EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Alhamisi ya Februari 6, 2015, Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ilianza kusikiliza kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Pacificus Cleofas Simon mwenye namba G 2573.
Kwa wale watu wa matukio ambao walishasahau kilichotokea, Mwangosi aliuawa Septemba 2, mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kazi wakati Chadema wanakiandaa kwa ajili ya kufanya maandamano na mkutano mkubwa pamoja na kufungua tawi la chama hicho.
Katika mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Sunday Hyre, anadai kuwa Septemba 2, mwaka 2012, mtuhumiwa (Pacificus Cleofas Simon) alimuua Mwangosi kwa kumpiga kwa bomu kwa makusudi. Hata hivyo, mtuhumiwa amekana shitaka hilo. Mtuhumiwa anatetewa na Wakili Rwezaula Kaijage. Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Jaji Paulo Kihwelo.
Wiki iliyopita Kihwelo aliamuru upande wa utetezi kupokea kielelezo cha gazeti la Septemba 3, mwaka 2012 kama utambuzi wa awali ili kusaidia ushahidi wa keshi hiyo. Jaji Kihwelo alisema kuwa kielelezo hicho ni muhimu kwa sababu kitasaidia kutumika katika ushahidi wa kesi hiyo ya mauaji ya Mwangosi.
Hapa tutakuwa tunaweka updates za kesi hiyo mpaka hukumu itakapotolewa.
PIA SOMA
- TANZIA - Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA