Upendo ni nini?

Upendo ni nini?

Joined
Jun 15, 2019
Posts
75
Reaction score
99
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali. Hivi upendo ni nini? au upendo unatoka wapi? mtu akipendwa anahisije? '

Maana sisi ni nyama, damu na maji, kwanini mtu akiumizwa kwenye mahusiano yoyote anaumia na wakati hajaguswa? kwanini kuna wivu?

Kwanini mtu akimpenda mtu mwingine anakuwa na wivu? No offense, only ciritcal thinking. Hiki ni nini?
 
Ina maana upendo unaooulizia ni ule wa bibi na bwana tu sio? Nionavyo mimi hii haiwezi kukupa maana halisi ya upendo, maana kwa sehemu kubwa upendo huu ni conditional , unategemea muonekano wa mtu, tabia, social status, benefits NK. Ndio maana leo unaweza kumpenda huyu kesho yule. Upendo halisi unaweza kuelezewa kwa mfano ule upendo wa mama na mtoto ambao ni unconditional, hata akiwa kichaa utampenda tu, hata akiwa mchawi utampenda tu.
 
"Nothing is a coincidence.
Every person you meet is written in your destiny to teach you, to heal you, or to love you. 💖🍀🦋"
 
Nadhani upendo ni hisia
Hisia sio kitu kinachoweza kuonekana

Kwa Mf: issue ya mahusiano ya kimapenzi ukipendwa utahisi utaona pia kwa matendo ya yule mtu

Ukiona unaanza kujiuliza et huyu ananipenda ujue hapo hakuna upendo
Penye upendo wa kweli hakuna alama ya kiulizo
 
Ni muunganiko wa hisia na akili unaoamua jinsi unavyomuona mtu mwingine kuwa muhimu zaidi kuliko kawaida.

Ukiibiwa, kudanganywa au kupuuzwa na mtu unayemjali, ubongo huwa unachukulia kama umepoteza kitu cha thamani, hali inayopelekea uhisi maumivu sana.
 
Upendo ni upekee wa Mungu alioudhihirisha kupitia YESU:

1) Alitupenda tukiwa hatustahili upendo wake

"Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu."
Waroma.5.8.BHN

2) Alijitoa / aliacha vya hadhi ya juu kwa ajili yetu

"Bali, kwa hiari yake mwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu, akaonekana kama wanadamu.

Alijinyenyekesha na kutii mpaka kufa, hata kufa msalabani."

Wafilipi.2.7-8.BHN

3) Alitoa uhai wake kwa ajili yetu.

"Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake."
Yohana.15.13.BHN

So ili kuthibitisha kama mtu kapenda au anakupenda atiki pote hapo:

Unakuta mtu kutwa kukutoa kasoro kukueleza kwanini hufai. Kukosoakosoa. Wanakwambia judge them by their past. Forgive but never forget.

Mtu baada ya muda anakuacha / anakusaliti akafuate anavyoona vyenye hadhi ya juu zaidi. Wanakwambia tafuta pesa ule vitu vizuri.

Na kuhusu uhai ndo kabisa
:2Head:
wanakwambia umezaliwa peke yako utakufa peke yako. No one is coming to save you.

Kulikuwa na this joke some time back: majambazi waliingia ndani wakawaweka mume na mkewe chini ya ulinzi, wakawaona majambazi yanajitayarisha kubaka, mume akamuambia mkewe sasa wewe tulia kila watakachotaka kubali tu ili wasitudhuru. Jambazi likamuita mwanamke kumuuliza mafuta yako wapi wanataka kumfuata mumewe yeye mke atoke. Mke akaenda kuwaonyesha akamuambia mume wangu wamesema ni wewe wanakutaka so kama tulivyokubaliana tulia ufanye yote wanayotaka wasitudhuru :2Head: .

Mungu ndiye Upendo, hakuna atakayekupenda zaidi yake,

though I beleive if the Spirit of God truly dwells in that person then God's character will be reflected through them. Indeed they will love you even when you don't deserve it, they will sacrifice themselves for you and surely they will die for your sake.
 
though I beleive if the Spirit of God truly dwells in that person then God's character will be reflected through them. Indeed they will love you even when you don't deserve it, they will sacrifice themselves for you and surely they will die for your sasake.
Hapa wamama kwa watoto ndo wanadhihirisha kweli Upendo upo. Ingawa wamama wa siku hizi wa mwendo kasi: wanaua watoto tumboni mwao, wanazaa wanawatupa, wanawabwaga watoto wao kwa watu.....

Ukiona mmama na beseni lake kichwani na mtoto mgongoni muheshimu sana. Muangalie vizuri, ndo Upendo huo unaoutafuta.

Nilimuuliza mmoja sasa huchoki kutembea naye siku nzima? ? Anasema sasa nifanyaje, kwanza nina amani nashinda naye kuliko kumuacha huko na watu 🙌🏾
 
Ina maana upendo unaooulizia ni ule wa bibi na bwana tu sio? Nionavyo mimi hii haiwezi kukupa maana halisi ya upendo, maana kwa sehemu kubwa upendo huu ni conditional , unategemea muonekano wa mtu, tabia, social status, benefits NK. Ndio maana leo unaweza kumpenda huyu kesho yule. Upendo halisi unaweza kuelezewa kwa mfano ule upendo wa mama na mtoto ambao ni unconditional, hata akiwa kichaa utampenda tu, hata akiwa mchawi utampenda tu.
Sidhani kama umemwelewa, anamaanisha Kwa Nini mtu anaumizwa na mapenzi!! Kupitia kujua huko ndo apate maana halisi ya upendo
 
Hapo Kila mtu atakuja na maneno, which is nothing, hakuna maana kwenye emotion. Depth ya hisia haiwezi kuelezeka. Ni nature, na sometimes tunafeel vitu based on past experiences, what we see and how we were raised. Kwa hiyo it is what it is.
 
Pia na expectation inahusika kutengeneza upendo, unapoona mtu au kitu ni kizuri akili inaanza kutengeneza mategemeo kuwa nikiwa nacho nitakuwa na furaha, hivyo hutengeneza physiological response kama arousal
 
Sidhani kama ni kweli. Kuna vitu vingi vizuri hapa duniani, lakini kumpenda mtu Huwa inakuwa unique... Hujawahi kukutana na demu mkali ila tu nafsi ikagoma? In the long run unaweza ukawa attracted Kwa muda ila upendo Huwa sio matamanio
 
In the long run unaweza ukawa attracted Kwa muda ila upendo Huwa sio matamanio
Umeniquote vibaya sijasema matamanio nimesema mategemeo

upendo wowote huwa unaishi kwa mategemeo, pale mategemeo yanapoanza kupungua basi na upendo unapungua, ndio maana watu wakiachana kauli kama haupo kama nilivyotarajia huwa zinahusika, sababu ulitegemea kitu fulani kwake na kama huwezi kukipata tena basi upendo unaisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom