Upande wa pili wa Edward Lowassa

Upande wa pili wa Edward Lowassa

Huo ndo uwezo wako wa kufikiri. Nadhani unatumika kama mipira ya kufanyia ngono then ukimaliza kazi yao wanakutupa tena jalalani.

Laiti ungejua pengine ungekuwa na fikira za ukombozi ili shangazi, babu, bibi na wadogo zako wapate kukombolewa kuliko kutetea fikira za mafisadi kama Lowasa.

Hili neno la Mtu anatumika linatumika vibaya inaaribu sura ya upinzani wa kweli.Inajenga dhana ya kusema uongo tu.Sasa mwaka 2000 hakukuwa na hizo shule za kata angalia jinsi uchaguzi ulivyokuwa umepooza..vijana walikuwa hawaelewi what is going on kadhalika 2005.So sio kila mtu anaeweza kusema zuri la mtu basi anatumika.Ni upumbavu kuwa na fikra kama hizo.Tubaki tukilaumu bape mtu anpokosea lakini pia kama ana jema tuweke visasi na visa pembeni.
 
Ni waziri mkuu pekee kulazishwa kujiuzulu kwa kashfa
ni mwanasiasa fisadi jasiri mwenye vitega uchumi lukuki
hakati tamaa wala hakubaliani na ukweli kwamba watz tulio wengi h a t u m p e n d i

Kweli ni upofu kumisifia mtu kwa mazuri yasiyo na tija wala kuleta manufaa ya wazi au nafuu katika maisha ya mtanzania. Yote hayo yanmezwa na unyonyaji anaoendelea kuwafanyia watanzania wanyonge hawa hata leo kuishi maisha ya utumwa. Maaumuzi mazuri ni kuileta Richmond? Aishie zake!
 
Hallow, Great thinkers!!!!
Pamoja lawama na takataka zote anazotupiwa Edward Lowassa. Pamoja na mabaya yote aliyonayo Edward Lowassa kama mimi na wewe tulivyo na mabaya yetu, tutakuwa hatumtendei haki Edward Lowassa kama tusipo yatangaza mazuri yake.

Kwangu mimi, Edward Lowassa namuona kama
1. kiongozi bora na anayeweza kusimamia maamuzi yake
2. Kiongozi ambaye yupo tayari kuchukua maamuzi mazito hata kama yataudhi wengi ilimradi yana maslaha kwa taifa
3. Kiongozi ambaye anaweza kulifikisha taifa pale tunapohitaji

Baadhi ya mambo makubwa ambayo huwezi kuyataja bila kumtaja Edward Lowassa ni Uthubutu wake wa kuuvunja mkataba kati ya serikali na city water. Ni yeye aliyeasisi na kusimamia mradi wa shule za kata, though hazifanyi vizuri. Ni Edward Lowassa angalau alionesha nia ya kuleta mvua artificial na ninaamini kama Lowassa angeendelea kuwa PM leo hii uwajibikaji serikalini ungekuwa na mkubwa sana.

Nimegusa tu mazuri ya Laigwanani Lowassa, mazuri yapi ya Lowassa unayajua? Yaandike hapa

Sina tatizo na namba moja hapo juu, tatizo langu linaanzia namba mbili pale uliposema "ilimradi yana maslaha kwa taifa" hapo nina tatizo kidogo. ukiangalia tokea huko nyuma alipokuwa anasimamia kitengo cha maafa na kujinufaisha (maslahi binafsi - hapo simtofautishi na mtu anayewakwapua majeruhi wa ajali) na alipokuwa waziri mwenye dhamana ya nyumba na ardhi - madudu aliyofanya, kwa kifupi tumwamini Nyerere aliyemwona moja kwa moja kwamba hafai uongozi ngazi ya juu. anachapa kazi kweli, lakini kuelekea wapi?

Tuangalie hili la shule za kata. sikatai kwamba mapinduzi yanahitaji nguvu kubwa, lakini kitu chochote katika ngazi hiyo kinahitaji umakini wa hali ya juu. maslahi ya taifa yanakudai ufanye jambo jema ambalo linadumu na linahitaji muda mrefu kutekeleza. maslahi ya kweli ya taifa humgharimu yule anayeyasimamia. sifa ni mara chache kwenda kwake maana yanaweza kukamilika wakati yeye hayuko madarakani.

mkakati wa kweli wa kuinua elimu Tanzania haiwezekani utekelezwe kwa staili hii ya shule za kata. kulikuwa na shinikizo kubwa la kisiasa, na kuburuzana. huwezi kufanya jambo kubwa linalodai kushirikisha wataalamu na wadau wengine wa elimu, kwa kuwaburuza. nani atatekeleza au kusimamia utekelezaji? tunahitaji phase one, two three, inayoeleweka.

Lowasa anachapa kazi kwa msingi wa populism, kujitafutia sifa za haraka haraka kwa maslahi binafsi. tunahitaji wachapa kazi ndio, lakini si kwa staili ya Lowasa.

Hilo la tatu ndio kabisaaa, Lowasa hawezi kutufikisha pale tunapohitaji. kujiuzulu kwake kwa kashfa ni kielelezo tosha cha utendaji wake. kwa support aliyokuwa toka kwa JK, aliwezaje kudondoka? ni wazi maji yalifuata mkondo. na kashfa iliyomwangusha bado ndio kwanza inarindima, na inanuka jitihada kubwa za ngazi za juu kufunika kombe mwanaharamu apite
 
Usisahau kuwa Kama alivyo Jakaya Kikwete, Edward Lowassa naye ni rafiki wa karibu wa Rostam Aziz.

Lakini Pia tusisahau haya kutoka Ripoti ya Kamati ya Harrison Mwakyembe:
 
Usisahau kuwa Kama alivyo Jakaya Kikwete, Edward Lowassa naye ni rafiki wa karibu wa Rostam Aziz.

Lakini Pia tusisahau haya kutoka Ripoti ya Kamati ya Harrison Mwakyembe:
 
Lowassa ana upande mmoja tu, nao ni pesa pesa pesa pesa!! Kwa hilo anaweza kufanya kila analaoweza kufikia malengo yake.
 
Crap!

Mambo mazuri ninayoyajua kuhusu Edward Lowassa:

1. Kiongozi mbovu anayeweza kusimamia maamuzi yake binafsi kibinafsi-binafsi bila kujali wengine. Mfano ni kujitajirisha yeye binafsi kwa rasilimali za Watanzania wote bila kuwajali Watanzania wengine ambao nao wanahaki ya kufaidi rasilimali hizo za nchi

2. Kiongozi ambaye yuko tayari kuchukua maamuzi mabovu hata kama maamuzi hayo yataathiri uchumi wa nchi. Mfano kusimamia Baraza la Mawaziri kuidhinisha kuingiza nchini kampuni ya mfukoni ya Richmonduli iliyozaa Dowans, mambo ambayo yanaleta matatizo makubwa katika uendeshaji wa nchi na yanaleta umaskini mkubwa miongoni mwa Watanzania.

3. Kiongozi ambaye amelifikisha taifa mahali lilipo sasa: serikali kulaumiwa na kulaaniwa na wananchi kuliko wakati wowote, serikali kudaiwa fidia ya mabilioni ya shilingi na kampuni ambayo hata wamiliki wake hawajulikani

4. Jamaa asiye ha haya wala aibu kuusaka urais wa nchi 2015 akidhani kwamba Watanzania ni wapumbavu ki-viiiiiiiile. Mfano ni harakati za kutumia UVCCM kutaka ishu ya Richmond irudishwe Bungeni ili kujisafishia nyota kwa nguvu za pesa ambazo atahonga watoa hoja kipindi cha mjadala

Ver well said Ng'wana o Ng'wise
 
mimi namsifu kitu kimoja ni jasiri asiye na aibu wala soni amejimilikisha mali nyingi sana kwa kutumi vyeo bila halali na kwa halali.
kifupi mwizi ni mwizi tuuu.
 
hallow, great thinkers!!!!
Pamoja lawama na takataka zote anazotupiwa edward lowassa. Pamoja na mabaya yote aliyonayo edward lowassa kama mimi na wewe tulivyo na mabaya yetu, tutakuwa hatumtendei haki edward lowassa kama tusipo yatangaza mazuri yake.

