Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 2,286
- 3,018
Nimejaribu kuangalia ratiba ya mechi ya Yanga dhidi ya Belouizdad, nimeshangaa kuona mechi inapigwa saa moja usiku. Hivi kweli mnataka kushinda mechi halafu mnawawekea mazingira rafiki mpinzani wako? Mamelod ni timu kubwa zaidi ya Yanga lakini huwezi kuona wanawachezesha waarabu usiku, bali wanawachezesha kwenye jua kali.
Waangalie hata watani zao Simba, wanaweka mechi zao mchana, sasa timu ya kiarabu unamchezesha mazingira rafiki kwake ili kujipa ugumu zaidi mechi yako.
Waarabu kwao wamezoea kucheza usiku, mechi za mchana kwenye jua huwa hawaziwezi. Kwasasa Dar kuna joto kali sana hivyo kucheza na Belouizdad mchana ingewapa advantage Yanga. Mechi ya Belouizdad dhidi Yanga, Yanga inatakiwa ishinde ndio ijiwekee mazingira mazuri ya kusonga mbele