Updates - Pres. Obama in Tanzania July 01-02, 2013

Updates - Pres. Obama in Tanzania July 01-02, 2013

Mbona akija Zuma wa South hamna shamra shamra na mapambo kama haya ya huyu jamaa wa US?
Au South Africa hakuna cha kufaudu Tanzania
 
Huenda tukawa masikini zaidi kuliko alivyotukuta

unajua miradi inayoendeshwa kwa pesa za wamarekani hapa tz? unajua wanatupa kiasi gani kwenye malengo ya milenia?
au hesabu yako iko kwenye elfu 10 watakazopewa kila mcheza ngoma au hivyo vimizinga ambayo vimelipuliwa kwa heshima obama? ulitaka iendelee kukaa tu ili ilipuke yenyewe?au akina kikwete kumngoja air port hushangai kikwete kukimbiza na misiba ya wasanii underground hata wasio kuwa na majina siku nzima kwani hana kazi ikulu?

Taifa ili linahitaji wawekezaji ndio wamekuja, KIKUBWA ULICHOTAKIWA KUCHANGIA NI KUWA VIONGOZI WAWE MAKINI KATIKA MAKUBALINO YA KIBIASHARA
 
Ee bwana ikulu imependeza sana imepambwa na bendera za Marekani na Tanzania.
 
Picha plzzzzz! Wadau!

MMG25097.jpg


MMG25118.jpg
 
mbona hakuna wanaume hapo? hayo majimama yamekodishwa nini? mane wanaonekana shughuli wanaiweza.
 
Hawa wapga drums kuna kpnd km walkua wanapga midundo ya joto hasira au maskio yangu tu
 
Hakuna kitu kama hicho bana.

Air Force One ina uwezo wa kukaa angani kwa wiki siku kadhaa tu.

Hiyo niliona kwenye Discovery Channel.

jamaa wametulisha sana chai aisee! si wasom e hata huku JF kuna thread kibao za ulinzi wa raisi wa marekani
 
najaribu kupiga picha inaonekana picha hazitoki wamezuia kamera na mitambo hatari sana hawa jamaa...kamera hazifanyi kazi kabisa aiseee
 
Kha ha ha ha ha haaaaaaa!
Tupe newz zaidi unayoiona!

Hata picha ikiwezekana Mkubwa!

Ila kiukweli nimegundua hisia hazizuiliki ha!!nimejikutaje nimetoka ofisini na kwenda kusimama
barabarani Nyerere rd loh,migari yenyewe imepita speed halafu hata huwezi jua lipi kapanda Obama
nilichoambulia ni kuona tu magari yao ah'
 
Watangazaji wa TBC wamenichefua sana, eti wana usalama wamevaa miwani zinazoonesha pande zote nne!!! Mara jiji lote la dar lipo kwenye msafara wa obama.. sikuelewa anaamanisha nini.. jamaa wameleta stori zile za kwenye vibanda umiza vya kuangalia video mtaani.. so pathetic!
Ka Vitz kangu kana GPRS ya East Africa na Japan.
 
lini utaacha ukabila mkuu?
aaah jamani!!yan mtu kusifia traditional dance ya kwao nao ni ukabila?!serious mwana jf.?!!!.i insist BIG UP TO WANYASA kwa ngoma ya mganda.LOL
 
mbona mama salma haonekani au? hahaa ananoa kingereza wama kwa ajili ya kesho ...mhh sijui itakuwaje michelle na ngeli yako ya kumung'unya utamfanya mama yetu apaliwe
 
Mbona akija Zuma wa South hamna shamra shamra na mapambo kama haya ya huyu jamaa wa US? Au South Africa hakuna cha kufaudu Tanzania
Huyo n raisi wa afrika kusini,huyu ni rais wa dunia nzma,upo? Lazma tz tumlambepo
 
jamaa wametulisha sana chai aisee! si wasom e hata huku JF kuna thread kibao za ulinzi wa raisi wa marekani


Mkubwa Mi kilichonishangaza ni kama ni kweli huyu mshua anaweza kubadili usafiri angani hakika wadau wako juu!
 
Urafiki wa muda mrefu uliopo kati ya tanzania na marekani, fursa za uwekezaji na kukua kwa demokrasia na utawala bora ni sababu kubwa zilizomfanya hussein obama kuja tanzania hii ni sifa kubwa kwa mh raisi kikwete.
 
Back
Top Bottom