Napoleon the second
Member
- Aug 25, 2019
- 79
- 80
EPISODE ONE
________________________________
UCHAMBUZI MAKINI WA KITABU CHA:
"SIRI ZA AKILI YA MTU TAJIRI" (SECRETS OF THE MILLIONAIRE MIND).
NA:
LEONARD JULIUS SHIGANGA WA MWANAMATINGATINGA.
Kitabu hiki kimeandikwa na T. HARV EKER, ambaye ni milionea, mwandishi na mzungumzaji maarufu nchini marekani. Kupitia mafudisho yake, watu wengi wametajirika na kufanikiwa sana kutoka kwenye umasikini wa kutupwa hadi kuwa milionea.
Ikiwemo mwandishi yeye mwenyewe (Eker), ambaye hapo awali alikuwa maskini wa kutupwa lakini mara baada ya kuzijua na kuzifanyia kazi SIRI hizi aliinuka na kuwa milionea ndani ya muda mchache.
Karibu tujifunze kwa pamoja SIRI ZA AKILI YA MTU TAJIRI. Siri ambazo watu waliofanikiwa walizitumia na wanaendelea kuzitumia ili kujiletea utajiri zaidi na zaidi.
Eker, ambaye ni tajiri mkubwa anasema kwamba, watu waliofanikiwa huwa wanafikiri kwa namna fulani ambayo ni tofauti sana na jinsi watu maskini wanavyofikiri na kupitia tofauti hiyo ya fikira ndio inaamua matendo yao na kuleta matokea tofauti kati ya mtu tajiri na maskini.
EKER, anaendelea kusema kuwa, kama utafikiri kwa njia ambayo matajiri huwa wanafikiri na kufanya kile ambacho matajiri wanafanya, utakuwa miongoni mwao.
(Shika kichwa chako na useme kwa imani)
"NINAKICHWA CHA DHAHABU"
Eker, anatufundisha somo kuwa, ikiwa unataka kupiga hatua flani katika maisha kuelekea juu, lazima uwe tayari kuachilia baadhi ya fikira zako za zamani ambazo zimepitwa na wakati au fikira potovu na kuwa tayari kukopi na kujifunza fikira mpya zitakazokusaidia kupiga hatua na matokeo yake yatajizihilisha menyewe.
MWONGOZO JUU YA PESA NA MAFANIKIO.
Eker, katika kitabu chake ameonyesha kuwa SHERIA ZA PESA zimegawanyika katika makundi makuu mawili.
KUNDI LA KWANZA: sheria ya PESA ya ndani au mwongozo wa PESA uliyoko ndani kabisa ya mtu. Mwongozo huu unatokana na maswali yafuatayo:
i: wewe ni nani?
ii: unawaza nini?
iii: unaamini nini kuhusu pesa?
iv: tabia zako ni zipi?
v: unajiamini vipi?
Vi: ni kweli kuwa unahisi unasitahili kuwa tajiri?
Vii: uwezo wako wa kutenda dhidi ya hofu ni upi?
Ukweli hapa ni kwamba, Tabia yako, fikira zako na imani yako ni sehemu muhimu zinazotoa mwelekeo na kiwango cha mafanikio yako. Kumbuka kuwa, kitu pekee kinachozuia mafanikio yako SIO kitu ambacho hukijui, rahasha, kikwazo pekee cha mafanikio yako ni kile kitu ambacho unakijua kwa njia isiyo sahihi.
Eker, anasema kuwa, moja ya kanuni ya utajiri ni kwamba, KIPATO CHAKO KINAWEZA KUKUA NA KUONGEZEKA KUTOKANA NA JITIHADA UNAZOCHUKUA.
ulishawahi kuona watu ambao walikuwa na pesa nyingi sana lakini baadae zikawatoka? Hii ndio sababu ya kwamba, ukipata pesa nyingi na ukawa haujajitayarisha ndani yako (mwongozo wa ndani), pesa zitaishi kwako kwa muda mfupi na kutoweka kabisa.
Na hii ni kwasabu, watu wengi hawana uwezo wa ndani wa kutengeneza na kumiliki pesa nyingi ndio maana haziji kabisa au zinakuja na kuwakimbia. Mfano halisi, ni wale wanaoshinda michezo ya kubahatisha au wale wanaopata pesa nyingi kwa ghafla machimboni kwenye migodi ya madini.
Mara baada ya kuipata, pesa huwa inawakimbia na hatimaye kurudi kwenye kiwango chao cha pesa wanachoweza kumiliki kutokana na uwezo wao wa ndani. " Internal Comfort zone"
#Jambo pekee la kujifunza hapa ni kwamba, MIZIZI NDIO INATENGENEZA MATUNDA.
Chukulia kwa mfano, mti huu unasimama kwa niamba ya mti wa maisha na kwenye mti huu kuna matunda. Kwenye maisha matunda yetu ni matokeo yetu. Kwahiyo tukiangalia matunda (matokeo yetu), ikiwa hatuyapendi, hayajitoshelezi, mabaya, madogo sana na hayana radha.
Kwahiyo tufanyeje? Wengi wetu tutaangalia zaidi matunda (matokeo yetu). Lakini ukweli ni kwamba, tunahitaji kujiuliza zaidi juu ya kitu gani kimeyatengeneza hayo matunda (matokeo)? Jibu ni kwamba, ni mbegu na mizizi ndio inatengeza matunda (matokeo).
#Eker anasema, ni kile kitu ambacho kiko chini ndicho kinatengeneza kile kitu kinachoonekana juu ya ardhi, ni kitu ambacho hakionekani ndicho kinaunda kitu ambacho kinaonekana.
Somo pekee la kujifunza kwenye EPISODE#1. Ni kwamba, ikiwa unataka kubadilisha kipato chako lazima ubadilishe kazi au uboreshe mazingira ya kazi yako, karibisha fikira, elimu, ujuzi, maarifa, uzoefu, ufahamu, mawazo, mtazamo, hisia, imani na matendo mapya.
MWISHO wa EPISODE#1
"You cannot change the fruits that are already hanging on the tree. You can, however, change tomorrow's fruits. But to do so, you will have to dig below the ground and strengthen the roots"
______________________________________
#kama umependezwa zaidi na makala hii, niandikie "comments" hapo chini, PIA kumbuka " kulike" na "kushare" na wengine ili wajifunze zaidi na kufuatilia " EPISODES" zinazofuata.
Lakini pia, kumbuka "kunifollow" Facebook, Twitter na Instagram kwa majina ya: Leonard Julius. Ili tujifunze zaidi kwa pamoja.
#THINKANDTAKESTEPS
shiganga@gmail.com