Upendeleo kwa Wanawake una Faida kweli Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upendeleo kwa Wanawake una Faida kweli Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jasho la Damu, Jul 21, 2011.

 1. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mlinganisho wowote kati ya mwanamke na mwanaume kwa pamoja kwa kuzingatia vigezo vyenye mizani sawa alwayz mwanaume atashinda tu. Hebu tuangalie mifano halisi katika nchi yetu mambo yanavyoenda. Pamoja na kuwa na sera ya upendeleo kwa wanawake huku tukiamini ukimuinua mwanamke umeinua jamii nzima. Je hv ni kweli Tz tumefanikiwa kwenye dhana hii ya upendeleo? Viti Maalumu, Mawaziri wa kike, Makinda, Migiro wametusaidia nini Tz. Je tumebadilika kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
   
 2. U

  UNDULE ROBERT Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sahihi, lakini usiwaangalie hao tu. Lengo la nafasi maalum lilikuwa ni muhimu lakini kama unavyojua mabaya hayakosi kama ilivyo tumeona wabunge wengi wa viti maalum wana upeo mdogo, wengi wanakwenda kutoa taarifa bila research, wengi pia hata uvaaji wao unapotosha maadili ya kitanzania kama vile wengine wanavaa vikuku, nguo za matiti nje, skirt fupi n.k. Kwa sasa umefika wakati tuwe na jopo la kupitisha viongozi bila kujali anagombea kupitia chama gani, kwa maana huko tunakoelekea uongozi wa tz unaonekana umekuwa cheap mno. Tutakuja kuongozwa na wahuni siku moja.
   
 3. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi chukulia mfano kwamba mwanamke anapendelewa marks kisha akawa Daktari, Je, magonjwa yatamwelewa kuwa huyu ni mwanamke?
   
 4. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kaka hapa umenena.
   
 5. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  UNDULE
  Mwanamke hv sasa akipata nyadhifa ya juu basi lazima kutakuwa na walakini ndani ya mchakato wa kumpatia yeye uongozi. wapo ambao uteuliwa kwa kuwa ni vimada wa wakubwa ama ni mapuppet wa dili fulani. Hata hivyo wanawake wengi huwa wanapwaya sana katika nafasi zao. Huku kwetu Ngorongoro tuna mwanamama ambaye ni DALDO yeye kazi yake kutengeneza bifu na watumishi wake huku akitegemea jinsia yake ya kike itamlinda.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Mfano mwingine mzuri ni Zakia Meghji!
   
 7. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Anna Makinda, Vicky Kamata, Dovtwa Likokola etc.
   
 8. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ninaamini wanawake wanatakiwa kulindwa wasinyanyaswe wakakosa haki zao. Lkn sio vema kuwalazimishia nafasi ambazo hawana uwezo nazo kisa kubalance gender inakua sio sahihi kabisa. Muhimu ni kuona mwanamke mwenye uwezo asinyimwe nafasi kisa mwanamke period!
   
 9. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yup Mkuu nimekusoma vizuri ila tuondoe pia zile dhana za kusema sasa tunataka mwanamke aongoze nafasi hii hali ya kuwa hana uwezo huo.
   
 10. delabuta

  delabuta Senior Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na hoja, mimi ni mwanamke lakini naunga mkono hoja hii kweli huu upendeleo kwa wanawake uangalie uwezo wa wanawake wenyewe na sio kubeba watu hata hawana uwezo basi tu kama huyu mama anatutia aibu kubwa kwa jinsi alivyobebwa bebwa mpaka uspika wakati hana uwezo wa kuwa spiker wa bunge jamani magamba mnatutia aibuuuu wanawake wakati wanawake tunaouwezo bila kubebwa.
   
 11. n

  neyro JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 232
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  mi huwa naumia mno kwa nafasi hizi za upendeleo. Nadhani BEIJING CONFERENCE haikueleweka kwa wengi. hebu turudie vile vipengele vyote thn tuone kama imeainisha kwamba hata kama mtu hana sifa apendelewe. tunapenda upendeleo sana ndo mana wanatuvua sana tu mwisho wa siku hatuna cha ku-reason!! TUTABAKI TUBULA RASA milele kwa kutojishughulisha na kungoja upendeleo. MUNGU TUSAIDIE WENYE UCHUNGU NA NAFASI ZA UPENDELEO!!!!!!
   
 12. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Thanx dada umesema ukweli. Hebu mtazame SOPHIA SIMBA HASTAHILI KUWA HATA KIONGOZI WA UKOO ikiwa
   
 13. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Hakuna walichotusaidia zaidi ya hao akina mama kuishi maisha mazuri na ya anasa kuliko wanawake wengine wasio na nafasi hizo za upendeleo.

