Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,275
6,621
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza

Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye eneo la mwisho ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika, kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.

Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini je tumeangalia nini athari yake?

Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza hayo majukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?

NAULIZA TU.
 
Athari ni pamoja na kufa taratibu kwa kuyajua mabaya mengi yanayoisumbua nchi na huna la kufanya zaidi ya kumweleza mkurugenzi mkuu na mfadhili. Ni mbaya sana kujua kisa na njia ya kukimaliza lakini huwezi tenda.

Lazima ufe kwa kihoro. Suluhisho: Ulevi na Umalaya
 
Kwani TISS ni kazi mzuri kuliko JWTZ
Ni mbaya kuliko JWTZ @ TPDF kwani wapo kazini saa 24 kwa siku saba. Pia hamjui adui na anatakiwa amfahamu kiundani hasa. Hana adui maalum kwani yote yake mradi usalama wa taifa uwe salama. Tiss personnel are supposed to detect and eliminate in covert and/or clandestine way any threat to national security.

Huo ndio ubaya wa TISS. TPDF anasubiri tuvamiwe ndo aingie kazini.
 
Athari ni pamoja na kufa taratibu kwa kuyajua mabaya mengi yanayoisumbua nchi na huna la kufanya zaidi ya kumweleza mkurugenzi mkuu na mfadhili. Ni mbaya sana kujua kisa na njia ya kukimaliza lakini huwezi tenda.

Lazima ufe kwa kihoro. Suluhisho: Ulevi na Umalaya
Hawa jamaa ni kweli wanapenda sana chini.
 
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza

Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya
KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu
ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia
ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja
kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye
eneo la mwisho la ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika,
kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa
Kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.

Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia
ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu
bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio
wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini
je tumeangalia nini athari yake?

Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama
wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje
(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye
Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu
kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza
hayo majuukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa
Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa
ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee
aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?

NAULIZA TU.

Thread yako natabiri itakufa kifo cha mende, ,japo kuna hoja ndani yake
 
Ni mbaya kuliko JWTZ @ TPDF kwani wapo kazini saa 24 kwa siku saba. Pia hamjui adui na anatakiwa amfahamu kiundani hasa. Hana adui maalum kwani yote yake mradi usalama wa taifa uwe salama. Tiss personnel are supposed to detect and eliminate in covert and/or clandestine way any threat to national security.

Huo ndio ubaya wa TISS. TPDF anasubiri tuvamiwe ndo aingie kazini.

Jeshi muda wote WaPo kazini mkuu,,iyo ya kusema wanasubiri hadi sijui kuvamiwa labda kwa nchi km uswisi huko, ,, lkn kwa sisi ambao tunapakana na nchi zenye makundi ya waasi, ,muda mwingi Jeshi letu Lipo mchakamchaka
 
Wengi wanaishia kwenye Pombe na Umalaya tu.Kuna kipindi nilikua na wakuu wakitengo maeneo flani walinchukua tukatembee nipate kujua maeneo kidogo ila cha kushangaza walipiga bia kama 19 kila MTU ila mmoja alizidiwa na kuanza kuropoka mission zao na majukumu waliyoyakamilisha Nilijifanya siwaelewi ila mmoja akabadili story kwa staili yaaina yake by that time nilikua napata soft drinks na kiepe changu.Mpaka sasa mmoja ananitaftaga sana kunifanya niwe karibu
 
Wengine wanashinda majumba ya Ibada kama waumini.
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom