Uongozi UWT Taifa Wanena Mazito "Bahati Ndingo Apewe Kura za Kishindo Jimbo la Mbarali"

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda akiambatana na Makamu Mwenyekiti Zainab Shomari wakimuombea kura Mgombea wa CCM Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bahati Ndingo katika Mkutano wa Hadhara Kata ya Ubaruku.

Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara ,Mwenyekiti Chatanda amewaomba Wananchi wa Kata ya Ubaruku na wanambarali kwa ujumla kumpigia kura nyingi na zakishindo kwa Mgombea wa CCM ambaye atahakikisha analeta Maendeleo makubwa zaidi ndani ya Jimbo hilo .

"Mimi pamoja na wenzangu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT tumekaa siku sita katika Wilaya hii ya Mbarali tumeonana na wakina mama na wananchi kwa ujumla wa Wilaya ya Mbarali tumeona Jinsi wananchi wa Mbarali wanavyokipenda Chama chao hivyo hatuna wasiwasi na wanambarali katika kukichagua Chama Cha Mapinduzi"

MWISHO.

WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.01.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.02.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.02(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.03.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.03(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.04(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.04(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.04.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-14 at 22.24.03(2).jpeg
 
Back
Top Bottom