Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

TIMU GANI ITAKUWA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA(Vodacom Premier League)


  • Total voters
    72
  • Poll closed .
Mpira umekwisha simba imefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu na goli moja lililofungwa dakika ya 24 kwa shuti ilililopigwa na Echesa nakumaliziwa na beki wa Azam kwa bahati mbaya, ilikuwa mechi ngumu sana. sasa tuna msubilia Yebo Yebo... Maji Maji 1 Africa Lyon 1...

Kweli mnyama mwaka huu atamaliza wanyama wote polini
 
Hongera Azam FC kuwa na tovuti tena anayokuwa updated mara kwa mara. Club kubwa na kongwe kama Simba na Yanga zimeshindwa kuwa na tovuti licha ya kuwa na uwezo wa kuajiri waamuzi wa kimataifa na kusajili wachezaji wa kimataifa. Uswahili ndo umetawala.

Kwakweli hata mimi nawapa hongera sana Azam FC, hii miklabu yetu miwili mikubwa inatia aibu, kila kitu ni dili mpaka wanashindwa kuleta maendeleo ya kweli
 
kwanza nawapongeza kwa kuwa na tovuti yao ni timu ambayo inaonyesha inamipango ya kueleweka... kwenye tovuti yao wamesema hivi "Simba leo jioni imepata ushindi wa bahati wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Azam FC lakini wachezaji wa Simba watalazimika kulala na viatu baada ya kucheshwa samba na vijana mahiri wa Azam Fc" kama walivyofanya walipocheza na Yanga leo tena Azam FC wameonesha kandanda la hali ya juu na kuwafunika kabisa Simba licha ya kupata ushindi wa goli ambalo Azam FC walijifunga wenyewe"... yote kwa yote mpira ni magoli wajitahidi mwakani labda watapata sare..ila niwang'ate sikio Mnyama anatisha..

>Maji Maji 2 - Africa Lyon 1
 
nilikua nikishangaa sana eti watu wakati ule wanapinga Yanga kuwa kampuni, wakati ni jambo la kisasa kabisa...eti yanga asili, ulikua ni ujinga sana.
 
nilikua nikishangaa sana eti watu wakati ule wanapinga Yanga kuwa kampuni, wakati ni jambo la kisasa kabisa...eti yanga asili, ulikua ni ujinga sana.
Yanga Asili ilikuwa rahisi sana kuiibia timu hasa pesa ya getini, ndiyo maana akina Mzimba na wanzake walikataa kabisa Yanga kuwa kampuni ampaka alipopewa pesa Manji na JK na kuanza kuzunguka Tanzania nzima kuonyesha umoja!? baada ya kupata chake nasikia alipata mtaji wa kupasua mbao... lakini Yanga kama kampuni wanafanya biashara gani pale maana hata bamia huwa sizioni au wako kwenye mchakato, walisema watauza hisa sijawasikia tena au nikimya kimya...
 
ah tim zetu utaziweza, ila Simba na Yanga ni vizuri wawe kampuni...na Azam wakiendelea hivi Simba na Yanga watapotea shauriao..maana mpira these days pesa na ubunifu mzuri wa maendeleo katika mpira...administratn ikiwa Mbov mpira hauendelei.
Yanga na simba wabadilike waende kwa mfumo wa kisasa na si kutegemea mara friends of Simba, mara Manji...wakiacha au wakipunguza tu ufadhili basi tim hai perform
 
Jamani leo vipi mbona kama kumenuna ??

Wakata miwa lazima waachie point au?
 
Ala kumbe ligi inaendelea mimi nilifikiri tushatwaa Ubingwa
 
hahahahaahha bado mkuu, watani vipi mbona kimyaaaaa?
 
Hahahaaa, we acha tu, sa hii watu wanafukua maiti huko kuroga mechi za raundi ya pili!!!

Leo Simba na Mtibwa sijui matokeo huko vipi?

Hata Sielewi mkuu, ngoja tuvute mkuu Mafuluto na Mastau nadhani soon watakuja na Data
 
ligi ya darts ndo huwa inaamuliwa kwa mechi chache hivyo...
Msikurupuke waungwana...
Kwanza ingekuwa jambo la kheri mngejichangisha ili mpake rangi jengo lenu.
 
ligi ya darts ndo huwa inaamuliwa kwa mechi chache hivyo...
Msikurupuke waungwana...
Kwanza ingekuwa jambo la kheri mngejichangisha ili mpake rangi jengo lenu.

Haya mkuu, hivi si ndio wewe ulikuja na tule tutakwimu twako twa yanga na mnyama kabla ya ile mechi??

Simba bingwa, kama hutaki basi!!
 
Back
Top Bottom