Mbunge Bahati Ndingo Ateuliwa Kugombea Ubunge Mbarali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mbunge Bahati Ndingo Ateuliwa Kugombea Ubunge Mbarali

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua, Bahati Ndingo kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.

CCM imetangaza mgombea wa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, unaotarajiwa kufanyika Septemba 19 mwaka huu.
Kwa sasa Bahati ni Mbunge wa Viti Maalum CCM, kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Francis Mtega aliyefariki Julai Mosi kwa ajili ya pikipiki na gari jimboni humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa Agosti 17 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema uteuzi huo umefanywa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya,” imesema sehemu ya taarifa iliyotolewa na chama hicho.

Bahati ameteuliwa kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni katika jimbo hilo, akiongoza watia nia 25 waliogombea.

Mbali na jimbo la Mbarali, NEC ilitangaza uchaguzi mdogo wa udiwani kufanyika katika kata sita kutoka Halimshauri nne nchini.

Kata hizo ni pamoja na Nala (Halmashauli ya Jiji Dodoma), Mfaranyaki (Manispaa ya Songea), Mtyangimbole (Madaba), Old Moshi Magharibi (Moshi), Marangu Kitowo (Rombo).

mbunge-pic.jpg
 
Hawa jamaa ulafi upo kwenye damu, yani mbunge anagombea mbunge!

Wananchi kazi kwenu msikubali kudharauliwa kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom