Upi Wakati Sahihi Wa Kufanya Mazoezi, Asubuhi Au Jioni?

Gelion Kayombo

Senior Member
Feb 17, 2018
149
193
Kwenye makala yetu ya leo tunaenda kujifunza na kujibu swali amabalo watu wengi hujiuliza upi ni wakati sahihi wa kufanya mazoezi kati ya asubuhi na jioni. Mara nyingi swali hili humjia mtu pindi anapoamua kuanza kufanya mazoezi ya mwili, sasa anakuwa anashindwa kuchagua wakati gani awe anafanya mazoezi hayo.

Kwanza kabisa muda sahihi wa kufanya mazoezi ya mwili hutofautiana baina ya mtu na mtu. Utofauti huu huja kutonaka na kutofautiana kwa ratiba baina ya mtu na mtu. Tofauti hii hufanya mtu fulani kufurahia kufanya mazoezi wakati wa asubuhi na mtu mwingine kufurahia kufanya mazoezi wakati wa jioni.

Ili kujibu swali la wakati gani ni sahihi kufanya mazoezi kwanza tuangalie faida za kufanya mazoezi asubuhi na faida za kufanya mazoezi jioni.

Tembelea blog hii Gelion Kayombo kujifunza makala bora zitakazo badili mtazamo wako wa maisha.

Faida Za Kufanya Mazoezi Asubuhi​

Zifuatazo ni faida za kufanya mazoezi wakati wa asubuhi

Kufanya mazoezi asubuhi hunyoosha mwili

Kufanya mazoezi asubuhi asubuhi hunyoosha mwili na kuandaa mwili kwa majukumu ya siku husika. Hii ni kwa sababu mtu akilala viungo na misuli ya mwili hulegea na kusinyaa. Hivyo kufanya mazoezi asubuhi hufanya viungo na misuli ya mwili kuwa imara.
Huchangamsha akili

Unapolala akili nayo hulala. Huchukua muda akili ya mtu kuchangamka kwa ukamilifu. Njia rahisi ya kuchangamsha akili na kuamsha akili kwa ukamilifu ni kufanya mazoezi. Wale wanaofanya mazoezi wanajua ninacho zungumza hapa.

Huunguza mafuta ambayo mwili hauyahitaji

Asubuhi ni wakati mzuri wa kuunguza mafuta ya vyakula anavyokula mtu kabla ya kulala. Mwili umemeng’enya chakula wakati mtu amelala na mafuta ambayo mwili hauyahitaji umeyahifadhi. Asubuhi ni wakati sahihi wa kuondoa mafuta hayo. Na utaweza kuondoa mafuta hayo kwa kufanya mazoezi asubuhi.

Hufanya siku ya mtu kuwa yenye furaha

Faida za kufanya mazoezi asubuhi haziishii tu wakati mtu anafanya mazoezi tu. Faida za kufanya mazoezi hudumu siku nzima. Hii ni kutokana na mwili huzalisha kemikali fulani zinahusika na kumfanya mtu ajisikie vizuri. Kemikali inayomfanya mtu ajisikie vizuri huzalishwa kwa wingi na kwa haraka pindi baada ya mtu kuchangamsha mwili kwa kufanya mazoezi.

Faida Za Kufanya Mazoezi Jioni​

Zifuatazo ni faida za kufanya mazoezi wakati wa jioni

Kufanya mazoezi jioni husaidia mtu kulala usingizi mzuri

Kwa sababu ya damu kuzunguka vizuri mwilini baada ya kufanya mazoezi husaidia mtu kulala usingizi mzuri.

Utakuwa na nishati(energy), nyingi mwilini mwako

Kufanya mazoezi jioni hufanya mwili uwe na nishati nyingi nyingi mwilini. Nishati hiyo huhusika na mtu kuamka asubuhi akiwa mchangamfu bila uchovu wowote.

Ni namna nzuri ya kumaliza siku yako

Umetoka kazini, siku yako ilikuwa imejaa kurupushani kiasi kwamba hujafurahi kabisa siku yako. Namna rahisi ya kurudisha mwili wako katika hali ya kawaida na bora ni kufanya mazoezi jioni. Mazoezi yatakuondolea msongo wa mawazo na maumivu mbalimbali uliyopitia katika siku yako.

Kuwa Na Muda Wa Kutosha Wa Kufanya Mazoezi

Ufanyaji wa mazoezi wakati wa jioni humfanya mtu kufanya mazoezi kwa kustarehe kwani anakuwa na muda wa kutosha wa kufanya mazoezi. Tofauti, na wakati wa asubuhi ambapo mtu anakuwa na mawazo ya kwenda kazini au kukabiliana na majukumu ya siku husika.

Pia ufanyaji wa mazoezi jioni unaweza kupelekea mtu kuchelewa kulala kutokana na mwili kuwa na nishati ya kutosha na kuchangamka sana.

Kwa hiyo ili kujibu swali la upi ni wakati sahihi wa kufanya mazoezi ya mwili kati ya asubuhi na jioni naweza kujibu kama ifuatavyo; Unaweza kufanya mazoezi muda wowote kati ya asubuhi au jioni. Ingawa ufanyaji wa mazoezi wakati wa asubuhi unaonesha kuwa na matokeo bora zaidi kuliko kufanya mazoezi wakati wa jioni. Faida za kufanya mazoezi wakati wa asubuhi ndiyo kama nilivyotaja kwenye makala hii. Faida nilizotaja hapa siyo peke yake, zipo na nyingine nyingi tu.

Hitimisho​

Wakati wowote unaweza kufanya mazoezi ya mwili kutegemeana na ratiba zako. Unaweza kufanya mazoezi asubuhi au unaweza kufanya mazoezi jioni. Ingawa kufanya mazoezi wakati wa asubuhi kuna faida nyingi kuliko wakati wa jioni. Utaweza kujijengea nidhamu binafsi haraka kama utafanya mazoezi wakati wa asubuhi.

Kusoma makala nyingine zitakazo badili mtazamo wako tembelea blog hii Gelion Kayombo.

Nakutakia wakati mwema
 
muda wowote unaweza kuwa Sawa kutokana na nafasi ya mtu. ingawa wapo wanaosema muda wa asubuhi mapema ni mzuri zaidi kwasababu ya mtu anaepuka moshi wa vyombo vya moto yaani kuvuta hewa chafu.
 
muda wowote unaweza kuwa Sawa kutokana na nafasi ya mtu. ingawa wapo wanaosema muda wa asubuhi mapema ni mzuri zaidi kwasababu ya mtu anaepuka moshi wa vyombo vya moto yaani kuvuta hewa chafu.
Ni kweli mkuu. Hata mimi napenda kufanya mazoezi wakati wa asubuhi
 
Back
Top Bottom