FDR.Jr
JF-Expert Member
- Jun 17, 2008
- 1,359
- 357
Sina tatizo na namba moja hapo juu, tatizo langu linaanzia namba mbili pale uliposema "ilimradi yana maslaha kwa taifa" hapo nina tatizo kidogo. ukiangalia tokea huko nyuma alipokuwa anasimamia kitengo cha maafa na kujinufaisha (maslahi binafsi - hapo simtofautishi na mtu anayewakwapua majeruhi wa ajali) na alipokuwa waziri mwenye dhamana ya nyumba na ardhi - madudu aliyofanya, kwa kifupi tumwamini Nyerere aliyemwona moja kwa moja kwamba hafai uongozi ngazi ya juu. anachapa kazi kweli, lakini kuelekea wapi?
Tuangalie hili la shule za kata. sikatai kwamba mapinduzi yanahitaji nguvu kubwa, lakini kitu chochote katika ngazi hiyo kinahitaji umakini wa hali ya juu. maslahi ya taifa yanakudai ufanye jambo jema ambalo linadumu na linahitaji muda mrefu kutekeleza. maslahi ya kweli ya taifa humgharimu yule anayeyasimamia. sifa ni mara chache kwenda kwake maana yanaweza kukamilika wakati yeye hayuko madarakani.
mkakati wa kweli wa kuinua elimu Tanzania haiwezekani utekelezwe kwa staili hii ya shule za kata. kulikuwa na shinikizo kubwa la kisiasa, na kuburuzana. huwezi kufanya jambo kubwa linalodai kushirikisha wataalamu na wadau wengine wa elimu, kwa kuwaburuza. nani atatekeleza au kusimamia utekelezaji? tunahitaji phase one, two three, inayoeleweka.
Lowasa anachapa kazi kwa msingi wa populism, kujitafutia sifa za haraka haraka kwa maslahi binafsi. tunahitaji wachapa kazi ndio, lakini si kwa staili ya Lowasa.
TATIZO HAPO NI KWAMBA LOWASSA YUKO WAZI SANA WHEN IT COMES KERO, HANA TOFAUTI NA MAGUFULI KTK ENEO HILO, HAWEZI KUMUITA MBUZI -NG'OMBE HATA KAMA WOTE WANATOA MAZIWA NA WANA PEMBE ATAMUITA MBUZI KWA WASIFU WA MBUZI. HAJIKWEZI BALI ANAJUA THAMANI YA MAMLAKA ALIYOMO, WAKATI NA NINI AFANYE ILI KUJIBU KIU NA MATARAJIO YA UMMA LAKINI ZAIDI ANAPENDA KURITHISHA AU KUELEKEZA JAMII KUTII MAMLAKA ZAO.
Hilo la tatu ndio kabisaaa, Lowasa hawezi kutufikisha pale tunapohitaji. kujiuzulu kwake kwa kashfa ni kielelezo tosha cha utendaji wake. kwa support aliyokuwa toka kwa JK, aliwezaje kudondoka? ni wazi maji yalifuata mkondo. na kashfa iliyomwangusha bado ndio kwanza inarindima, na inanuka jitihada kubwa za ngazi za juu kufunika kombe mwanaharamu apite
KUJIUZURU KWAKE NI FUNZO LA UWAJIBIKAJI KTK MAAMUZI UNAYOYAAMINI ULIYAFANYA KWA NIA NJEMA, KAMA KIONGOZI MKUU WA SERIKALI ALIKUWA NA OPTION MBILI, 1. KUKUBALIANA NA MWAKYEMBE'S TEAM KUWA WAKO SAHIHI 100% AND I'M SORRY KWA WANANCHI, BUNGE KWA NIABA YA SERIKALI NA YEYE BINAFSI, BUNGE LINGEJITAFAKARI NA KUJA NA AZIMIO AMBALO 65% LINGEMNUSURU KTK JANGA LA UWAZIRI MKUU.
2. KUIPINGA TEAM YA MWAKYEMBE, KUSIMAMIA MAAMUZI YAKE, KUTOOMBA MSAMAHA KWA WATZ NA BUNGE KWA NIABA YA SERIKALI NA KUCHUKUA MSIMAMO WAKE BINAFSI AMBAO UMEIPA CCM FURSA YA KIUTENDAJI KWA KUMLETA MBADALA WAKE BAADA YA YEYE KU STEP DOWN. AMEFAURU FUNZO LA MWALIMU J.K.NYERERE KUWA UNAPOKUWA KIONGOZI HUPASWI KUWA NA KAULI MBILI AU MISIMAMO MIWILI AU SURA MBILI ZA UONGOZI.... UKIWA HIVYO HUFAIIII...NDIO LINE ALIYOICHUKUA NA NDIO MSINGI WA KUENDELEA KWA MALUMBANO YA RICHMOND NA DOWANS TODATE, NA NDIO MSINGI WA SISI TUNAOAMINI KUWA MH. RAIS ALIFANYA MAKOSA KUKUBALI KUJIUZURU KWA WAZIRI MKUU WAKE KWA IMANI KUWA APATE FURSA YA KUANZA UPYA..... KUMBUKENI KUWA MPAKA SASA SERIKALI YA JAKAYA HAIJAKIRI KUKOSEA KTK ISSUE YA RICHMOND, WANAKIRI UDHARURA WA ISSUE YENYEWE ZAIDI KULIKO TARATIBU....MATOKEO YAKE NI UJIO WA KILIMO KWANZA BAADALA YA ELIMU KWANZA 2005 MISSION........, NDIO MATOKEO YA KUYUMBA KWA UTAWALA WAKE KTK UCHAGUZI HUU ULIOPITA, HAWA WALIKUWA WAMOJA TANGU 1995....... LOWASA WAS LEFT IN 1ST BWM BARAZA BCOZ OF JK CAMPAIGN AGAINST WAZEE WA CCM.........LOWASA ALITULIZANA NA KUTII CHAMA 1997 AKAREJESHWA, 2005 HAKUIGEUKA KAMBI YA RAFIKI YAKE KAMA AKINA MKUCHIKA N.K....
BADO NAAMINI MH.JK MISSES THAT FELLOW WITH WHITE HAIR MNOOOOO....
NDIYE MTU WAKE WA KWELI, WALIOWEZA KUMTENGANISHA NAYE NDIO MAADUI WA LEGACY YA JK NA SIYO LOWASA......
HOFU NI KIVULI CHA LOWASA KWAO WHEN JK ATAKAPOREJEA ZAKE MSOGA KWA MAPUMZIKO BAADA SULUBA NA MATESO ALOYAPATA TOKA KWETU WATZ, SIJUI KAMA HUYU MH. LOWASA ANAMPANGO WA KUMRITHI MH.RAIS J.K KWA NGUVU YOYOTE ILE? KAMA NI UMMA BASI TUUACHIE UFANYE MAAMUZI HAYO WAKATI UKIFIKA ILA KWA SASA TUCHAPE KAZI WAKURU.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
NAOMBA NIAGE KTK HOJA HII KWA NUKUU WATANZANIA WENZANGU "NO ONE INDIVIDUAL IS BIGGER THAN THIS CLUB. THERE NEVER HAS BEEN AND NEVER WILL BE " LIVERPOOL BOSS KENNY DAGLISH (Mie mnazi wa Bwawa la Maini wakuru)