Updates from Kilosa district(taarifa kutoka wilayani Kilosa)

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,543
2,000
Habari ndgu jamaa na marafiki na hasa hasa wale ndugu zangu mliozaliwa au mliowahi kuishi wilayani Kilosa,iliyopo katika mkoa wa Morogoro. Najua si wote mliozaliwa kilosa mmefanikiwa kuishi, wapo wengi ambao ni wazaliwa wa wilaya hiyo lakini mko mbali na wilaya hiyo.

Hiyo inatokana na sababu kadhaa zikiwemo zile za kujitafutia ridhiki aka maisha. Pamoja na hayo kuna wakati unapenda sana kufahamu nini kinachoendelea huko kilosa, lakini huna njia ya kupata habari za huko.

Kutokana na jambo hilo, nimeona si mbaya kama tutatumia njia hii(thread hii), kwa ajili ya kupashana habari. Tuomba yeyote mwenye taarifa ya aina yoyote ile iwe ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, sherehe,msiba, ajali,majanga yanayohusu wilaya kilosa awe tayari kutufahamisha. Kwa kutumia njia hii wana kilosa wataweza kufahamu kinachoendelea huko wilayani Kilosa.

Kwa kuanzia naomba niwataarifu kuwa Hiza wa Senkubo(Abdallah Dogo) amefariki dunia juzi. Mazishi yake yanategemewa kufanyika mchana huku kilosa. Kifo cha marehemu Hiza kimesababishwa na ajali ya gari iliyotokea maeneo ya bwawani nje kidogo ya mji wa Morogoro. Inallillah wa innallillah rrajun.

Wengingine katika ajali hiyo ni Sultan(mdogo wake na Fadhiri). Yeye inasemekana amevunjika mbavu mbili na amepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa matababu zaidi. Wote walikuwa ni watumishi wa Tanzania investment Bank ya jijini DSM
 
Sometimes

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
4,546
1,500
Sina uhakika na wale waathirika wa mafuriko walioahidiwa kujengewa nyumba na Gaddafi wametekelezewa! Ni suala la kulifuatilia.
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,543
2,000
Sina uhakika na wale waathirika wa mafuriko walioahidiwa kujengewa nyumba na Gaddafi wametekelezewa! Ni suala la kulifuatilia.

Yeap, ni kweli. Ahadi ile ilkuwa wazi, matokeo yake hatujui iliishia wapi. Ni suala la kufuatilia ilimtujue hatma ya ahadi zile
 
Mr. Mwalu

JF-Expert Member
Feb 4, 2010
1,057
1,500
rest in peace QS hiza senkubo! alumni wa mzumbe 1990- 1997, uclas BE 1998 - 2002!!
 
Gedeli

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
497
250
nilisoma hapo kilosa miaka ya sabini katika shule moja ilikuwa ikiitwa Mazinyungu mwalimu kuu alikuwa akiitwa Mzee kilosa Je hii shule bado iko au ilishapandishwa daraja ???
 
Slow pancha

Senior Member
Mar 16, 2013
182
225
Dah!mwenyezi mungu ailaze pema roho yake.hrf niliwahi kusikia yule bwana ni mdg wake mahita.najua pia kuwa babylon hatokosa kumzika bosi wake wa zamani
 
Septemba11

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
611
1,000
Nlizaliwa kimamba palem hiyo ajali ya juzu Bwawan niliiona ila sikuwa nawafahamu hao wahanga, pia asahv Gairo imejitenga toka Kilosa ni wilaya mpya sasa
 
Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Nimfurah sana kukuta uzi kama huu,mi ni mwana Kilosa,nimesoma Mkondoa Promary 1989-1995,nna miaka mingi sana sijafika kilosa,juz nilipata taarifa za msiba wa Mtoto wa Abdallah Dogo kwa sms ,sijui ile namba ni ya nani,ila mdau Kilosa ni Miongon mwa wilaya Kongwe,ila wilaya iliyochoka sana,hivi naomba uniambie maana inaonesha kwa sasa upo Kilosa,hivi baraza la madiwan na mbunge (Mzee Mkulo) kweli wana mipango ya maendeleo kuhusu Kilosa,vile vile CAG kwa miaka kadhaa (sijui mwaka huu) huwa anaipa hati chafu wilaya yetu,,,kuna picha zilirushwa mitandaon zikionesha uwekaj wa lami barabara iendayo Bomani,hivi wazo hilo alitoa nani???na pia kilosa ni wailaya inayotoa vijana wengi wasomiwasomi,ila wapo nje ya wilaya ya kilosa nadhan si mbaya ukaanzishwa mtandao wa vijana wa kilosa walio nje ya wilaya ya Kilosa,napamiss kilosa,naimis mkwatani,Miombo(nilikua nakata mkaa),mto mkondoa nilikua naoga na kula miwa,muhomwa where i was living na kuangua maembe,kisak nilikua nalima na mama yangu na baba yangu (rip),kichangani nilikua nasoma tuition ya mwalim maringo(rip),mtenden nilikua naenda kununua kambale wa mboga usiku,hospital ambako nilipata huduma za afya kwa utoto wangu wote,magomen kule Lamlilo tulikua tunaenda kwenye michezo,uwanja wa azimio,uwanja wa ,mazinyungu,naikumbuka mkono wa mara ambako nilisoma 1 year,naskitika shule yangu Mkondoa ilizolewa na maji na haikujengwa tena,huenda BRN itaijenga
'KILOSA KWETU'
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,543
2,000
nilisoma hapo kilosa miaka ya sabini katika shule moja ilikuwa ikiitwa Mazinyungu mwalimu kuu alikuwa akiitwa Mzee kilosa Je hii shule bado iko au ilishapandishwa daraja ???

Lazima itakuwa mazinyungu primary. Yeap bado ipo. Isipokuwa kuna shule nyingine ya sekondari ya kutwa imeanzishwa palepale kiilosa inaitwa Mazinyungu pia. So we have Mazinyungu Secondary School pia. Unapaswa kutembelea shule yako ilimupate radha ya ulikopitia.
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,543
2,000
Nlizaliwa kimamba palem hiyo ajali ya juzu Bwawan niliiona ila sikuwa nawafahamu hao wahanga, pia asahv Gairo imejitenga toka Kilosa ni wilaya mpya sasa

Yeap, imesaidia sana kusogeza huduma kwa wananchi, ingawa bado wana changamoto kadhaa. Naamini mbunge wa gairo mh shabibu anaweza zitafutia suluhisho iwapo atashirikiana vyema na wananchi wake
 
Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Habari ndgu jamaa na marafiki na hasa hasa wale ndugu zangu mliozaliwa au mliowahi kuishi wilayani Kilosa,iliyopo katika mkoa wa Morogoro. Najua si wote mliozaliwa kilosa mmefanikiwa kuishi, wapo wengi ambao ni wazaliwa wa wilaya hiyo lakini mko mbali na wilaya hiyo.

Hiyo inatokana na sababu kadhaa zikiwemo zile za kujitafutia ridhiki aka maisha. Pamoja na hayo kuna wakati unapenda sana kufahamu nini kinachoendelea huko kilosa, lakini huna njia ya kupata habari za huko.

Kutokana na jambo hilo, nimeona si mbaya kama tutatumia njia hii(thread hii), kwa ajili ya kupashana habari. Tuomba yeyote mwenye taarifa ya aina yoyote ile iwe ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, sherehe,msiba, ajali,majanga yanayohusu wilaya kilosa awe tayari kutufahamisha. Kwa kutumia njia hii wana kilosa wataweza kufahamu kinachoendelea huko wilayani Kilosa.

Kwa kuanzia naomba niwataarifu kuwa Hiza wa Senkubo(Abdallah Dogo) amefariki dunia juzi. Mazishi yake yanategemewa kufanyika mchana huku kilosa. Kifo cha marehemu Hiza kimesababishwa na ajali ya gari iliyotokea maeneo ya bwawani nje kidogo ya mji wa Morogoro. Inallillah wa innallillah rrajun.

Wengingine katika ajali hiyo ni Sultan(mdogo wake na Fadhiri). Yeye inasemekana amevunjika mbavu mbili na amepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa matababu zaidi. Wote walikuwa ni watumishi wa Tanzania investment Bank ya jijini DSM

Chiwaso umefanya jambo la maana sana mdau,,,,,shukran sana,Kwa Abdallah Dogo napakumbuka bhana,usiku ukipita unakua na wasiwasi kulikua na mbwa pale wakali,ila kupitia uzi huu ntakutna na watu wengi nilopotezana nao kwa miaka mingi sana,najihis nipo Kilosaa kwa uzi huu,in shaa Allah mwaka huu ntazuru Kilosa kabla haujaisha,
 
Last edited by a moderator:

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Yeap, imesaidia sana kusogeza huduma kwa wananchi, ingawa bado wana changamoto kadhaa. Naamini mbunge wa gairo mh shabibu anaweza zitafutia suluhisho iwapo atashirikiana vyema na wananchi wake

Mbunge wa Kilosa hazion changamoto eeenh???,
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,543
2,000
nilipata kuskia bado wanakaa makambin (baadhi yao)

Labda tutapata majibu ya mheshimiwa mbunge(mr mustafa mkullo). Mheshimiwa kama ukiiona hii thread tunaombaa majibu yako, na hasa ikizingiwa kuwa mwaka 2015 ni mwaka wa uchaguzi
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,543
2,000
Chiwaso umefanya jambo la maana sana mdau,,,,,shukran sana,Kwa Abdallah Dogo napakumbuka bhana,usiku ukipita unakua na wasiwasi kulikua na mbwa pale wakali,ila kupitia uzi huu ntakutna na watu wengi nilopotezana nao kwa miaka mingi sana,najihis nipo Kilosaa kwa uzi huu,in shaa Allah mwaka huu ntazuru Kilosa kabla haujaisha,

Ni pale karibu na kwa akina Pocho, si mbali sana na tingetingeni. Mkuu usiku huo ulikuwa unatokea wapi tena? Teh teh teh
 
Last edited by a moderator:

Tuvulile

Member
Apr 24, 2013
42
70
Nilishawahi kufanya kazi ktk wilaya yenu ya Kilosa,. Kiukweli maendeleo pale mtasubiri sana coz.....
1. Uchawi
2. Wazee wenu waliweka network za kuwapa nyadhifa nyeti sana watoto wao ambao hawajaenda hata shule. Hivyo wenye shule vigezo/taaluma wakija hapo wanapigwa majungu, wakikomaa wanarogwa. Hii imefanya pale bomani pawe kama mto wenye kambale, huwezi jua baba, mama, mtoto ni yupi.
Mfano tu!... zile kokoto zilizowekwa pale bomani na kule hospitali inadaiwa zimegharimu zaidi ya 300M.

Ushauri;. Washaurini wazee wenu wawatoe watoto wao wasokua na sifa kwenye vitengo mbalimbali pale.
 
ua ryt mdau,,,,any way ndo changamoto za Kilosa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom