Upanuzi wa Barabara ya Morocco - Mwenge umelenga nini?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,305
12,600
Morocco/Victoria hadi Mwenge ni kipande kifupi sana kuhitajii kupanuliwa kuwa njia 8 kwakuwa kinaunganisha barabara nyembamba za Mwenge kwenda Tangi bovu na Sam nujoma ambazo ni njia NNE zote. Hivyo magari yatapita mengi na kwenda kujazana Mwenge au kutoka Mwenge na kwenda kujazana Morocco.

Barabara ile ni heri ingejengwa barabara ya Nyerere kutoka Airport kuja Dar center, au barabara ya mandera kwenda bandarini.
 
Haueleweki mkuu
Wenzio wameelewa. Hivi unaweza kufunga bomba dogo kutoka chanzo cha maji kisha katikati ukaunga kipande cha bomba kubwa halafu mbele yake tena ukaunga kipande cha bomba Dogo, hayo maji yata flow vipi. Mfano, kipande kile kina pitisha sasa kwa wingi na speed magari mengi kutoka posta, mwananyamala, kinondoni, na Mikocheni kuelekea Mwenge kwa kuungana na magari ya kutoka makumbusho, lakini yakifika pale Mwenge njia sio kubwa kama iliyoyaleta hivyo kusababisha foleni. Je, asieleweka ni mimi au ni wewe?
 
Ule ni Mwanzo tu lakini huku kwingine kutazidi kupanuliwa mfano Mwenge hadi Bunju badae hadi Bagamoyo. N.k
 
Morocco/Victoria hadi Mwenge ni kipande kifupi sana kuhitajii kupanuliwa kuwa njia 8 kwakuwa kinaunganisha barabara nyembamba za Mwenge kwenda Tangi bovu na Sam nujoma ambazo ni njia NNE zote. Hivyo magari yatapita mengi na kwenda kujazana Mwenge au kutoka Mwenge Na kwenda kujazana Morocco.

Barabara ile ni heri ingejengwa barabara ya Nyerere kutoka Airport kuja Dar center, au barabara ya mandera kwenda bandarini.
Hio ni njia nne kama Mwenge tanki bovu, hapo katikati ni njia ya mwendokasi ambayo pia itajengwa Mwenge -tanki bovu
 
Dogo labda akili yako inawaza hapa hapa 2021!.

Wale wa mbagara nao walikuwa na mawazo kama yako wkt wa upanuzi wa ile barabara but leo unaona kinachofanyika kule from pale gerezani.

Hapo kati ni maandalizi ya BRT ikitoka kivukoni au gerezani haitaishia morocco bali inaunga cross Sam Nujoma kurudi town na nyingine direct tegeta sokoni.

Soon utarudi Dar wewe, si ulikimbilia Dodoma kisa makao makuu 😁!.
 
Hahaha, hujanishawishi bado, kama lengo lingekuwa BRT basi mradi huu usingekuwa Morocco-Mwenge, ungekuwa Morocco - Tegeta watu wangeelewa. Kama malengo ni BRT ya Morocco hadi Tegeta ambayo haijulikani ujenzi utaanza lini kwanini barabara ya Morocco - Mwenge ambayo pia ilikuwa njia nne kwanini ipanuliwe na watu kubomolewa nyumba zao leo? Kuna uharaka gani? Kwanini hiyo hela isingekwenda kuchimba mabwawa ya maji kwa wasiokuwa na maji leo tangu uhuru? Nani anapanga vipaumbele vyetu?
 
Sijaandika nikushawishi wewe as mdogo wangu bali nimeandika kukupa muelekeo wa kile kinachokuja.

Pia shule uliyosoma ndiyo chanzo cha kutoelewa kinachoandikwa as, nimeandika neno (maandalizi) hapo ndipo shida ilipoanzia. Pole.
 
Morocco/Victoria hadi Mwenge ni kipande kifupi sana kuhitajii kupanuliwa kuwa njia 8 kwakuwa kinaunganisha barabara nyembamba za Mwenge kwenda Tangi bovu na Sam nujoma ambazo ni njia NNE zote. Hivyo magari yatapita mengi na kwenda kujazana Mwenge au kutoka Mwenge Na kwenda kujazana Morocco.

Barabara ile ni heri ingejengwa barabara ya Nyerere kutoka Airport kuja Dar center, au barabara ya mandera kwenda bandarini.
Barabara yenyewe toka 2016 haiishi
 
Njia zimepungua toka 5 hadi 4 halafu unasema wamepanua? Umechanganyikiwa?
 
Mi kinachonishangaza ni muda unaotumika kujenga kipande kifupi kama hicho.
Ikumbukwe sherehe za uhuru za mwaka 2015 zilifutwa na hela zake zikaigizwa kwenye ujenzi huo.
Tangu uhai wa rais wa 5, mpaka sasa barabara hiyo bado inajengwa!!
Wajuvi mtuambie, kuna nini cha ziada hapo mpaka inatumika miaka zaidi ya mitano sasa kujenga kipande kifupi kama hicho!?
 
Back
Top Bottom