ya miaka mingi. Nyerere alivyoletewa 20% alijua fika kabisa hiyo tume ingefanya kwa uhuru na kuweka ukada pembeni waliotaka vyama vingi wangekuwa 50+.
 
Ndio nawauliza wanabodi, je huu ndio wakati muafaka wa kuheshimu maoni ya wale 80%?
Nyerere alishasema anawashangaa viongozi wetu kwani yale mazuri yake wanayatupilia mbali lakini mabaya yake ndio wanayakumbatia. Nakuona nawe waelekea huko huko. Lakini kwa kuwa munashikilia bunge mnaweza kupitisha tu kuvifuta hivyo msivyo vipenda. Ni afadhali kufanya hivyo kuliko kuendelea na hizi sarakasi za kishenzi tunazoziona.
 
Upinzani unaoita watu mafisadi na kisha baadae kuwakubali na kuwapa ugombea uraisi ndani ya wiki..? Huo upinzani lzm udharaulike tu maana chichiem inajua kucheza nao na wanachezwa kisawasawa,usije kufikiri huko upinzani kuna safu nzuri ya uongozi Kama wanamuita chama tawala fisadi na kisha wanamtumia fisadi kutaka kuupata uraisi,hili halina tofauti na kuruka majivu na kukanyaga Moto!! Hao wapinzani acha wafunzwe mpk watakapo komaa!!
Nimekuelewa mkuu!
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa Upinzani tulionao uliasisiwa kwa baraka za baba wa taifa mwalimu Nyerere baada ya 80% ya watanzania kutaka mfumo wa chama kimoja uendelee.

Ndio nawauliza wanabodi, je huu ndio wakati muafaka wa kuheshimu maoni ya wale 80%?

Au ifanyike kura ya maoni kuukubali au kuukataa mfumo wa vyama vingi nchini?

Mlale unono.

Maendeleo hayana vyama!
Dhana halisi ya upinzani si tu Chadema ama vyama fulani, upinzani upo ktk fikra na mioyo ya watu na umeanza hata kabla ya vyama viitwavyo vya upinzani kuanza na hata enzi ya chama kimoja upinzani ulikuwepo ila huenda watu walilazimika kuishi katika unafki yaani kukubali kilichokuwepo hata kama hawakitaki.

Upinzani hauwezi kufeli labda kufelishwa na huwezi kumalizwa hata aje yoyote atakaye jinasibu kuumaliza.

Kinadharia, wengi wape hao asilimia 80 Ila kiuhalisia kila mtu anataka kuwepo na machaguo mbadala.

Mfumo wa vyama vingi hauathiri mawazo ya wengi maana kama wengi wanaipenda CCM indelee kuwepo basi wataipigia kura ktk uchaguzi huru na haki, pia uwepo wa upinzani utadhihirisha ukweli kwa chama talawa wapi hawapendwi? vinginevyo tuishi ktk unafki kwamba watu wengi kati ya takribani milioni 50 ati tunapenda chama kimoja.
 
Nimeipenda pointi yako!
 
Back
Top Bottom