Uongozi UWT Taifa Waridhishwa na Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MWENYEKITI UWT AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA KALIUA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ndugu Mary Chatanda Ametembelea Hospital ya Wilaya ya Kaliua na kuridhishwa na Ujenzi wa Hospital hiyo ambapo ametoa wito Kwa Wananchi na Viongozi kuishi vizuri na watumishi ili watumishi waweze kufanya Kazi zao kwa mujibu wa Taratibu na miongozo ya Wizara ya Afya.

Aidha, Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu. Mary Chatanda na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu. Zainab Shomari wamechangia Milion Moja (1,000,000) kwenye nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Katika Mapokezi ya Msafara wa Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Zainabu Shomari waliambatana na Wajumbe wa NEC UWT Wilayani Kaliua Mkoani Tabora katika muendelezo wa Ziara yao.

Vilevile, Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Mhe. Aloyce Andrew Kwezi ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Viongozi wa UWT Taifa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya Wilaya ya Kaliua.

UWT JESHI LA MAMA
KAZIENDELEE​

 

Attachments

  • F34oJSOaQAAm-fB.jpg
    F34oJSOaQAAm-fB.jpg
    178.4 KB · Views: 2
  • F34oRCWaYAAtAAB.jpg
    F34oRCWaYAAtAAB.jpg
    133.8 KB · Views: 2
  • F34W0tJaYAAO0oU.jpg
    F34W0tJaYAAO0oU.jpg
    69.6 KB · Views: 2
  • F34W2m0aIAAdlGawa.jpg
    F34W2m0aIAAdlGawa.jpg
    101.5 KB · Views: 2
  • F34GXaHWgAA1-us.jpg
    F34GXaHWgAA1-us.jpg
    321.1 KB · Views: 2
  • F34GbciWQAAxJnZ.jpg
    F34GbciWQAAxJnZ.jpg
    303.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom