Updates from Kilosa district(taarifa kutoka wilayani Kilosa)

MTU kwao bwana ,dah nimeimisi Kilosa ,VP hali ya mjini Kwa sasa baada ya mafuriko? Nitatia timu june
 
Wapi Gheto, Yetu Afrika, Mazulia, Taro, Msimba, Kikoboba, Mamoyo rangers, Kanseli(KDC), Magomeni stars, Kilosa Estate,nk.
 
Copy from fb group...Kilosa Kwetu.....>Kilosa KwetuWanakilosa Mnakera Kinoma Mnalike Na Kukoment Mambo Ambayo Hayanafaida Ktk Maendeleo Ya Wilaya Yetu,,,kwa Sasa Kilosa Kuna Tatizo La Misingi(miferej).. Misingi Imejaa Maji Tena Kuna Samaki Ana Watu Wana Vua Tena Kwa Kumwaga Dawa(kitupa) Kumbukuken Kuwa Baada Ya Kuvua Samaki Kuna Wadudu Na Baadh Ya Samaki Watakao Kufa, Husababisha Harufu Kari Katika Mitaa Na Hata Magonjwa Ya Miripuko Je Mmejiandaaje Na Magonjwa Ya Mripuko? Mnamkakati Gani Na Hiyo Mifereji?? Hali Hii Inawakumba Wakazi Wa Mjn(mbumi) Wadau Hebu Tuwasaidie Hao Wakaz Wahayo Maeneo Maana Wanahis Kama Ni Neema Kwao Lkn Hajui Kama Kuna Madhara Baadae... Nice Day
 
Nina mpango wa kuishi KILOSA naomba msaada wa kufahamishwa mazingira halisi ya hii wilaya.

1 Shughuri kubwa za kiuchumi ni zipi?
2 Gharama za vyumba vya kupanga, viwanja na mashamba.
3 Hali ya hewa
4 Miundo mbinu hasa ya maji, shule na umeme.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Hamzah J,

Wilayani Kilosa shughuli kubwa ni Kilimo na Biashara. Mazao makuu ya chakula ni Mahindi na Mpunga na mazao ya Biashara ni Ufuta, Alizeti na Mbaazi. Aidha, kuna kilimo cha vitunguu maeneo ya Lumuma na Viazi vitamu hasa maeneo ya Gairo.

Ardhi ya Kilosa imejaaliwa kuwa na rutba ya kutosha kwa kilimo hasa maeneo ya Kivungu, Mateteni, Zombo, Ulaya, Ilonga, Lumuma, Tindiga, Kidete kwa mazao ya Mpunga, Mahindi, Alizeti, Ufuta, Mbaazi na Vitunguu.

Upatikanaji wa mashamba ni kwa njia ya kukodi, na unaweza pia kununua japo population inaongezeka na kuongeza competition ya resource hiyo.

Viwanja:
Gharama za viwanja zinapanda kwa kasi kulingana na ukuaji wa mji. Athari ya mafuriko imefanya viwanja viwe ghari sana hasa maeneo ya Manzese na Mtendeni. Pia gharama za vyumba inategemea na ubora wa nyumba husika na eneo iliyoko. Lakini kwa ujumla bei ya pango ni reasonable na ni affordable.

Miundombinu:
Kuna mradi mkubwa wa maji tayari ulikwishafanyika kwa kutandaza mabomba kwa Kilosa mjini na viunga vyake hasa Manzese yote. Kukamilika kwake kutapunguza kero ya maji kwa kiasi kikubwa.

Aidha, maeneo mengine yaliyosalia hayana uhaba wa maji hata kidogo, isipokuwa asilimia kubwa ni maji ya bomba na visima.

Shule zipo za kutosha, kila kata ina shule ya sekondari na shule za msingi zisizopungua nne.

Hali ya hewa;
Ni kama tu ilivyo mikoa mingine ya Pwani, hali ya hewa ni joto tu la kawaida hufikia hadi juzijoto 32 kwa nyakati za joto (Oktoba hadi April) na kipindi kifupi cha baridi kuanzia May hadi July. Huhitaji jackets wala sweaters ndani ya Kilosa.

Umeme:
Hii bado ni changamoto kwa maeneo ya nje ya mji kama Zombo, Tindiga, Ulaya, Mhenda. Lakini huwenda mpango wa umeme vijijini (REA) ukafanya umeme kufika maeneo hayo.

Kwa upande wa barabara kwa ujumla hakuna barabara ya lami. Zilizopo ni za changarawe na zinapitika nyakati zote bila tatizo. Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami bado unaendelea na sasa imefikia Ludewa kuelekea Kilosa Mjini.

Natumai nitakuwa nimekupa mwanga kidogo japo mimi kwa sasa sipo Kilosa ila ni mzaliwa wa huko na ndio kwetu.

Karibu sana Kilosa.
 
Hongera Chiwaso,wengi wazaliwa wa hapo,nami miaka ya 80 nilikuwa nikiishi kule nguzo sita kwa binti Konyaki, baadaye tuliamia hapo jirani na uwanja wa Jamuhuri ni mtoto wa armaarufu Mzee Shombe(r.i.p) Wilaya yetu,ni ya miaka mingi mno imedumaa sana wakati wilaya nyingine zimishapandishwa adhi!Wana Kls kwa sasa napatikana kanda ya Ziwa kwa masuala ya uvuvi na madini(dhahabu)nione nitakupokea.Hapo mtendeni nimepotezana na mwanangu wa kiume, si unajua tena mambo ya ujana, tuwasiliane 0789554955.
 
Hongera Chiwaso,wengi wazaliwa wa hapo,nami miaka ya 80 nilikuwa nikiishi kule nguzo sita kwa binti Konyaki, baadaye tuliamia hapo jirani na uwanja wa Jamuhuri ni mtoto wa armaarufu Mzee Shombe(r.i.p) Wilaya yetu,ni ya miaka mingi mno imedumaa sana wakati wilaya nyingine zimishapandishwa adhi!Wana Kls kwa sasa napatikana kanda ya Ziwa kwa masuala ya uvuvi na madini(dhahabu)nione nitakupokea.Hapo mtendeni nimepotezana na mwanangu wa kiume, si unajua tena mambo ya ujana, tuwasiliane 0789554955.
kwakina Ally Shombe?
 
Back
Top Bottom