Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
CCM ilimpitisha mgombea wa Jimbo la Muhambwe Jamal Tamim, huku wakijua wazi kuwa ni mtuhumiwa wa ujambazi, utekaji wa mabasi na hata uhusika katika biashara ya viungo vya maalbino.
Uamuzi huo umeleta mgawanyiko kati ya wana CCM Kibondo, ambao walio wengi dhamiri zinawakataza kumpigia kampeni mgombea wa chama chao kutokana na sifa zake mbaya.
Hata katika uongozi wa CCM Kibondo, imeonekana kuwa wamemsusia kampeni Bw. Jamal mwenyewe, ambaye nguvu yake kubwa ni pesa zake anazozitumia kwa Rushwa kama alivyofanya kwenye kura za maoni CCM. Katibu wa CCM wa wilaya ya Kibondo amesimaishwa uongozi, na kamati ya CCM wilaya Kibondo imeitwa mkoani Kigoma kuhojiwa tarehe 29 Septemba kwa kile kinachoitwa Kukosa ushirikiano na wagombea wao. Wameitwa na Mwenyekiti wa Mkoa, Mfanyabiashara tajiri Azim Premji, ambaye alimtetea sana Jamal Tamim kwenye kikao cha NEC CCM pamoja na mjumbe mwingine Mfanyabiashara tajiri Abdallah Muhsin Sheni
Mgombea anayeonekana kwenda vizuri Jimbo la Muhambwe ni Felix Mkosamali wa NCCR Mageuzi.
Mzee Ntagazwa anagombea kwa Tiketi ya CHADEMA lakini rekodi yake ya nyuma imemfanya asikubalike sana, na hata kampeni zake haziendi vizuri.