Update: Rais Magufuli atazikwa Machi 26, 2021

Update: Rais Magufuli atazikwa Machi 26, 2021

Visiwani walishamzika maalim seif inatosha
Zbar walio wengi ni Waislamu na huwa hawaagi. Leo hii Magu ndio WA kuhangaishwa hivyo? . Tuombe alazwe salama maana maisha ya MTU huwa yanamfuata hata akiondoka dunia hii.😔😔😔
 
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli atazikwa nyumbani kwao Chato Machi 26, tofauti na tarehe iliyotajwa awali ambayo ilikuwa Machi 25.

Mwili wa Rais Magufuli utaagwa na wananchi wa Dar, Machi 20 na 21 Uwanja wa Uhuru kabla ya kusafirishwa kwenda Dodoma ambapo utaagwa Machi 22.

Baada ya Dodoma mwili utapelekwa Zanzibar ambao watapata nafasi ya kuaga Machi 23. Kisha utaelekea Mwanza ambapo wataaga Machi 24.

Ukitoka Mwanza, mwili wa Rais Magufuli utapelekwa Chato ambapo utaagwa Machi 25. Kisha Machi 26 itakuwa siku ya Mazishi huko Chato Mkoani Geita.
Ile public holiday nayo inahamia tarehe 26? Wanakurupuka sana hawa watu
 
Hii yote ni njia ya kupiga pesa tu, kitu ambacho marehemu mwenye alikipinga. Waratibu wa safari wanapigia mafundi ujenzi kwenye viwanja vyao waendelee kujenga, maana hapa mpunga mrefu unapigwa. Sitostaajabu bajeti ya mazishi ya raisi kuja kusemwa imetumika trilioni kadhaa.
Dar kwenda ZNZ ni karibu zaidi, kwanini wasimpeleke Zanzibar halafu ndio Dodoma. Lakini wao wanamzungusha mpaka Dodoma halafu wanamrudisha nyuma tena kwenda Zanzibar.
Kama marehemu angeweza jisemea angeamuru azikwe hata leo.
 
Huu utaratibu wa kutembeza jeneza kama bidhaa, ni wa hovyobkabisa. Hiki kinachofanyika ni waliowazima wanamuaga marehemu au marehemu anawaaga walio hai?

Kawaida ni walio hai kumfuata marehemu kumuaga, siyo marehemu kumwendea kila mmoja aliko.

Huku ni kuwasumbua wafiwa. Hatukufanya hivyo kwa Karume, Sokoine, Mkapa wala Mwalimu Nyerere.
 
Huu ni ushamba unaoendelea kwenye ile timu yake ya Praise & Worship au MATAGA
 
Ni yale yale ya utumiaji mbaya wa rasilimali za nchi. Mtu ameshakufa wanamuagaje wakati yeye hayuko hai tena?

Hizi kweli ni mbinu tu za watu kupiga pesa sasa kutembezwa huko kote maana yake nini. Ni ufisadi tu wanafanya.
 
Ndio mjuu bado utawala huu ni mauza uza. Sasa visiwani anapelekwa kufanya nini?

Huyu azikwe leo leo mtasababisha afufuke.
Umefikia kiwango kibaya kabisa cha chuki.Chuki humla yeye aliyeibeba, bali wema humneemesha yeye aliyeibeba.
 
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli atazikwa nyumbani kwao Chato Machi 26, tofauti na tarehe iliyotajwa awali ambayo ilikuwa Machi 25.

Mwili wa Rais Magufuli utaagwa na wananchi wa Dar, Machi 20 na 21 Uwanja wa Uhuru kabla ya kusafirishwa kwenda Dodoma ambapo utaagwa Machi 22.

Baada ya Dodoma mwili utapelekwa Zanzibar ambao watapata nafasi ya kuaga Machi 23. Kisha utaelekea Mwanza ambapo wataaga Machi 24.

Ukitoka Mwanza, mwili wa Rais Magufuli utapelekwa Chato ambapo utaagwa Machi 25. Kisha Machi 26 itakuwa siku ya Mazishi huko Chato Mkoani Geita.
Duh! Mbona mnausumbua mwili wa marehemu hivyo, yani mwili mnaukimbiza kama mwenge?
Sijui lengo ni nini hapa, lakini kwangu hii sio sawa
Enewei kama ndio protokali fanyeni tu
 
Back
Top Bottom