Upi mtazamo wako juu ya kipindi maarufu cha Jahazi kufungiwa?

RAMAJ

Member
Sep 24, 2018
86
83
Siku ya jana, tumeshuhudia na kusikia hukumu iliyotolewa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania juu ya kipindi maarufu cha Jahazi kinachoruka kupitia Clouds Fm.

Hukumu hiyo imekuja baada ya watangazaji wa kipindi hicho akiwemo G. Habash, Dj Fetty na wenzao kukiuka miiko na maadili ya utangazaji.

Watangazaji hao kupitia kipindi hicho kilichokuwakikiruka kila siku za wiki kuanzia majira ya saa 10 alasiri walisikika wakihamasisha jamii kufanya tendo la kujichua yaani "Punyeto". Jambo ambalo ni kinyume na maadili ya jamii yetu na kuwafunza tabia mbovu vijana na watu mbalimbali.

Baada ya kipindi watangazaji pamoja na msimamizi wa kipindi, Abdul Chembea, msimamizi wa maudhui wa Clouds, Seba Maganga pamoja na Sheba Kusaga waliitwa na kuhojiwa. Wote walikiri makosa hayo na uongozi wa Clouds uliwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji wawili, mmoja akisimamishwa kazi mwezi mmoja na Dj Fetty akisimamishwa kazi wiki mbili.

Pamoja na hayo, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania wanasema kuwa, vitendo hivyo vimekuwa vikijirudia rudia kwa watangazaji wa kipindi wa kipindi hicho ambapo, mwezi June mwaka huu waliitwa kutokana na kukiuka miiko na maadili ya utangazaji wakiwa katika kipindi hicho na walikiri kosa na kupigwa faini ya million 5.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, imekifungia kipindi hicho na kuwaambia CMG wasizalishe kipindi kingine tena chenye maudhui yanayofanana na kipindi hicho katika muda husika. Pia, wamepewa rai ya kuwapa mafunzo watangazaji na wasimamizi wa vipindi juu ya miiko na maadili ya utangazaji. Kadhalika, kuzihariri taarifa na maudhui ya siku husika kabla ya kwenda hewani.

Watu mbalimbali wapenzi na wafwatiliaji wa kipindi hicho wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii. Wengine wakisema kuwa walikuwa wanafanya 'comedy'. Wengine wakisema hivyo ndivyo kipindi kinachangamka kwani hakuna mtu anaeyazingatia.

Upi mtazamo wako?
 
Clouds nawenyewe wameshazoea mifaini tu halafu kile ni kipindi cha watu wazima na akili pevu Ni aibu kwa kosa kama Lile!,hayo mambo mengine wawaachie watoto huko ndo basi tena jaramba limeshapita watulie tu waje na maudhui mengine ila jahazi ije irudi ni kipindi kizuri.
 
Hundred percent masturbation kuliko ngono hawa vijana wasiojitambua watazidi kupotea zaidi...sasa hao watoto waanze kutongozana tena alafu wanapiga kelele mimba za utotoni..... what the hell!!.....?
 
Kwahiyo nyeto ina ubaya gani? Mbona radio zingine zinahamasisha utumiaji wa condom kuzuia maambukiz na hawafungiwi? Nyeto na kutumia condom ni kitu kilekile tu alaf nyeto iko salama zaidi, inazuia maambukiz na inapunguza stress
Kimaadili, si sahihi. Na kiafya pia si sahihi. Nafikiri wengi tunaelewa madhara ya kujichua. Hatuwezi kupigia debe kitu ambacho tunajua kina madhara na kinakiuka maadili.

Swala la condom ni kinga dhidi ya magonjwa. Hivyo inachukuliwa kama tahadhari.
 
Kimaadili, si sahihi. Na kiafya pia si sahihi. Nafikiri wengi tunaelewa madhara ya kujichua. Hatuwezi kupigia debe kitu ambacho tunajua kina madhara na kinakiuka maadili.

Swala la condom ni kinga dhidi ya magonjwa. Hivyo inachukuliwa kama tahadhari.
Hakuna utafit wowote wa kisayansi unao thibitisha nyeto ina madhara
 
Hii kasumba ya kuokoteza watu waropokaji wasio na weledi na kuwapa vipindi haina afya kwa tasnia ya habari, eti wanaojiita ‘wachekeshaji’ ndo wamekuwa watangazaji!!
 
Hii kasumba ya kuokoteza watu waropokaji wasio na weledi na kuwapa vipindi haina afya kwa tasnia ya habari, eti wanaojiita ‘wachekeshaji’ ndo wamekuwa watangazaji!!
Very good point. Swala la kufanya kazi bila weledi litatafuna vyombo vya habari vingi ikiwa Mamlaka zinazosimamia vyombo hivi vitasimamia sheria na kanuni kama inavyopaswa.

Taarifa siku hizi hazichakatwi, hazihaririwi. Uropokaji ndiyo umekuwa msingi wa utangazaji.

Kuna upande tasnia imepwaya, hakika.
 
Hii kasumba ya kuokoteza watu waropokaji wasio na weledi na kuwapa vipindi haina afya kwa tasnia ya habari, eti wanaojiita ‘wachekeshaji’ ndo wamekuwa watangazaji!!
Kuna vipindi havihitaji kuwa seriously na kukaza uso ili kukiendesha.
Ni soga tu Kama kijiweni na kipindi kinaenda swaafi kabisa.

La muhimu kusiwe na maneno mengi yenye ukakasi Kama aliyokuwa anayatoa Marehemu Kibonde..yule alikuwa mropokaji haswa
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom