Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

TIMU GANI ITAKUWA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA(Vodacom Premier League)


  • Total voters
    72
  • Poll closed .
Kwa matokeo hayo, Azam Fc imejihakikishia kukaa either nafasi ya kwanza au ya pili(itategemea na Yanga) kwani Mbeya city haiwezi kuzifikia points za Azam, ni Yanga pekee ndiyo inauwezo wa kuzifikia points za Azam.
 
Azam anatoa sare michezo yote iliyobakia, na Yanga anashinda michezo yote iliyobakia,na kuutangaza ubingwa.....
 
MATOKEO LIGI KUU VODACOM:

Yanga 5-1 JKT Ruvu,


Mgambo 2-0 Coastal Union,


JKT Oljoro 2-1 Prisons.
===============================
Leo ni KUFA au KUPONA:

JKT RUVU 1-5 YANGA, (FT)
UWANJA WA TAIFA.


COASTAL UNION Vs MGAMBO, Mkwakwani, Tanga.


JKT Oljoro dhidi ya Tanzania PRISONS,
pale Sheikh Amri Abeid, Arusha.


Rhino Rangers watawakaribisha Mtibwa Sugar, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora...


Karibuni Wadau wote, kutupia hapa janvini taarifa na UPDATES toka viwanja mbalimbali...
 
YANGA SC wanatarajia kukabiliana na maafande wa JKT Ruvu katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Viingilio katika mechi hiyo ni kama ifautavyo; VPA Tshs 20,000/=,VIP B na C ni Tshs 15,000/=, huku viti vya rangi ya Chungwa, Bluu na Kijani ni Tshs 5,000/=
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kwani kushinda kutawafanya waendeleze uhakika wa kutetea ubingwa wao msimu huu.
Mpaka sasa Yanga wao nafasi ya pili kwa pointi 46 baada ya kushuka dimbani mara 22.
Mbele yao wapo Azam fc wenye pointi 53, huku wakiwa wameitangulia Yanga kwa mchezo mmoja.
Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na machungu ya kufungwa mabao 2-1 mechi iliyopita dhidi ya Mgambo JKT katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
JKT Ruvu wapo nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 23 na kujikusanyia pointi 28 kibindoni.
Kama watashinda leo watazidi kujiweka mazingira mazuri zaidi ya kubakika ligi kuu.
Hivyo kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro ataingia kwa lengo moja la kuifunga Yanga ambayo ameifundisha kwa muda mrefu akiwa kocha msaidizi na wakati fulani kukaimu nafasi ya kocha mkuu .
Mchezo wa leo unaweza kuwa na changamoto kubwa kwa timu zote, lakini timu itakayokuwa na mipango mizuri itaweza kushinda.
Kocha mkuu wa Yanga, Mhalonzi, Hans Van Der Pluijm anaweza kuwaanzisha mlinda mlango Deogratius Munish `Dida`kwasababu yuko fiti baada ya kupona majeraha yake yaliyokuwa yanamsumbua kwa takribani wiki tatu.
Beki ya kulia anaweza kuanza Juma Abdul, kushoto, Oscar Joshua.
Mabeki wa kati bila shaka watasimama, Mbuyu Twite na `Nadir Haroub Canavaro`.
Twite anaweza kulazimika kucheza beki ya kati kwasababu Kelvin Yondani anatumia kadi mbili za njano.
Frank Domayo `Chumvi` anaweza kuanzishwa nafasi ya kiungo wa ulinzi, huku Saimon Msuva akianza winga ya kulia.
Kiungo namba nane anaweza kusimama kinda, Hassan Dilunga, huku namba tisa akianza Didier Kavumbagu.
Kiungo mshambuliaji anaweza kuanza Hamisi Kiiza, wakati winga wa kushoto leo hii anaweza kusimama Mrisho Halfan Ngasa.
Pluijm leo hii atakosa huduma ya Athuman Idd `Chuji`, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi na Kelvin Yondani wenye matatizo tofauti.
Kikosi kilichotajwa hapo juu si rasmi, bali ni utabiri tu kulingana na umuhimu wa mechi yenyewe na wachezaji waliopo tayari kucheza kipute hiki.
Lakini kuna wachezaji wengi wanaoweza kuanzishwa wakiwemo akina Jerryson Tegete na Hussein Javu kwa safu ya ushambuliaji.
Maeneo mengine pia wapo wachezaji wengine wanaoweza kuanza kutegemeana na uchaguzi wa kocha mkuu, Hans Van Der Pluijm, kwasababu wote wana uwezo mzuri.
Mechi nyingine za jioni ya leo ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mgambo uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Vibonde JKT Oljoro watakuwa na kibarua muhimu na maafande wa jeshi la Magereza kutoka jijini Mbeya, Tanzania Prisons `Wajelajela` katika dimba la Shk. Amri Kaluta Abeid jijini Arusha.
Rhino Ranger waliopoteza matumaini ya kubakia ligi kuu watawakaribisha, Mtibwa Sugar kutoka Marogoro kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mechi ya Ruvu Shooting na Azam iliyotakiwa kupigwa leo imesogezwa mbele mpaka aprili 9 mwaka huu kwasababu wachezaji wengi wa Azam fc wameondoka na kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.


by: SD
 
RATIBA: "LALA SALAMA"

06/04/14
VPL: COASTAL UNION Vs MGAMBO SHOOTING, Mkwakwani


VPL: JKT OLJORO Vs T.PRISONS, Sh. Amri Abeid


VPL: RHINO Vs MTIBWA SUGAR, A.H Mwinyi


VPL: RUVU SHOOTING Vs AZAM FC, Mabatini


VPL: YANGA Vs JKT RUVU, U/Taifa
09/04/14


VPL: YANGA Vs KAGERA SUGAR, U/Taifa


12/04/14
VPL: MTIBWA SUGAR Vs RUVU SHOOTING, Mabatini


VPL: COASTAL UNION Vs JKT RUVU, Mkwakwani


VPL: PRISONS Vs RHINO, Sokoine


13/04/14
VPL: MGAMBO Vs KAGERA SUGAR, Mkwakwani


VPL: SIMBA SC Vs ASHANTI, U/Taifa


VPL: MBEYA CITY Vs AZAM FC, Sokoine


VPL: OLJORO JKT Vs YANGA, Sh. Amri Abeid


19/04/14
VPL: RHINO RANGERS Vs RUVU SHOOTINGS, A.H Mwinyi


VPL: MBEYA CITY Vs MGAMBO JKT, Sokoine


VPL: TANZANIA PRISONS Vs ASHANTI UNITED, Jamhuri


VPL: JKT RUVU Vs AZAM FC, U/Azam


VPL: JKT OLJORO Vs MTIBWA SUGAR, SH. Amr Abeid


VPL: COASTAL UNION Vs KAGERA SUGAR, Mkwakwani


VPL: YANGA Vs SIMBA SC, U/Taifa
 
Tuko pamoja kamanda japo wadau wa yanga hawaonekani sijui tatizo gani limewakumba.
 
Nimetoka kuongea na wachezaji wa jkt ruvu wamenambia kandambili hawatoki leo!
 
Back
Top Bottom