  Msimamo wangu: -
  (a) Nafasi zote za viti maalum bungeni ziondolewe, kila mtu agombee jimboni kwa usawa kati ya wanawake na wanaume
  (b) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto ivunjwe, kazi zake za kuendesha vyuo vya maendeleo ya jamii ziwe chini ya VETA, tubaki na idara tu katika kila halmashauri kuangalia watoto wa mitaani, yatima n.k. Aidha shughuli nyingine zote ziende katika wizara husika mfano Afya, Ujenzi, Mambo ya Ndani n.k.

  Kwa kufanya hivi serikali itaokoa mamilioni ya kodi za Watanzania yanayotumika bila tija.
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Upendeleo huo hauna faida yoyote, unatutia hasara. Mfano viti maalumu ni kero, visitishwe!
   
 15. L

  Ledio Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka MMASAI huyo DALDO wa Ngorongoro kumbe nawe unamjua. Katika wakuu wa idara vibuyu huyo nafikiri anaongoza. watumishi wake wanamwekea mitego wanamwandikia ripoti mbaya naye kwa ujinga wake anasoma kwa watu bila kupitia. Huyo mama ni kibuyu haswa anashindwa kazi hata na watumishi walioko chini yake.
   
 16. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ledio namjua huyo mama lkn kwa ujumla Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ni hovyo kuanzia DED-Afisa Mtendaji wa kijiji.
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  nafasi za wanawake kwenye uongozi wa kisiasa sio tatizo, nadhani shida iko kwenye mchakato wa jinsi ya kuwapata hao wagombea. lakini pia wenye uwezo wa kuzimudu nao hawana interest kwa sababu hizi tunazoongelea hapa!
  kwa sababu ya mfumo ambao ulikuwepo kwa muda mrefu na kujenga mazingira kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi, ipo haja ya kuweka upendeleo katika nafasi fulani fulani so that they can prove a point. kwa mfano mzuri: ungemuona HAlima Mdee siku ya kwanza katokea anakuomba kura yako, ungeweza kumpa? Lakini alipata upendeleo, aka-prove capable na sasa anapambana kiume. MMeaning sasa jinsi yake sio issue tena

   
 18. A

  ACTIVISTA Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sijawhi kukutana na best reasoner like yuo in JF... hakuna haja ya kuwapendelea after all wanawake ndio wapo wengi kuliko wanaume, kwa sera za kuwapendelea tuuuu tutajakuta mfumo umejaa wanawake watupu
   
 19. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  King'asti
  Kama kuna mfumo mbovu wa kuwapata hao wagombea wa viti maalumu ambao unapelekea wanawake wenye uwezo wasipate nafasi hizo basi hakuna haja ya kuwa na upendeleo kwa wanawake maana dhana nzima ya upendeleo kwa wanawake ni kupata constructive ideas frm them on how govt can improve socio-economic of women. Hebu mtazame Vicky Kamata anasema yeye ndo kwanza anajifunza kuongea bungeni kwa maana ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni kumbe wao wanajifunzia bungen na bunge limekuwa chuo cha mafunzo.
   
 20. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana na hoja kwamba kuwapendelea wanawake siyo njia sahahihi ya kuendesha nchi hasa nafasi za uongozi! Lakini napenda pia kutofautiana kidogo kwenye wazo la kusema hata wao walioko madarakani wamefanya nini? Kwani wao wanaume walioko madarakani wao wamefanya nini? Jk, Ngeleja, Jairo, Hosea, Chenge,n.k waha nao ni wanawake jamani? wao wamefanya nini kwa taifa hili? Tatizo hapa siyo mwanamke au mwanaume, ila ni upeo wa kufikiri sahihi na kuongoza kwa sheria na kanuni.
  Labda nitoe mawazo yangu kwani nafikiri wanawake walioko madarakani wanashindwa kuperform kama tulivyotarajia
  1. Mchakato wa kuwapata waha wanawake kwa kiasi kikubwa unafanya na wanaume ( wanaume ndiyo wanawaweka pale, ndiyo wenye maamuzi kwenye nchi hii, nani akae pale au nani aondoke)
  2. Wanawake wengine wanaingia kwa nguvu ya pesa (money baba) badala ya uwezo wao wa akili. Hi inatokana na mfumo wa kuendesha nchi kwa rushwa. Mfumo huu umewekwa na wanaume wanaoliongoza hili taifa tajiri sana duniani lenye watu waliokisiri na umasikini.
  3. Wale wanawake wachache ambao wametumia uwezo wao wa akili hawawezi kutimiza malengo yao kutokana na mfume dume wa nchi (angalia Beatrice shelukindo sasa ametishiwa hata kuuawa). Wanawake wanawezaje kuonyesha uwezo wao kwenye mfumo huu kandamizi na wa kulindana?
   
Loading...