Kwangu mimi, edward lowassa namuona kama
1. Kiongozi bora na anayeweza kusimamia maamuzi yake
2. Kiongozi ambaye yupo tayari kuchukua maamuzi mazito hata kama yataudhi wengi ilimradi yana maslaha kwa taifa
3. Kiongozi ambaye anaweza kulifikisha taifa pale tunapohitaji

baadhi ya mambo makubwa ambayo huwezi kuyataja bila kumtaja edward lowassa ni uthubutu wake wa kuuvunja mkataba kati ya serikali na city water. Ni yeye aliyeasisi na kusimamia mradi wa shule za kata, though hazifanyi vizuri. Ni edward lowassa angalau alionesha nia ya kuleta mvua artificial na ninaamini kama lowassa angeendelea kuwa pm leo hii uwajibikaji serikalini ungekuwa na mkubwa sana.

Nimegusa tu mazuri ya laigwanani lowassa, mazuri yapi ya lowassa unayajua? Yaandike hapa
4. Ni kiongozi ambaye si mdini na hayuko tayari kusukumwa wala kushawishi kupitia mlango dini ili akubalike.
5. Ni rafiki anayeamini ktk kumpenda na kumtetea rafiki ktk hali yoyote aili muradi ajiridhishe kuwa umetenda kwa nia njema
6. Hayumbi katika maamuzi yake hata kama jamii yote inamuona amekosea na yuko tayari kuibeba gharama ya maamuzi yake.
7.si mnafiki, si muoga, anapenda kuogopwa ktk mamlaka yake, anaheshimu mamlaka za wengine, wazee, vijana na ni mkweli ktk matendo ya maisha yake binafsi, biashara na siasa.
8. Ana maono na yuko tayari kuishi ktk kupigania maono yake binafsi na umma.
9.mjasiria mali anayependa kuwekeza ndani ya nchi.
10.siyo mtu wa kijiweni.....

Kiongozi bora ni yule asiyetengeneza marafiki wapya mara baada ya kuyakwaa mamlaka..... Lowasa ndivyo alivyo.....hana marafiki wapya............
 
Todate ndie mwana ccm pekee aliyepingana na dhana ya kilimo kwanza, yeye anasisitiza sana kuwa "elimu kwanza" ktk hili la elimu/kilimo sioni cdm ,cuf, nccr na uvccm wakitupatia dira sahihi kwa hoja zaidi ya lowasa.

Kumbukeni baada ya bunge la samwel sitta dan tido mhando aliwagonganisha vichwa pinda na lowasa ktk jambo hili, lowasa huku akijua msimamo wa serikali juu lipi lianze yeye alilipinga la kuanza na kilimo tena ni baada ya rais kuhutubia kuvunja bunge.........

Kwa hiyo ninaungana na wale wanaikubali hoja hii ya mwenye mada kuwa hata kama tunamuona kachafuka bado anabaki ring leader kimaono ktk awamu hii tuliomo.
Nasisitiza , "aliyekosea ni yule aliyethubutu na asiyekosea ni yule ambaye hajathubutu" huwezi kukosea kama hujatenda lolote ktk uhai wako........
 
Hallow, Great thinkers!!!!
Pamoja lawama na takataka zote anazotupiwa Edward Lowassa. Pamoja na mabaya yote aliyonayo Edward Lowassa kama mimi na wewe tulivyo na mabaya yetu, tutakuwa hatumtendei haki Edward Lowassa kama tusipo yatangaza mazuri yake.

Kwangu mimi, Edward Lowassa namuona kama
1. kiongozi bora na anayeweza kusimamia maamuzi yake
2. Kiongozi ambaye yupo tayari kuchukua maamuzi mazito hata kama yataudhi wengi ilimradi yana maslaha kwa taifa
3. Kiongozi ambaye anaweza kulifikisha taifa pale tunapohitaji

Baadhi ya mambo makubwa ambayo huwezi kuyataja bila kumtaja Edward Lowassa ni Uthubutu wake wa kuuvunja mkataba kati ya serikali na city water. Ni yeye aliyeasisi na kusimamia mradi wa shule za kata, though hazifanyi vizuri. Ni Edward Lowassa angalau alionesha nia ya kuleta mvua artificial na ninaamini kama Lowassa angeendelea kuwa PM leo hii uwajibikaji serikalini ungekuwa na mkubwa sana.

Nimegusa tu mazuri ya Laigwanani Lowassa, mazuri yapi ya Lowassa unayajua? Yaandike hapa

Nampongeza sana kwa jitihada zake za kuutafuta uongozi,hata kwa kuwatumia wale anaoona ni changamoto kwake watu wa kuuwa.Majambazi na wataalamu wa kunyonga.kwa hili Sisi wapenda mageuzi tutamkumbuka pale atakapotimiza adhma yake.
 
Mkuu nimekugongea senkis kwa kuifanya siku yangu, Ahsante sana

Ni ajabu na hatari sana kwamba watu wengine wanaangalia walikosimama na hawaoni usawa kelekea mbele. Yaani wanadhani Tz itaongozwa au inahitaji mijitu ile ile.....ndio maana ya hizi pathetic comparisons and statistics.

Forget Lowassa, he's uncleanable; he's as corrupt as JK, RA etc and whatever iota of credibilty he seems to crave the fact to be told is in the new Tz he has no role to play whatsoever. He rather will stand charges to account for his hefty theft and graft he so accomplished to the detriment of Tz. Please convey this message to him....asante
 
mimi namsifu kitu kimoja ni jasiri asiye na aibu wala soni amejimilikisha mali nyingi sana kwa kutumi vyeo bila halali na kwa halali.
kifupi mwizi ni mwizi tuuu.

Jamaa kweli ni jasiri. Si unakumbuka alipokuwa waziri wa ardhi kipindi cha Mwinyi, aliuza open space za mnazi mmoja? Ni nguvu za umma zikatumika kwa wananchi kuandamana na kupinga hilo. Jamaa ninamfagilia sana kwa UJASIRI WA KIFISADI.
 
Ukiwa na mazuri matatu,halafu ukawa na BAYA moja umekwisha !
 
Hallow, Great thinkers!!!!
Pamoja lawama na takataka zote anazotupiwa Edward Lowassa. Pamoja na mabaya yote aliyonayo Edward Lowassa kama mimi na wewe tulivyo na mabaya yetu, tutakuwa hatumtendei haki Edward Lowassa kama tusipo yatangaza mazuri yake.

Kwangu mimi, Edward Lowassa namuona kama
1. kiongozi bora na anayeweza kusimamia maamuzi yake
2. Kiongozi ambaye yupo tayari kuchukua maamuzi mazito hata kama yataudhi wengi ilimradi yana maslaha kwa taifa
3. Kiongozi ambaye anaweza kulifikisha taifa pale tunapohitaji

Baadhi ya mambo makubwa ambayo huwezi kuyataja bila kumtaja Edward Lowassa ni Uthubutu wake wa kuuvunja mkataba kati ya serikali na city water. Ni yeye aliyeasisi na kusimamia mradi wa shule za kata, though hazifanyi vizuri. Ni Edward Lowassa angalau alionesha nia ya kuleta mvua artificial na ninaamini kama Lowassa angeendelea kuwa PM leo hii uwajibikaji serikalini ungekuwa na mkubwa sana.

Nimegusa tu mazuri ya Laigwanani Lowassa, mazuri yapi ya Lowassa unayajua? Yaandike hapa

Kaumza nimeipenda hii topic, Kwasababu umependekeza tuguse mazuri yake tu na mimi ninalo moja.
1.Alikuwa ana uwezo mkubwa wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji waliokuwa chini yake bila woga.
 
Yaani waki team up Lowassa, Slaa na Magufuli mhh muziki munene
 
Back
Top Bottom