RAMAJ
Member
- Sep 24, 2018
- 88
- 88
Siku ya jana, tumeshuhudia na kusikia hukumu iliyotolewa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania juu ya kipindi maarufu cha Jahazi kinachoruka kupitia Clouds Fm.
Hukumu hiyo imekuja baada ya watangazaji wa kipindi hicho akiwemo G. Habash, Dj Fetty na wenzao kukiuka miiko na maadili ya utangazaji.
Watangazaji hao kupitia kipindi hicho kilichokuwakikiruka kila siku za wiki kuanzia majira ya saa 10 alasiri walisikika wakihamasisha jamii kufanya tendo la kujichua yaani "Punyeto". Jambo ambalo ni kinyume na maadili ya jamii yetu na kuwafunza tabia mbovu vijana na watu mbalimbali.
Baada ya kipindi watangazaji pamoja na msimamizi wa kipindi, Abdul Chembea, msimamizi wa maudhui wa Clouds, Seba Maganga pamoja na Sheba Kusaga waliitwa na kuhojiwa. Wote walikiri makosa hayo na uongozi wa Clouds uliwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji wawili, mmoja akisimamishwa kazi mwezi mmoja na Dj Fetty akisimamishwa kazi wiki mbili.
Pamoja na hayo, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania wanasema kuwa, vitendo hivyo vimekuwa vikijirudia rudia kwa watangazaji wa kipindi wa kipindi hicho ambapo, mwezi June mwaka huu waliitwa kutokana na kukiuka miiko na maadili ya utangazaji wakiwa katika kipindi hicho na walikiri kosa na kupigwa faini ya million 5.
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, imekifungia kipindi hicho na kuwaambia CMG wasizalishe kipindi kingine tena chenye maudhui yanayofanana na kipindi hicho katika muda husika. Pia, wamepewa rai ya kuwapa mafunzo watangazaji na wasimamizi wa vipindi juu ya miiko na maadili ya utangazaji. Kadhalika, kuzihariri taarifa na maudhui ya siku husika kabla ya kwenda hewani.
Watu mbalimbali wapenzi na wafwatiliaji wa kipindi hicho wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii. Wengine wakisema kuwa walikuwa wanafanya 'comedy'. Wengine wakisema hivyo ndivyo kipindi kinachangamka kwani hakuna mtu anaeyazingatia.
Upi mtazamo wako?