TP Mazembe vs Pyramids mechi inaanza saa tisa Lubumbashi, Mamelodi mechi zake na Waarabu ni saa tisa. Kwanini Yanga iwe saa 1?

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,872
6,280
Yanga tuna ujinga mwingi sana

Hatujui kama mpira wa africa una fitna zake

Timu zote za weusi zilizowai ku win caf champions league zinajua weakness ya warabu ni jua

Yanga home games zetu tunawaweka waarabu usiku kwenye taa.

CAF hawapangi muda wa home games

Ndiyo maana mazembe ameweka mechi yake na pyramids kesho ianze saa tisa jua kali lubumbashi. Cheki post hapo utaona 15:00 time lubumbashi

Mamelodi kila siku tunaona jinsi anavyocheza na waydad na Al ahly kwenye jua la saa tisa south africa.

Je, yanga tunajua mpira wa Afrika kuliko Mamelodi na mazembe.

Screenshot_20240224-013351_Instagram.jpg
 
Hukutoa taarifa kama hio saa tisa ni kwa saa za Congo ama Tanzania.

Kama mpira kiwango ni kidogo ni kidogo tu, na kama umezidiwa umezidiwa tu.

Kucheza juani si suluhisho katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Nimeweka screen shot from official page ya TP Mazembe.

Page ya tp mazembe imeandika match start 15:00 Lubumbashi time
 
Usiwaige Mazembe

Pengine kabla ya kulaumu ungefanya utafiti, inawezekana Mazembe kucheza katika muda huo ni jadi yao na wala sio kama wameitumia kama mbinu ya kumdhoofisha mpinzani.

Angalia hii ndio time zone yao pale Lubumbashi yani tumewazidi lisaa limoja.

Screenshot_20240224-014451.png

Sasa angalia na muda wa mechi wanaocheza kwenye ligi yao ya ndani.

Utaona karibia mechi zote wamecheza muda huohuo wa saa 9 (kwa masaa ya Lubumbashi)

Screenshot_20240224-014534.png

Isipokuwa game hii ndio imepangwa muda wa saa 8 na nusu.

Screenshot_20240224-014409.png

Sasa kwa takwimu hizo sioni namna yoyote ambayo unaweza kusema Tp Mazembe ametumia ujanja kucheza mechi katika muda huo ili kumdhoofisha mpinzani wakati tunaona ndio muda ambao siku zote amekua akicheza kwenye ligi yao.
 
Nimeweka screen shot from official page ya tp mazembe.

Page ya tp mazembe imeandika match start 15:00 lubumbashi time
Weka picha full mkuu, sio unaweka kama attachment unatuma kwenye email, wengine wavivu ku click.
Screenshot_20240224-013351_Instagram.jpg
 
Usiwaige Mazembe

Pengine kabla ya kulaumu ungefanya utafiti, inawezekana Mazembe kucheza katika muda huo ni jadi yao na wala sio kama wameitumia kama mbinu ya kumdhoofisha mpinzani..

Kwenye page yao wao wameandika saa tisa kwa saa za uwanjani mechi inaanza lubumbashi

Wewe unalazimisha kuweka saa za nchi zingine.

Muda ninao ongelea wa uwanjani nchi ambayo mechi inachezwa
 
Mimi y
We mjomba mgumu kuelewa..

Hio 16:00 google wameonyesha kwa masaa ya Tanzania kwa kuzingatia location ya kifaa.

Ina maana kwa akili za darasa la kwanza kwa Congo hio ni saa 9, na ndicho jamaa kasema.
 
Usiwaige Mazembe

Pengine kabla ya kulaumu ungefanya utafiti, inawezekana Mazembe kucheza katika muda huo ni jadi yao na wala sio kama wameitumia kama mbinu ya kumdhoofisha mpinzani.

Angalia hii ndio time zone yao pale Lubumbashi yani tumewazidi lisaa limoja.

View attachment 2914223

Sasa angalia na muda wa mechi wanaocheza kwenye ligi yao ya ndani.

Utaona karibia mechi zote wamecheza muda huohuo wa saa 9 (kwa masaa ya Lubumbashi)

View attachment 2914224

Isipokuwa game hii ndio imepangwa muda wa saa 8 na nusu.

View attachment 2914225

Sasa kwa takwimu hizo sioni namna yoyote ambayo unaweza kusema Tp Mazembe ametumia ujanja kucheza mechi katika muda huo ili kumdhoofisha mpinzani wakati tunaona ndio muda ambao siku zote amekua akicheza kwenye ligi yao.
Baelezee baambie baelewe
 
Yanga tuna ujinga mwingi sana

Hatujui kama mpira wa africa una fitna zake

Timu zote za weusi zilizowai ku win caf champions league zinajua weakness ya warabu ni jua

Yanga home games zetu tunawaweka waarabu usiku kwenye taa.

CAF hawapangi muda wa home games

Ndiyo maana mazembe ameweka mechi yake na pyramids kesho ianze saa tisa jua kali lubumbashi. Cheki post hapo utaona 15:00 time lubumbashi

Mamelodi kila siku tunaona jinsi anavyocheza na waydad na Al ahly kwenye jua la saa tisa south africa.

Je, yanga tunajua mpira wa Afrika kuliko Mamelodi na mazembe.

View attachment 2914222
Kwahiyo Misri hamna jua?
 
Hakuna visingizio ambavyo vitaiokoa Yanga kuishia hapa ilipo.

Ili Yanga muingie robo fainali mnatakiwa kushinda goli kuanzia 4 kitu ambacho hamuwezi labda mpate bahati ya mtende.

Kushinda tuu mechi ya Leo hakuwapi uhakika wa Kusonga Mbele maana mechi ya Mwisho na Al Ahly sidhani kama mtatoa hata sare.
 
Sidhani ndio nn kitu cha muhimu ni kupata ushindi hizo goli nne unazosema wewe zitapatikana kulingana na mazingira ya mchezo yatakavyokuwa ila muhimu ni ushindi point tatu huwezi jua ya mbele bado kundi lipowazi yeyote atapita
 
Hukutoa taarifa kama hio saa tisa ni kwa saa za Congo ama Tanzania.

Kama mpira kiwango ni kidogo ni kidogo tu, na kama umezidiwa umezidiwa tu.

Kucheza juani si suluhisho katika maendeleo ya mpira wa miguu, nchi nyingi hata ulaya wanacheza usiku.
Epl mechi huwa wanaanza asubuhi ya saa tano kama ni weekend mpaka saa kumi na moja jioni

Mechi za kati ya wiki ndio wanacheza usiku wa saa moja ama saa mbili wakiwapa mashabiki muda wa kuwa wametoka kazini.
 
Sawa je mechi inachezwa physical kwenye jua la saa tisa ama jua la saa kumi ?
Hapa nafkiri kilichofanya mpaka mechi ikubaliwe ni hali ya hewa ya mji husika, kwa maana Lubumbashi ina elevation ya 1200 mita kutoka usawa wa bahari.

ambapo Dar ina elevation ya 50 mita kutoka usawa wa bahari.
Yaani mji hupo juu kwa 1150 kutoka usawa wa bahari.kadri eneo linapokuwa juu kwa mita 100,joto hupungua kwa 0.6
So hapo joto kwao linapungua kwa ((1150÷100)×0.6C⁰) = 7.4⁰C
Wakati huku saa 9 mchana joto ni 32⁰C,Kule saa 9 mchana joto ni 25⁰C.

So CAF huwa hawakubali kizembe,kwani mpira lazima uchezeshwe katika hali ya hewa rafiki.

Nenda hata Mbeya uone kama saa mchana yake ni ya kutesa kama Dar.
 
Back
Top Bottom