Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?


Umejuaje kama JWTZ hawakua na majasusi wao wa MI?

Au mpaka waje kwenye vyombo vya habari kukuhadithia?

Acha ujinga
 
Kasome riwaya ya Mimi na rais.
 
Swali zuri
 
Eti TPDF anasubiri tuvamiwe ndiyo aingie kazini 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ila umesema kweli 😁😁😁😁
 
Ubaya mwingine ni unaweza kusacrifice maisha yako kwa mission ulio ifanikisha mwenyewe..pia wanamaisha magumu sana sababu inawachukua mda mrefu kuishi maisha ambayo sio halisi
Duh! Ila kazi ni kazi tu, kikubwa mkono uende kinywani.
 
Kwa utawala wa Magufuli na Samia, nimeamini TISS ni watu wa kawaida mnoo...

Tuwaheshimu JWTZ wanaolinda mipaka na kuwafanya viongozi hawa kujawa na kiburi...

Tunahitaji mageuzi makubwa mno kwenye taasisi hii
Kumbe na wewe upo humo? Fanyeni mageuzi sasa mpaka mtutangazie huku?
 
Kiinchi hiki ngwengwe tupu..
Lakini mnakijadili kuhusu usalama wa taifa utadhani kina uwezo wa kinyukilia yaani upupu mtupu.
hawa njaa kali wanalinda nini?
upuuzi mtupu tu, sanasana wanafuatafuata vijichama vya upinzani ambako hawana chochote yaani mnachosha kweli kupoteza muda kujadili utopolo kama huu
Hakuna usalama wa taifa wala nini, eti hawalali, wanalinda masaa 24, hebu acheni upuuzi
Vitambi vitupu vimejaa kwenye kaunda suti...
 
Watakutafuta
 
Mods huyu si mpige life ban tu 😝😝
 
Nina hakika Nina na uhakika kabisa yakuwa nitakacho kisema Leo nitarukiwa na kushukiwa kama mwewe na mijitu inayo itwa Usalama wa TAIFA na mawakala wao kimsingi Hali ya ufisadi katika TAIFA inazidi kuwa mbaya mbaya mbaya na watu wanao takiwa kuchunguza na kubaini upuuzi HUU wapo na wanalipwa mishahara mikubwa tu.

Tunaambiwa na mkaguzi halimasharu zetu kalibia mamlaka 188 zimetoa Bilioni 88 zimepotea Kwenye mikopo ya vikundi nataka niseme hakuna Halimashauri ambayo Haina vijana wetu wa Usalama wa TAIFA wapo na wanao uwezo wa kuchunguza kama fedha za umma zimepelekwa kwa vikundi kweli au ni hewa nasema hivi maana niliwai Kuta mfano wilaya ya mreba tu, mikopo zaidi ya milioni 60m ipo mikononi mwa vijana wawili na wake zao na hao vijana ni marafiki wakubwa wa hao vijana wetu wanapika wanakunywa pamoja na taarifa wanazo lakini wao wanaahindwa kulipoti ilo tu Kwa idara usika?

HUU wizi tunao ambiwa unajitokeza Nina Imani tunao.vijana wetu pendwa Kwenye mawizara na taasisi zetu je hao vijana walioko uko wanafanya kazi gani kama wanaahindwa kuripoti mambo kama hayo kabla hayajatokea?

Nilichokibaini ni kuwa vijana tunao ila changamoto je wanauwezo wa kuchunguza na kuhoji dhidi ya wizi huo unapotokea?

Yote haya lazima tukubaliane mfumo wa ajira wa vijana wa idara hii unachangamoto kubwa sana

Kitendo Cha kuajili watoto wa wakubwa, vijana wa umoja wa vijana wa ccm ambao wengi wao ni form four failure ni kosa kubwa sana tuna vijana ambao hawana uwezo mfumo ubadilidilishwe
 
Huwa kila siku tunasema, kama CCM itaendelea kukaa madarakani kwa shuruti, mifumo yetu ya utawala itaendelea kuwa mibovu. Kwa hapa tulipofika maana kansa ya athari ya utawala wa shuruti wa CCM imeshaenea nchi nzima, ni aidha yatokee machafuko tuanze upya, ama serekali ipinduliwe kuwe na kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi mpya wa kidemokrasia ambao hautapendelea chama chochote kama ilivyo sasa.

Vinginevyo hao usalama wa taifa wataendelea kupatikana kwa mchongo ili kulinda huu mfumo wa wizi wa chama cha mapinduzi. Nilishangaa sana uchaguzi wa 2020 idara ya usalama kufuata maelekezo ya rais aliyekuwa madarakani ya kuchezea uchaguzi kwa kiwango cha kutisha. Ikifika mahali ukaona idara ya usalama wa taifa inafuata matakwa binafsi ya kiongozi aliyeko madarakani, ujue hapo hakuna idara ya usalama tena, bali genge hatari la usalama wa taifa. Kwao hao usalama wa taifa wako kuhakikisha CCM haitoki madarakani, kwani ajira zao zinatokana na CCM kuwepo madarakani, na sio uwezo wao wa kazi.
 
Wanasema ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya ccm, sijui kama ni kweli...
Na pia vijana wanaofanyiwa recruitment na idara Wana personal relationship na high profile figures wa hii nchi.. just vidokezo TU na mwana mmoja kanipa.

Hilo liko wazi, usalama huu wa taifa uko kulingana na utashi wa watawala walioko madarakani. Na hili limechangiwa na katiba inayomfanya rais kuwa mungu mtu. Ukiangalia ni taasisi iliyoundwa kulingana na mitazamo ya rais aliyekuwa madarakani wakati wa kutungwa kwa hiyo sheria.

Kutokana na udhaifu wa muundo wake, rais anaweza kuagiza wafanye chochote atakacho iwe ni kwa maslahi yake binafsi, au ya chama chake, na sio lazima iwe kwa maslahi ya taifa na watafanya. Tazama hiyo idara ya usalama wa taifa, huwa inafanya kazi kulingana na utashi wa rais anayekuwa madarakani, na sio sheria zitakavyo.
 

Very true

Pale bandarini wamejaa tiss kila kona but wizi ndio kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…