Update: Rais Magufuli atazikwa Machi 26, 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,828
2,000
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli atazikwa nyumbani kwao Chato Machi 26, tofauti na tarehe iliyotajwa awali ambayo ilikuwa Machi 25.

Mwili wa Rais Magufuli utaagwa na wananchi wa Dar, Machi 20 na 21 Uwanja wa Uhuru kabla ya kusafirishwa kwenda Dodoma ambapo utaagwa Machi 22.

Baada ya Dodoma mwili utapelekwa Zanzibar ambao watapata nafasi ya kuaga Machi 23. Kisha utaelekea Mwanza ambapo wataaga Machi 24.

Ukitoka Mwanza, mwili wa Rais Magufuli utapelekwa Chato ambapo utaagwa Machi 25. Kisha Machi 26 itakuwa siku ya Mazishi huko Chato Mkoani Geita.
 

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,000
2,000
Zanzibar pia ni sehemu ya JMT, fair decision.
Ilisahaulika?

VP alisema nchi itaomboleza kwa siku 14
Mwenezi akasema chama kitaomboleza Siku 21
Raisi akasema nchi itaomboleza siku 21

Raisi akasema Hayati Jemedari atazikwa target 25/03
Siku nano kasema kuwa atazikwa tarehe 26/03

VP alisema ugonjwa uliomuondoa mwamba alikuwa nao kwa miaka 10.
Rekodi zinasema alifanyia upasuaji wa moyo akiwa anasoma uzamili, ambapo ni kabila ya 1995.

Ni mwanzo wa namna gani huu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom