Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

TIMU GANI ITAKUWA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA(Vodacom Premier League)


  • Total voters
    72
  • Poll closed .
Du Kandambili mwaka wa Shetani huu, Mnyama Kesho jamani LoL!
labda Manji hakuwa ahidi chochote au ni game lilikuwa tight maana Azam FC hawafai hasa yule mfungaji wao John Boko aka Adebayo kila gemu lazima aingie nyavuni gemu nane magoli 8, kama hatalewa sifa atakuwa tegemeo la Taifa..
 
Jamani leo vipi mbona kimya maana JKT wapiga kwata leo wanajaribu kumuua mnyama..?
 
...Nina mashaka na haya matokeo according to dullonet ?

Dullo wanachanganya sana,yale mpaka ya 1-1 yalikuwa sahihi.Haya ya 4-1 ghafla ndo yanaleta utata.Lakini nina uhakika muda si mrefu Dullo mwenyewe atayaleta matokeo ya ukweli
 
Nilikuwepo uwanjani. Simba wanatisha! Matokeo ya mwisho ni SIMBA 4 JKT RUVU 1. Wafungaji wa magoli ya Simba ni UHURU SELEMANI, EMMANUEL OKWI, RAMADHANI CHOMBO REDONDO na MUSSA HASSAN MGOSI. Yule aliyeifungia JKT Ruvu simjui.
 
Kwa Simba niliyoiona leo kama Yanga watatia mguu tarehe 31 Oktoba, lazima wanywe! Kocha wao mpya kutoka Serbia alikuwepo uwanjani na alikuwa anashangilia mabao ya Simba. Ila aliondoka kabla mchezo haujaisha na kusababisha kuzomewa na wana-Simba.
 
shukran mkuu, kule dullonet kumejaa manazi wa Yanga. Nilishagundua ni uongo ila sikuwa na uhakika lakini kelele za simba sugu wakati cimu inakatika katika nilihisi tumewabanjua hawa jamaa...

Okwi is only 17, na ana future nzuri sana. Ndiyo maana sisi wengine tunakubali kuchangia pesa kila siku through FOS, usajili huu ni mzuri sana, na wa kitaalam zaidi. Kwa age factor na quality, mwaka huu tutafanya maajabu makubwa..!

YY wamekuwa wakitoa pesa ili tufungwe lakini wananshindwa kulipa madeni ya timu yao. KIla mechi, tunacheza na timu zaidi ya 5..! YY lazima bakora zitembee, maana hata marefa wakitoka ikulu lazima wachapwe tu. Timu hii imejengwa kisaikolojia na kimpira, na morali ipo juu sana.
 
Dullo wanachanganya sana,yale mpaka ya 1-1 yalikuwa sahihi.Haya ya 4-1 ghafla ndo yanaleta utata.Lakini nina uhakika muda si mrefu Dullo mwenyewe atayaleta matokeo ya ukweli

Hata hayo ya 1-1 hayakuwa sahihi mkuu Simba walipiga Mbili ndani ya dakika mbili mkuu, Ruvu hawakusawazisha katika mtanage wa leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom