Morning Express ya UFM ni kipindi bora cha asubuhi kwa Tanzania

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,945
7,947
Habari zenu jamani, Beberu nawasalimu kwa bashasha kubwa,

Kwa vipindi vya Asubuhi ndani ya nchi hii hakuna kipindi bora zaidi ya Morning Express cha UFM.

Napendea kipindi hiki vitu vifuatavyo:

✓ Wanatumia kiswahili sanifu sana, Hakuna kiswanglish huku

✓ Wanareport kwa utaratibu, hakuna kupandiana juu kama Wasafi au Clouds 360

✓ Hawa jamaa hawana ujuaji, wao kama ni issue ya utalaamu lazima watamleta mtaalamu wa eneo husika, redio nyingi watangazaji wana ujuaji hadi wanakera, (hususani wawe wanachambua taaluma yako halafu ushuhudie wanavyoongea uongo kwa kujiamini)

✓ Wanahoji watu wazito kwa uhuru sana, UFM kumpigia simu mkuu wa mkoa, au waziri ni chap tu, na wanamhoji kwa utulivu

✓ Wanautulivu sana, hawana kelele, ni rahisi mtu kukuuliza kama unasikiliza BBC au DW kumbe upo na UFM tu

Na nyingine nyingi, Mimi Beberu nawapongeza, kila morning kabla sijaenda kujenga nchi (wakati najiandaa) lazima niwasikilize, kazeni sana

Kwa kifupi nawapa maua yenu

Wenu yule yule wa siku zote

Beberu J
 
Nawasikiliza kwenye michezo na kipindi fulani Cha Reggae

Asubuhi mi ni wasafi michezo

Usiku taarifa ya habari Kisha

Sports Extra ya clouds na Mchongo wa big Joe
 
Nawasikiliza kwenye michezo na kipindi flani Cha Reggae
Asubuhi mi ni wasafi michezo
Usiku taarifa ya habari Kisha
Sports Extra ya clouds na Mchongo wa big Joe
Michezo si hadi saa 2 na nusu, Morning Express ni saa 12 asubuhi
 
Mimi radio napenda kusikiliza, morning nikiwa naoga, nakunywa chai inakuwa inanipa updates
Bado mnasikilizaga Radio, Aisee tunatofautiana sana, huo ujinga sifanyia , Radiobna TV
A
 
Mimi radio napenda kusikiliza, morning nikiwa naoga, nakunywa chai inakuwa inanipa upd
Bado mnasikilizaga Radio, Aisee tunatofautiana sana, huo ujinga sifanyia , Radiobna TV
A
 
Back
Top Bottom